Rais Jakaya Kikwete anatarajiwa kurejea nchini
Jumamosi, Novemba 29 baada ya taratibu za matibabu yake nchini Marekani
kukamilika.
Taarifa ya Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais, Ikulu
ilisema jana kuwa taratibu hizo zilikamilika saa 12 asubuhi jana, baada
ya madaktari bingwa katika Hospitali ya Johns Hopkins kumfanyia hatua
ya mwisho ya tiba.
Hata hivyo, Rais Kikwete ataendelea kupumzika na
kuangaliwa kwenye Hoteli Maalumu inayohusiana na Hospitali ya Johns
Hopkins kwa siku mbili hadi tatu kabla ya kuanza safari ya kurejea
nyumbani.
Rais Kikwete aliondoka nchini Alhamisi ya Novemba
6, 2014, kwenda kufanyiwa uchunguzi wa afya yake lakini madaktari katika
Hospitali ya Johns Hopkins waliamua kumfanyia upasuaji wa tezi dume
Jumamosi ya Novemba 8, 2014.
Taarifa hiyo ilisema Rais Kikwete anaendelea
kuwashukuru Watanzania kwa sala na maombi yao ya kumtakia heri ya kupona
haraka na kurejesha afya njema katika kipindi chote cha ugonjwa wake. Asante
kwa kutembelea blog hii na endelea kuwa nasi siku zote, kuwa wa kwanza
kupata habari zetu kwa ku-Like page yetu ya facebook kwa ku-click/ bofya
neno Jambo Tz
No comments:
Post a Comment