Walikamatwa
na kikundi cha kigaidi cha kiislam boko Haram kutoka shuleni kwao huko
chibok. Ingawa kunaahadi nyingi kutoka serikali ya Nigeria kwamba
wataokolewa na pia watapewa msaada kutoka dunia nzima lakini mpaka sasa
bado hawajaonekana, ripoti ya mwandishi wa BBC Will Ross kutoka Lagos
inasomwa na Regina Mziwanda
Miezi sita sasa na wasichana 219 bado
wametekwa, ni ushaidi kidogo sana unaojulikana kwa kile kilichotokea
kuhusu wao tangu walipoondolewa katika shule yao ya bweni huko chibok na
boko haram, serikali ya Nigeria imepata wakati mgumu sio tu kuwaokoa
lakini pia kwa kuonesha mwitikio mdogo wa umma..Wazazi wa chibok wameiambia bbc kuwa wameachwa na maneno tu na ahadi zinazovunjwa kwamba watoto wao wa kike watarudi nyumbani hivi karibuni, baba mmoja amesema wanasiasa wamejikita kwenywe uchaguzi wa mwakani ujao zaidi yakuwaokoa watoto wao waliopotea.
Tangu mwezi April vijana wengi wa kike na wa kiume wametekwa nyara na kikundi cha kiislam cha Boko haram ambao wanaongoza mijini na vijijini karibu na mpaka wa Cameroon.
Serikali ya Nigeria imesema jeshi kwa sasa limepata mafanikio dhidi ya vita na boko haram lakini wamezidiwa nguvu kaskazini mashariki ambapo raia hawako salama na maelfu ya watu wamehama makazi yao katika wiki za hivi karibuni. Kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa ku-Like page yetu ya facebook kwa ku-click/ bofya neno Jambo Tz
No comments:
Post a Comment