Baadhi ya
Mabaki ya bidhaa zilizoteketea kwa moto katika SOKO la bidhaa za
utamaduni lijulikanalo kwa jina la MT.MERU CURIOS& CRAFTS MARKET
usiku wa kuamkia leo.
Bango la Soko hilo. Asante
kwa kutembelea blog hii na endelea kuwa nasi siku zote, kuwa wa kwanza
kupata habari zetu kwa ku-Like page yetu ya facebook kwa ku-click/ bofya
neno Jambo Tz
Sehemu ya
Wafanyabiashara wa SOKO la bidhaa za utamaduni lijulikanalo kwa jina la
MT.MERU CURIOS & CRAFTS MARKET wakiwa wameduwaa bila kujua la
kufanya mara baada ya Soko hilo kuteketea kwa moto usiku wa kuamkia leo
na kuunguza bidhaa zote za wafanya biashara zililopo katika soko
hilo.
Kaimu Mkuu wa
Mkoa wa Arusha, Magesa Mulongo ameagiza uchunguzi wa kina kufanyika
kufuatia soko la wafanyabiashara wa Vinyago na bidhaa mbalimbali za
kitalii la Maasai Market kuteketea kwa moto.
Mulongo
ambaye alifatana na kamati ya Ulinzi na Usalama alishangaa kuona maduka
hayo ambayo yapo jirani na Kikosi cha Zima Moto kushindwa kuzima moto na
kusababisha hasara kwa wananchi. "Sitakubali kuona uzembe unaendelea
katika mkoa wetu,lazima watu wawajibishwe kwa uzembe hasa Kikosi cha
kuzima moto ambao mko karibu na Ofisi za Chama Cha mapinduzi wilaya
yalipo maduka haya"amesema Mulongo
Chanzo
cha moto bado hakijaweza kufahamika huku maduka hayo yapatayo 188, huku
yakiwa hayajaunganishwa na Umeme kwa lengo la kuepusha hatari ya moto
kwani bidhaa nyingi ni vinyago vinavyotengenezwa kwa mbao. Asante
kwa kutembelea blog hii na endelea kuwa nasi siku zote, kuwa wa kwanza
kupata habari zetu kwa ku-Like page yetu ya facebook kwa ku-click/ bofya
neno Jambo Tz
Habari picha kwa hisani ya woindeshizza blog
No comments:
Post a Comment