Kamati
ya Ulinzi na Usalama ya Mkoa wa Tabora na Wadaau wa Usafiri
wamependekeza uanzishwaji wa matumizi ya vitabu (log book) kwa magari ya
mizigo ili kudhibiti madereva kusafiri mwendo mrefu bila kupumzika na
hivyo kusababisha ajali kwa magari yao au kugongana uso kwa uso na
magari mengine kutokana na uchovu.
Tamko hilo limetolewa jana wilayani
Igunga na Mkuu wa Mkoa wa Tabora Aggrey Mwanri mara baada ya kikao cha
kujitathimini kwa ajili ya kuja na majibu ya kuondoa ajali za barabarani
mkoani humo.
Mkuu huyo wa Mkoa alisema vitabu hivyo
vitasaidia kuonyesha muda alitoka , mahali alitoka na kama amesafiri
muda mrefu atalazimisha apumzike ili kuepusha ajali.
Alisema malori yamekuwa yakisafiri
mwendo mrefu bila hata dereva wake kupumzika jambo ambalo limesababisha
magari hayo yapate ajali au wakati mwingine yawe chanzo kinachosabisha
ajali katika magari ya abiria.
Mwanri alisema kwa
kulitambua hilo wanaona wakati umefika kwa magari ya mizigo nayo kuwa na
vitabu(log book ) inayoonyesha muda alianza safari katika kituo chake
cha kwanza na muda alipo baada ya kusimamishwa ili kuona kama kweli
amezingatia matawaka ya kitaalamu na sharia ya kutokwenda kasi.
Alisema kitaalamu dereva anatakiwa
aendeshe chombo cha moto kwa muda usiozidi saa nane lakini mara nyingi
madreva wa malori wamekuwa wakiendesha magari yao hata zaidi ya muda huo
jambo ambalo limekuwa kiwasababisha baadhi yao kuendesha huko
wakisinzia na kupelelea gari kukosa mwelekeo.
Mwanri alisema ili kuepukana na hilo
wadau wamependekeza wammiliki wa gari wa ya mizigo ya masafa marefu ni
vema wawe na madereva wawili ili wasaidiane.
Mkuu huyo wa Mkoa alisema hatua
nyingine ambayo wameamua kuichukua ni pamoja na kuongeza askari na
magari ya doria katika barabara kuu ya Igunga, Nzega kwenda Mwanza na
Shinyanga.
Alisema hatua hii inalenga kupambana na
madreva ambao nyakati za usiku wakwenda mwendo mkali kwa sababu ya
kujua kuwa nyakati hizo tochi hazifanyi kazi.
Mwanri aliongeza kuwa Wadau wa usafiri
wameiagiza Wakala wa Barabara Tanzania(TANROADS) mkoani Tabora
kuhakikisha wanaziba mashimo yaliypo katika barabara kuu zote ili
kuondoa uwezekano wa yenyewe kuwa chanzo cha ajali za barabarani.
Aidha alisema kuwa Wadau
wamekuwabaliana kuwa ukaguzi wa madereva na magari katika barabara kuu
zinazopita Mkoani Tabora utakuwa unafanyika kila siku ili
kujihakikishia kama gari linazo breki, taa zifanya kazi vizuri , matari
yako vizuri na dreva ajatumia kilevi.
Alisema hatua hiyo inalenga kujihakikishia kama chombo cha usafiri na dreva wake yuko katika hali nzuri.
Hivi karibuni (4 /4/2018) kulitokea
ajali ambapo basi la abiria Kampuni ya City Boy yenye namba T 983 DCE
iligongana uso kwa uso lori lenye namba T .486 ARB Mitsubishi Fuso
wilayani Igunga na kusababisha watu 12 kufa palepale na mmoja kufia
katika Hospitali ya Rufaa Bugango.
Taarifa za awali zinaoonyesha kuwa
chanzo cha ajali hiyo ni mwendo kasi wa dereva wa Fuso uliosababisha
tairi kupasuka na gari kuhamia upande wa basi. Lori hiyo lilikuwa na
viazi ambavyo lilivitoa Njombe.
Na Tiganya Vincent, Tabora
No comments:
Post a Comment