NABII wa
Kanisa la The Revelation lililopo Buza Kipera jijini Dar, Yaspi Bendera
amesema uchaguzi mkuu ujao utakuwa balaa kubwa kufuatia maono anayoyaona
wakati akishiriki ibada katika nyakati mbalimbali, Risasi Jumatano
linakupa mkanda kamili.
Nbii wa Kanisa la The Revelation lililopo Buza Kipera jijini Dar, Yaspi Bendera.
Akizungumza
wakati wa ibada kanisani kwake na baadaye na waandishi wetu Novemba 16
mwaka huu, Nabii Yaspi alisema kuna mgongano mkubwa miongoni mwa watu
wanaotajwa kugombea urais, ili kumrithi rais Jakaya Kikwete ambaye
alimwelezea kama kiongozi anayemuona kiroho kila mara.
“Nilimuona
katika maono yangu kama mtu aliye kwenye majaribu makubwa kiroho,
nikaandaa maombi hapa kanisani na tukamuombea kwa muda wa nusu saa na
tunashukuru Mungu hali yake inaendelea vizuri baada ya kufanyiwa
upasuaji wa tezi dume nchini Marekani. Bado namuona akiwa na maumivu
kuanzia sehemu za kiuno, uti wa mgongo na shingoni mwake.
Mhe. Edward Lowasa. Asante
kwa kutembelea blog hii na endelea kuwa nasi siku zote, kuwa wa kwanza
kupata habari zetu kwa ku-Like page yetu ya facebook kwa ku-click/ bofya
neno Jambo Tz
“Hivi
sasa ninapomuombea atasikia moto unawaka na kupita kwenye sehemu hizo na
kuwa mzima kabisa. Tunamuombea baraka na uzima rais ili aweze kukabidhi
madaraka vizuri kwa rais ajae,”alisema Nabii huyo na kuongeza kuwa
alilazimika kumuombea rais ili asipatwe na madhara kwani kama hali hiyo
ingetokea, kungekuwa na vurugu kubwa kuelekea wakati wa Uchaguzi mkuu.
Waandishi
wetu waliokuwa eneo la tukio walimshuhudia Nabii Yaspi akiwa ameshika
picha ya Rais na waumini wake wakizama katika maombi kwa ajili ya Rais
Kikwete huku na walipomaliza alisema tatizo lake limemalizika.
Waziri Mkuu Mizengo Pinda.
Kana
kwamba haitoshi, Nabii huyo alisema baadhi ya wagombea urais wanapita
kwa waganga wa kienyeji lakini akasema hawatafanikiwa kwa kuwa yeye
anaomba Rais ajaye atoke kwa Mungu kwa kuwa yeye atakuwa nyuma ya
mgombea huyo bila kujali chama anachotoka.
Nje ya
ukumbi wa kanisa, Nabii huyo alizungumza na waandishi wetu ambao
walimuuliza kuhusu jinsi anavyoona kuelekea uchaguzi mkuu wa
mwakani.Vipi kuhusu utafiti wa Twaweza
Mwenyekiti wa CUF Prof. Ibrahim Lipumba.
Kuhusu
utafiti uliotolewa hivi karibuni kuhusiana na uchaguzi mkuu kama
ulivyowasilishwa na taasisi ya Twaweza, ambao umewagawa wananchi, Nabii
huyo alisema anaunga mkono kwani umefanywa kwa usahihi kwa vile ndivyo
hata yeye anavyoona.
“Utafiti
umefanywa vizuri na nadhani kila kitu kipo kama kilivyoainishwa, lakini
kama walivyosema wenyewe kwenye ripoti yao, upepo unaweza kubadilika
wakati wowote maana miujiza ya Mungu huja bila kutarajiwa,” alisema.Nani
atashinda Urais?
Wazari wa mambo ya nje Benard Membe.
“Hivi
unauliza swali kama hilo kweli wakati huu? Ripoti iliyotolewa imemaliza
kila kitu na majibu yako wazi kabisa,” alisema nabii huyo bila kutoa
ufafanuzi zaidi.
Utafiti
uliotolewa na taasisi hiyo ya Twaweza uliotolewa hivi karibuni, ulisema
kuwa endapo Uchaguzi mkuu wan chi ungefanyika hivi sasa, Waziri Mkuu wa
zamani, Edward Lowassa angeibuka mshindi, huku akifuatiwa kwa karibu na
Waziri Mkuu wa sasa, Mizengo Pinda na Katibu Mkuu wa Chadema, Dk.
Wilbroad Slaa akiibuka katika nafasi ya tatu. Asante
kwa kutembelea blog hii na endelea kuwa nasi siku zote, kuwa wa kwanza
kupata habari zetu kwa ku-Like page yetu ya facebook kwa ku-click/ bofya
neno Jambo Tz
Na GPL
No comments:
Post a Comment