Alikuwa akitoa maelezo hayo huku akiwa amemshikilia
mtoto huyo aliyetapakaa uchafu ikiwamo haja kubwa na ndogo alizokuwa
akitoa ndani ya boksi na kusema kwamba mara ya mwisho alimwogesha Julai
mwaka jana.
Morogoro. Mwanamke
aliyetambuliwa kuwa ni Mariamu Said mkazi wa Kiwanja cha Ndege, Morogoro
juzi alishushiwa kipigo na wananchi kutokana na kumficha mtoto wa
marehemu mdogo wake kwenye boksi kwa miaka minne.
Tukio hilo lilitokea juzi saa nne asubuhi baada ya
majirani zake kutoa taarifa kwa Ofisa Mtendaji wa Kata ya Kiwanja cha
Ndege, Dia Zongo kuhusu mtoto huyo, Nasra Rashid, kufichwa ndani ya
boksi tangu akiwa na umri wa miezi tisa. Zongo alisema majirani hao walimweleza pia kuwa jirani yao huyo hamfanyii usafi mtoto huyo wala kumtoa nje.
Baada ya kupata taarifa hizo, Zongo alimtafuta
Mwenyekiti wa Mtaa huo, Tatu Mgagala na kuongozana naye hadi kwenye
nyumba hiyo na kumhoji mwanamke huyo ambaye alikuwa akijibu kwa
kubabaika. Tafadhari Like Ukurasa Wetu Wa Facebook Kwa Kubofya/ Click Neno Jambo Tz
Moja ya maswali aliyoulizwa ni idadi ya watoto
wake na akajibu kuwa ana wawili lakini wakati akiendelea kujibu maswali,
ghafla mtoto huyo alipiga chafya na kuanza kukohoa, hivyo kuwapa
wasiwasi na kuamua kuingia chumbani kwa mwanamke huyo kwa nguvu na
kumkuta mtoto Nasra akiwa ndani ya boksi.
Ofisa mtendaji huyo alisema wakati wakimtoa mtoto
huyo ndani ya nyumba, kundi kubwa la watu waliokuwa na fimbo na mawe
walianza kumshambulia mwanamke huyo na kumlazimu mtendaji kutoa taarifa
polisi. Tafadhari Like Ukurasa Wetu Wa Facebook Kwa Kubofya/ Click Neno Jambo Tz
Alisema muda mfupi baadaye, polisi waliwasili na
kumkamata Mariam na kumpeleka katika ofisi ya kata ambako aliwekwa chini
ya ulinzi. Baadaye aliwekwa rumande katika Kituo Kikuu cha Polisi, Morogoro na mtoto alipelekwa Ofisi za Ustawi wa Jamii.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Morogoro, Leonard Paulo
alisema wanaendelea kukusanya taarifa za tukio hilo ikiwamo matokeo ya
vipimo vya madaktari kuhusu afya ya mtoto huyo kabla ya kuchukua hatua
zaidi.
Kamanda Paulo alisema watuhumiwa hao wanashikiliwa kwa kosa la kumfanyiwa mtoto vitendo vya kikatili.
Hata hivyo, kamanda huyo alisema polisi
wanakadiria kwamba mtoto huyo alianza kufichwa kwenye boksi hilo akiwa
na umri wa mwaka mmoja na nusu.
Utetezi wa Mariam
Alivyonaswa
Baba wa mtoto
Akijibu maswali ya polisi, mwanamke huyo alikiri
kuanza kumlea mtoto huyo tangu akiwa na umri wa miezi tisa baada ya
mama wa mtoto huyo kufariki dunia mwaka 2010.
Pia mtuhumiwa alikiri kwamba mtoto huyo hajawahi kupewa chanjo yoyote wala kupelekwa kliniki.
Alikuwa akitoa maelezo hayo huku akiwa
amemshikilia mtoto huyo aliyetapakaa uchafu ikiwamo haja kubwa na ndogo
alizokuwa akitoa ndani ya boksi na kusema kwamba mara ya mwisho
alimwogesha Julai mwaka jana.
