Rais Barack Obama wa Marekani
amesema mauaji ya mwandishi wa habari James Foley raia wa Marekani
aliyeuawa na wapiganaji wa kundi la Kiislam yameishtua dunia.
Obama amesema kitendo hicho ni cha kikatili na
kisichokubalika mbele za Mungu na kwamba ni matokeo ya mawazo duni
yasiyoendana na karne ya sasa.Kauli hiyo ya Rais Obama inakuja huku wazazi wa mwandishi huyo wakielezea kutoridhishwa kwao na hatua zinazochukuliwa na Marekani kutokana na mauaji ya mtoto wao.
Wazazi hao wamesema wakati mwingine waandishi wa habari huru hawathaminiwi katika aki zao hata pale wanapojitolea maisha yao kwa ujira mdogo. Kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa ku-Like page yetu ya facebook kwa ku-click/ bofya neno Jambo Tz
No comments:
Post a Comment