Robo tatu ya
wanafunzi waliofaulu kidato cha nne kwa kupata daraja la kwanza hadi la
tatu (Division I – III), wamechaguliwa kujiunga na kidato cha tano. Idadi hiyo ya wanafunzi watakaojiunga katika shule
za Serikali mwaka huu, imeongezeka kutoka 33,683 mwaka jana hadi
kufikia 54, 085 sawa na asilimia 75.6 ya wanafunzi 71,527 wenye sifa ya
kujiunga na kidato cha tano Tanzania Bara.
Akizungumza na waandishi wa habari jana, Naibu
Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu (Tamisemi), Kassim Majaliwa alisema kati ya
waliochaguliwa wavulana ni 31,352 na wasichana ni 22, 733.
“Wanafunzi waliochaguliwa kujiunga na kidato cha
tano 2014 ni kutoka shule za Serikali na zisizo za Serikali.
Kati yao wavulana 14, 826 sawa na asilimia 27.41 wamechaguliwa kusoma masomo ya sayansi na wengine 16, 526 sawa na asilimia 30.5 wamechaguliwa kusoma masomo ya sayansi ya jamii,” alisema. Kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa ku-Like page yetu ya facebook kwa ku-click/ bofya neno Jambo Tz

Alisema wasichana 7,859 sawa na asilimia 14.5
wamechaguliwa kusoma masomo ya sayansi na wengine 14, 874 sawa na
asilimia 27.5 watajiunga na masomo ya sayansi ya jamii.
“Wanafunzi hao wamechaguliwa kujiunga kidato cha
tano katika shule 241 zikiwamo 33 zilizopangiwa wanafunzi kwa mara ya
kwanza mwaka huu,” alisema.
Mbali ya wanafunzi hao wanaojiunga kidato cha tano, Majaliwa alisema wengine 472 watajiunga na vyuo mbalimbali vya ufundi.
Alisema waliochaguliwa wanatakiwa kuripoti katika
shule husika kuanzia Julai 10 na kwamba watatakiwa kufanya hivyo ndani
ya siku 20 vinginevyo nafasi zao zitachukuliwa.
Kuhusu robo ya wanafunzi ambao walifaulu lakini
hawakuchaguliwa, Majaliwa alisema hiyo ilitokana na ufinyu wa nafasi za
shule na kukosa tahasusi (combination).
“Wanafunzi 16,800 wakiwamo watahiniwa wa
kujitegemea 10 waliokuwa na sifa za msingi hawakuchaguliwa. Waliokosa
kuchaguliwa kwa sababu ya ufinyu wa nafasi ni wanafunzi 16, 400 na wale
kutokana na combination ni 400,” alisema.
Kuhusu wanaojiunga na vyuo vya ufundi, Majaliwa
alisema idadi yao imepungua kutoka 530 mwaka jana hadi 472 mwaka huu
kutokana na vyuo hivyo kuanza kudahili wanafunzi wa shahada ya kwanza.
Alisema kati ya hao waliochaguliwa, wavulana ni
355 na wasichana ni 117 na kwamba idadi ya wasichana imeongezeka kwa
wanafunzi watatu kutoka 114 mwaka jana sawa na asilimia 2.63.
“Serikali inatarajia kufanya uchaguzi wa awamu ya pili baada ya kubaini nafasi zitakazokuwa wazi zinazotokana na wanafunzi ambao hawakuripoti awamu ya kwanza na imeweka utaratibu wa kuwapatia nafasi ya kusoma kidato cha tano na cha sita pamoja na stashahada ya elimu wanafunzi wenye sifa,” alisema. Kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa ku-Like page yetu ya facebook kwa ku-click/ bofya neno Jambo Tz
Na Mwananchi

No comments:
Post a Comment