Rais wa
mstaafu wa awamu ya Pili Alhaji Ali Hassan Mwinyi
Rais wa
Awamu ya Pili Alhaji Ali Hassan Mwinyi amesema serikali haijawahi kufuta
Azimio la Arusha kama inavyodaiwa na baadhi ya wananchi, bali ilizimua
azimio hilo kuwapatia viongozi wa kati uwezo wa kumudu makali ya maisha.
"Serikali
haikufuta Azimio la Arusha. Ililizimua azimio hilo kuwapatia viongozi
wa kati kumudu makali ya maisha, lakini baadhi ya viongozi wamekuwa
wakitumia vibaya nafasi hiyo kuvunja sheria ya maadili ya viongozi,"
amesema.
Alhaji
Mwinyi ameeleza hayo leo jijini Dar es Salaam katika semina ya siku moja
ya maandalizi ya sheria ya kudhibiti mgongano wa maslai miongoni mwa
viongozi na watumishi wa umma iliyoandaliwa na Sekretarieti ya Maadili
ya viongozi.
"Baadhi
ya watu wamekuwa wakitumia vibaya nafasi hiyo kuvunja maadili ya
viongozi wa umma kwa kutumia raslimali za umma kujinufaisha. Tabia hii
imewafanya wananchi kutokuwa na imani na viongozi wao," amesema.
Kwa
mujibu wa Alhaji Mwinyi, mgongano wa maslai ini tatizo kubwa nchini
linalotakiwa kuangaliwa kwa umakini vinginevyo baadhi ya viongozi
wataendelea kujinufaisha kwa kutumia nafasi zao kazini.
Kwa
upande wake Kamishna wa Sekretarieti ya Maadili ya viongozi Jaji Salome
Kaganda amesema lengo na makusudi ya mapendekezo ya sheria hii ni kuleta
amani na utulivu wan chi.
Jaji
Kaganda amesema, "mapendekezo ya sheria hii hayalengi kuwafanya viongozi
kuwa maskini, bali kasi yao ya ukwasi iendane na halii halisi ya kipato
chao."
"Sheria
hii itakapopitishwa na ngazi husika, itapunguza ubinafsi wa viongozi
walioko madarakani kujipendelea wenyewe na maeneo wanayotoka," amesema
na kuongeza kuwa, "Lazima kuwepo na hatua uya serikali kurejesha maadili
ya maadili. Kama itazingatiwa na kuheshuimiwa, taifa litafikia
maendeleoo ya haraka yaliyokusudiwa." Kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa ku-Like page yetu ya facebook kwa ku-click/ bofya neno Jambo Tz
No comments:
Post a Comment