Amina Mohamed,waziri wa mambo ya nje wa Kenya
Kenya imekuwa nchi ya kwanza kutoka
Jumuia ya Afrika Mashariki kuipongeza Tanzania kwa hatua yake ya
kutangaza bayana kwamba haiko tayari kutoka katika jumuiya hiyo kama
ilivyodhaniwa.
Wasiwasi kuwa Tanzania ingejitoa
kutoka jumuia ya Afrika Mashariki ulitokana na hali iliyojitokeza kwa
baadhi ya nchi za jumuia hiyo kuendesha mikutano yao bila kuishirikisha
Tanzania na Burundi.
Baadhi ya wanasiasa na wananchi nchini
Tanzania walitaka nchi yao iachane na jumuia hiyo wakizishutumu Kenya,
Rwanda na Uganda kuitenga Tanzania hata katika mikutano ya masuala
yaliyohitaji maamuzi ya jumuia.
Kufuatia mfarakano huo, ulionekana
kutishia uhai wa Jumuia ya Afrika Mashariki, Rais Jakaya Kikwete wa
Tanzania, wiki hii alilihutubia bunge la Muungano wa Tanzania mjini
Dodoma, katikati ya nchi na kutangaza bayana kuwa Tanzania haitatoka
katika jumuiya ya Afrika Mashariki, kwani imefanya kazi kubwa kuifufua
na kuiunda upya baada ya kusambaratika mwaka 1977.
Kwa upande wake, Kenya moja ya nchi
waanzilishi wa Jumuia ya Afrika Mashariki na ambayo ilishutumiwa
kushiriki kuibagua Tanzania, imemtuma waziri wake wa mambo ya nje, Amina
Mohammed kwenda Tanzania na kuwa na mazungumzo na waziri mwenzie wa
mambo ya nje Bernard Membe kuhusu mfarakano huo na nia ya kuimarisha
zaidi uhusiano wa nchi mbili hizo.
Katika mkutano na waandishi wa habari
jijini Dar es Salaam, Jumapili, waziri Amina Mohammed, amesema Kenya
inaunga mkono hotuba ya Rais Jakaya Kikwete, kuhusu uamuzi wake wa
kutojitoa katika Jumuia ya Afrika Mashariki, huku akisisitiza kuwa bila
Tanzania hakuna Afrika Mashariki na bila Afrika Mashariki hakuna
Tanzania.
"Kama unavyojua Kenya na Tanzania
tumekuwa tukiijenga jumuiya ya Afrika Mashariki kwa muda mrefu sana,
tuko na mafanikio mengi sana, kuna mambo mengi tumeyafanya, kuna njia
ndefu imebakia kuna mambo mengi yasiyoweza kupimwa kati ya nchi hizi.
Na tuna tumaini kwamba tutaendelea kuijenga Afrika Mashriki kwa nguvu zote na tutawasiliana na watu wetu kwa sababu tunataka watu wetu waishi vema na wawe majirani wazuri na waendelee .
Kwa Tunataka uchumi wetu uende vizuri. Kwa hiyo tutaendelea kushirikiana, sisi ni wale wa kwanza tuliokuwa pale kwa hiyo tunataka tufanye kile tunachoweza kuendeleza Afrika Mashariki..... Lakini tumefurahia sana sana hotuba ya Rais aliyotoa pale bungeni na tunawashukuru pia Watanzania kumuunga mkono."
Na tuna tumaini kwamba tutaendelea kuijenga Afrika Mashriki kwa nguvu zote na tutawasiliana na watu wetu kwa sababu tunataka watu wetu waishi vema na wawe majirani wazuri na waendelee .
Kwa Tunataka uchumi wetu uende vizuri. Kwa hiyo tutaendelea kushirikiana, sisi ni wale wa kwanza tuliokuwa pale kwa hiyo tunataka tufanye kile tunachoweza kuendeleza Afrika Mashariki..... Lakini tumefurahia sana sana hotuba ya Rais aliyotoa pale bungeni na tunawashukuru pia Watanzania kumuunga mkono."
Uhusiano wa Kenya na Tanzania ni wa kindugu
Pia waziri Amina amesisitiza kuwa
hakuna namna ambavyo Tanzania na Kenya zitatenganishwa, kwa namna
ambavyo zimejenga maingiliano makubwa ya kijamii na kiuchumi, huku
akiomba Tanzania kusaidia kusukuma ombi la Kenya la kutaka kesi
ianyomkabili Rais wake, Uhuru Kenyatta iahirishwe kwa mwaka mmoja zaidi
ili kumpa fursa ya kutekeleza majukumu yake ya kitaifa.
Kwa upande wake waziri wa mambo ya nje
wa Tanzania, Benard Membe amesema serikali yake imefurahi kuona Kenya
imekuwa nchi ya kwanza kuipongeza Tanzania kwa kuinusuru jumuia ya
Afrika Mashariki kama ilivyokuwa mwanzoni na kujenga jumuiya ya watu na
si ya viongozi, na kuahidi kushirikiana na Kenya katika masuala
mbalimbali likiwemo la kutaka kesi inayomkabili Rais Uhuru Kenyatta
katika mahakama ya ICC iahirishwe kwa mwaka mmoja zaidi.
Waziri Membe amesema waziri mwenzake
Amina kutoka Kenya amesema hotuba ya Rais Kikwete imewazindua kwani
hawakujua kuwa baadhi ya yale waliyokuwa wakiyafanya yalikuwa ni kukiuka
taratibu za Jumuia ya Afrika Mashariki na kuahidi kuwa Kenya
itashirikiana kikamilifu na nchi waanzilishi halisi wa Jumuia ya Afrika
Mashariki.
Katika kuonyesha nia thabiti ya
kutotoka katika Jumuia ya Afrika Mashariki, Rais Kikwete katika hotuba
yake aliyoitoa bungeni, alisema "Tanzania ni mwanachama mvumilivu,
mtiifu na mwaminifu na tunatimiza wajibu wetu kwa jumuia na kuhusika
kikamilifu katika ujenzi wake."alisema.
Rais Kikwete alitumia muda mrefu
katika hotuba hiyo kuchambua masuala mbalimbali ya msingi ya uhai wa
jumuia hiyo huku akisema ameshangazwa na nchi za Kenya, Uganda na Rwanda
kuzitenga Tanzania na Burundi.
No comments:
Post a Comment