Baraza Kuu la Shirikisho la Vyama vya Wafanyakazi Tanzania (TUCTA )
jana Jumamosi Aprili 7, 2018 limetoa tamko lenye mambo saba, likiwemo la
kupinga uamuzi wa Serikali kuwafuta kazi watumishi wake wenye elimu ya
darasa la saba.
Akisoma tamko hilo mbele ya wajumbe wa baraza kuu
la TUCTA katika mkutano wa baraza hilo uliofanyika mkoani Morogoro
mwenyekiti wa TUCTA, Tumaini Nyamhokya amesema uamuzi huo wa Serikali si
sahihi na hivyo wametaka watumishi hao kurejeshwa kazini.
Amesema baraza limesikitishwa na uamuzi wa kuwaondoa kazini watumishi wa umma na taasisi zinazopokea ruzuku kutoka serikalini.
Nyamhokya amesema uamuzi huo si wa kisheria ikizingatiwa kuwa watumishi hao waliajiriwa kwa kufuata taratibu halali za ajira.
“Kwa
hiyo TUCTA tunaitaka serikali kutengua uamuzi wake na kuwarudisha
watumishi hao kazini bila kupoteza haki zao za kiutumishi kwa kipindi
chote,” amesema.
Mambo mengine sita yaliyopo katika tamko hilo
wanayotaka yafanyiwe kazi ni; ongezeko la mishahara, kodi ya mishahara
(PAYE), kupandishwa madaraja na vyeo kwa watumishi wa umma, malimbikizo
ya mishahara kwa wafanyakazi na watumishi kwa baadhi ya taasisi,
ucheleweshwaji wa malipo ya wastaafu kwa baadhi ya mifuko ya hifadhi ya
jamii na uamuzi wa Serikali kuunganisha mifuko ya hifadhi ya jamii.
Na Mwananchi
No comments:
Post a Comment