Yaya Toure amekoleza moto
kwenye sakata lake kutaka kuihama Manchester City akisema hajui hadi
sasa atakapokwenda kucheza msimu ujao.
Wakala wa mchezaji huyo, Dimitri Seluk alibainisha
kuwa Yaya anaweza kuondoka kwa sababu anadhani kwamba amekuwa
akichukuliwa kama mtu asiyeheshimika na wamiliki wa klabu hiyo.
Hivyo kwa sasa, Toure ambaye ana miaka 31, hajaamua hatima yake kuhusu klabu atakayochezea msimu ujao.
Alipoulizwa kama anaweza kuichezea klabu nyingine
msimu ujao, alijibu: “Ndio. Hatujui katika soka nini kitatokea. Kamwe
hatuwezi kujua hilo.”
Katika mahojiano maalumu na mtandao wa BE IN
SPORTS, nyota huyo wa timu ya taifa ya Ivory Coast alisema: “Kwa sababu
ya msimu mzuri niliokuwanao klabu ya Man City, kila mtu ananizungumzia
na kila kitu kiko wazi.
“Wakala wangu Dimitri, siku zote amekuwa
akizungumza na watu kwa simu na anajua cha kufanya kwa sababu siku zote
nimekuwa nikimuamini sana.
“Hatujui kesho itakuwaje, lakini kwa sasa akili
yangu iko katika Kombe la Dunia na baada ya kumalizika kwake tutajua
nini kimetokea.”
Toure alisaini mkataba mpya wa miaka minne kuichezezea City Aprili mwaka jana.
Hata hivyo, majaaliwa yake yamebaki kuwa na
mashaka kutokana na wakala wake kuwalaumu wamiliki wa City kwa
kutoonyesha heshima kwa kiungo huyo alipotimiza miaka 31. Tafadhari Like Ukurasa Wetu Wa Facebook Kwa Kubofya/ Click Neno Jambo Tz
No comments:
Post a Comment