Kocha mkuu Marcio Maximo ameingia kambini na kikosi cha wachezaji 28
kujiandaa na mchezo huo ambapo kikosi chake kitakua kikifanya mazoezi
katika Uwanja wa Boko – Veterani kila siku kujweka fit kwa kuzisaka
pointi tatu muhimu siku ya jumamosi. Kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa ku-Like page yetu ya facebook kwa ku-click/ bofya neno Jambo Tz
Akiongelea kuhusu maandalizi ya mchezo huo, Maximo amesema anashukuru
vijana wake wote wapo katika hali nzuri kiafya, kifikra na morali ni
hali ya juu kuelekea kwenye Dar Derby siku hiyo jumamosi.
Natambua mechi za wapinzani wa jadi huwa hazitabiriki, ila sisi kama
Yanga tunajiandaa kuhakikisha tunapata ushindi katika mchezo huo dhidi
ya Simba SC siku ya jumamosi, makosa yaliyokuwa yakijitokeza katika
michezo iliyopita tumeshayafanyia kazi” alisema Maximo.
Wachezaji saba waliokuwa kwenye kambi ya timu ya Taifa Tanzania
(Taifa Stars) wameungana na wachezaji wengine leo wakiwa fit kabisa na
hakuna mchezaji majeruhi hali inayompelekea kuwa na kikosi kipana cha
maandalizi.
Wachezaji waliongia kambini kujianda na mchezo huo wa jumamosi ni:
Walinda mlango: Juma Kaseja, Ally Mustafa “Barthez” na Deo Munish “Dida”
Walinzi: Juma Abdul, Salum Telela, Oscar Joshua, Amos Abel,
Edward Charles, Rajab Zahir, Pato Ngonyani, Kelvin Yondani, na Nadir
Haroub “Cannavaro”
Viungo: Mbuyu Twite, Said Juma “Makapu”, Omega Seme, Hamis Thabit, Nizar Khalfani, Issa Ngao na Haruna Niyonzima.
Washambuliaji: Geilson Santos “Jaja”, Andrey Coutinho, Said
Bahanuzi, Hamis Kizza, Saimon Msuva, Mrisho Ngasa, Hussein Javu na
Jerson Tegete Kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa ku-Like page yetu ya facebook kwa ku-click/ bofya neno Jambo Tz
No comments:
Post a Comment