Dar es Salaam. Waziri wa Maliasili na Utalii, Lazaro Nyalandu, amewaondoa katika nyadhifa zao, Wakurugenzi mbalimbali kwa sababu zilizoelezwa kushindwa kutekeleza majukumu yao.
Hatua ya Nyalandu imekuja ikiwa ni utekelezaji wa azimio la Bunge la Desemba 22, 2013 lililotaka Mkurugenzi wa Idara ya Wanyamapori kuwajibishwa kutokana na tuhuma za uzembe na ukiukwaji wa haki za binadamu katika Operesheni Tokomeza.
Nyalandu alisema: "Namwondoa Prof Alexander Songorwa (Mkurugenzi wa Idara ya Wanyamapori) na kumteua Paul Sarakikya kukaimu nafasi hiyo."
Alisema pia kuwa amemwondoa Mkurugenzi
Msaidizi wa Matumizi Endelevu ya Wanyamapori, Profesa Jafari Kidegesho
kwenye nafasi hiyo na Dk Charles Mulokozi ameteuliwa kushika wadhifa
huo.
Mwingine aliyeteuliwa ni Julius Kibebe
kuwa Mkurugenzi Msaidizi Uzuiaji-Ujangili, nafasi iliyoachwa wazi na
Sarakikya wakati Mkurugenzi Msaidizi wa Mafunzo, Utafiti na Takwimu,
Nebbo Mwina anabaki kwenye nafasi yake. Kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa ku-like page ya facebook ya Jambo Tz
Nyalandu alisema Herman Keiraryo
anaendelea kuwa Mkurugenzi Msaidizi wa Uendelezaji wa Wanyamapori na
kwamba waliotangazwa kuondolewa kwenye nyadhifa, kazi zao mbadala
zitatangazwa baadaye.
Waziri Nyarandu alitoa siku 30 kwa
Wakurugenzi Wakuu wa kila Idara, Shirika na Taasisi za Wizara ya
Maliasili na Utalii, kutengeneza viashiria vya utendaji kazi (Key
Performance Indicators) na kuvikabidhi kwake.
Alisema hatua hiyo itafanikisha
kufikiwa malengo ya wizara hiyo, kwani uwajibikaji na ufanisi wa kazi za
kila siku utapimwa katika hali ya uwazi ili mikakati ya wizara
itekelezwe katika mifumo inayopimika na hatimaye kufikia malengo
yaliyokusudiwa.
Waziri huyo aliagiza kila mtumishi
akiwamo yeye mwenyewe, kutekeleza majukumu yaliyopangwa kwa kuzingatia
kanuni za mwenendo (code of conduct), zitakazopendekezwa na kupitishwa
na Baraza la Wafanyakazi la wizara hiyo. Kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa ku-like page ya facebook ya Jambo Tz
Chanzo, mwananchi.co.tz.
No comments:
Post a Comment