Washabiki wa mpira wa miguu nchini
watashuhudia bure mechi ya timu ya Taifa ya mpira wa miguu ya wanawake
(Twiga Stars) dhidi ya Zambia (Shepolopolo).
Mechi hiyo ya marudiano ya raundi ya
kwanza ya michuano ya Afrika kwa Wanawake (AWC) itachezwa Ijumaa
(Februari 28 mwaka huu) kwenye Uwanja wa Azam Complex uliopo Chamazi,
Dar es Salaam kuanzia saa 10 kamili alasiri.
Twiga Stars ambayo ilipoteza mechi ya
kwanza iliyochezwa Lusaka, Februari 14 mwaka huu kwa mabao 2-1 iko
kambini chini ya Kocha Rogasian Kaijage na msaidizi wake Nasra Juma
ikijiwinda kuwakabili Wazambia wanaotarajiwa kutua nchini Alhamisi
(Februari 26 mwaka huu).
Waamuzi wa mechi hiyo Ines Niyonsaba,
Jacqueline Ndimurukundo, Axelle Shikana na Suavis Iratunga kutoka
Burundi kutoka Burundi wanatarajiwa kuwasili nchini keshokutwa (Februari
26 mwaka huu). Kamishna Fran Hilton Smith kutoka Afrika Kusini yeye
atatua nchini Februari 27 mwaka huu kwa ndege ya South Africa Airways. Kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa ku-like page ya facebook ya Jambo Tz
Chanzo: TFF
No comments:
Post a Comment