Kamanda wa
Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Kamishna Suleiman Kova amesema
ulinzi utaimarishwa kabla, wakati na baada ya mdahalo maalumu wa Katiba
ulioandaliwa na Taasisi ya Mwalimu Nyerere (MNF), kwenye Ukumbi wa
Mlimani City, Dar es Salaam mzungumzaji mkuu akiwa Mwenyekiti wa
iliyokuwa Tume ya Mabadiliko ya Katiba, Jaji Joseph Warioba.
Hatua ya Kova imekuja baada ya kuibuka kwa vurugu
zilizosababisha kuvunjika mdahalo wa kwanza uliofanyika Novemba 2,
kwenye Hoteli ya Blue Pearl Ubungo, Dar es Salaam. Asante
kwa kutembelea blog hii na endelea kuwa nasi siku zote, kuwa wa kwanza
kupata habari zetu kwa ku-Like page yetu ya facebook kwa ku-click/ bofya
neno Jambo Tz
Kova alisema polisi imejiandaa kwa ulinzi ili
kudhibiti vurugu zozote zitakazotokea pamoja na kuhakikisha usalama wa
washiriki na eneo zima kwa ujumla.
“Mdahalo ule wa kwanza uliovurugwa, hatukuwa na
taarifa nao, lakini huu waandaaji wametupa taarifa hivyo tumejiandaa
kuimarisha ulinzi, ili kuhakikisha amani inatawala katika eneo hilo,”
alisema.
Juzi, Mwenyekiti wa MNF, Joseph Butiku alisema
ofisi yake inaamini kwamba mdahalo huo wa wazi kwa ajili ya Watanzania
wenye mapenzi mema utakuwa wa amani. Alisema uhakika wa usalama katika
mdahalo huo unatokana na kwamba wameshatoa taarifa kwa vyombo vya
usalama.
Alisema mdahalo wa leo ni sehemu tu ya ushiriki wa
mijadala ya umma kuhusu Katiba Inayopendekezwa, ambayo kwa sasa
inaendelea katika maeneo yote ya nchi, ikifanywa na viongozi wa kisiasa,
mashirika ya kijamii na hata watu binafsi katika vyombo mbalimbali vya
habari.
Alisema japokuwa kwa sasa wamepata ukumbi mdogo
unaoweza kuingiza watu 350, watatoa fursa kwa watu kuuliza maswali na
kupata majibu kuhusu vifungu na vipengele mbalimbali vyenye utata
vinavyoyahusu makundi yote ya kijamii ambayo yamepata uwakilishi katika
mapendekezo hayo ya Katiba. Asante
kwa kutembelea blog hii na endelea kuwa nasi siku zote, kuwa wa kwanza
kupata habari zetu kwa ku-Like page yetu ya facebook kwa ku-click/ bofya
neno Jambo Tz
No comments:
Post a Comment