Pia alisema alikuwa akimwekea chakula na maji ndani ya boksi lililokuwa nyuma ya mlango wa chumba.
Mume wa mwanamke huyo, Mtonga Ramadhani anayefanya
biashara katika Soko la Mawenzi, Morogoro ambaye pia anashikiliwa na
polisi, alidai kuwa hakuona sababu ya kutoa taarifa za kufichwa kwa
mtoto huyo kwa sababu hamhusu na wajibu wake ni kutafuta chakula.
Alivyonaswa
Baadhi ya majirani wa mwanamke huyo ambao
hawakutaka kutajwa majina, walisema Mariam alihamia katika nyumba hiyo
mwaka 2010 na hawajawahi kumwona mtoto huyo akitolewa nje wala kufanyiwa
usafi.
Walisema mtoto huyo alibainika baada ya kusikika
akikohoa na kulia nyakati za usiku, jambo lililozua wasiwasi kuwa huenda
mtuhumiwa alikuwa mshirikina anayefuga misukule. Tafadhari Like Ukurasa Wetu Wa Facebook Kwa Kubofya/ Click Neno Jambo Tz
Baba wa mtoto
Baba mzazi wa mtoto huyo, Rashid Mvungi alisema hakujua kama mwanaye alikuwa analelewa katika mazingira hatarishi. Akihojiwa na Ofisa Ustawi wa Jamii wa Mkoa wa
Morogoro, Oswin Ngungamtitu, Mvungi alisema alimzaa mtoto huyo nje ya
ndoa na amekuwa akituma fedha za matumizi kwa mama yake mkubwa.
Mvungi ambaye ni mtumishi wa Halmashauri ya Wilaya
ya Morogoro, alisema baada ya mzazi mwenzake kufariki dunia alishindwa
kumchukua mtoto wake kwa sababu tayari alishakuwa na mke. Alisema hata hivyo, alikubaliana na upande wa familia ya marehemu kuwa mtoto huyo alelewe na mama yake mkubwa.
Mtoto azungumza
Wakati Mvungi akihojiwa, baadhi ya watu waliofurika katika Ofisi za Ustawi wa Jamii walianza kuangua kilio baada ya mtoto huyo anayeonekana mlemavu kuanza kujibu maswali aliyokuwa akiulizwa na maofisa wa Ustawi wa Jamii.
Wakati Mvungi akihojiwa, baadhi ya watu waliofurika katika Ofisi za Ustawi wa Jamii walianza kuangua kilio baada ya mtoto huyo anayeonekana mlemavu kuanza kujibu maswali aliyokuwa akiulizwa na maofisa wa Ustawi wa Jamii.
Swali: Unaitwa nani:
Jibu: Naitwa Nasra
Swali: Ulikuwa unapewa chakula gani?
Jibu: Ubwabwa na maharage
Swali: Una umri wa miaka mingapi?
Jibu: Miaka minne
Swali: Baba yako yuko wapi?
Jibu: (anamwonyesha kwa kidole)
Ngungamtitu alisema huenda ulemavu wa mtoto huyo
umetokana na kuishi kwenye boksi au kukosa lishe yakiwamo maziwa ya
mama, hewa safi na upendo. Alisema si ajabu mtoto huyo kushambuliwa na magonjwa mbalimbali
kama minyoo, pneumonia, utapiamlo na malaria, ndio maana aliagiza
apelekwe katika Hospitali ya Mkoa kwa uchunguzi, chanjo na tiba.
Na Hamid Shariff, Mwananchi
Ofisa huyo alisema matibabu mengine atakayopatiwa ni pamoja na kunyooshwa viungo, mikono na miguu iliyolemaa. Ngungamtitu aliwaomba wasamaria wema, mashirika ya
dini na wadau mbalimbali kutoa misaada ya nguo, lishe, matibabu na
mahitaji mengine kwa mtoto huyo. Tafadhari Like Ukurasa Wetu Wa Facebook Kwa Kubofya/ Click Neno Jambo Tz
Na Hamid Shariff, Mwananchi
No comments:
Post a Comment