Sunday, November 10, 2013

TUCTA YATAKA SH. 750, 000 KIMA CHA CHINI

kazi 857ac
Shirikisho la Vyama vya Wafanyakazi (Tucta) Mkoani Mbeya, limetangaza kiwango kipya cha mishahara inayotakiwa kuwa kima cha chini ni Sh 750,000.
Mwenyekiti wa Tucta mkoani hapa, Alinanuswe Mwakapala alisema kwa maisha ya sasa kima cha chini lazima kiwe Sh750,000 na kwamba, pendekezo hilo la mkoa litawasilishwa kwenye ngazi za juu za Tucta ili kulibariki.
Mwakapala alisema hayo kwenye hafla ya Chama cha Walimu Tanzania (CWT) kukabidhiwa jengo la ghorofa tano lililojengwa na Jeshi la Kujenga Taifa (JKT).
"Wafanyakazi nchini sasa wamechoshwa na mishahara midogo, hivyo wakati umefika kwa wafanyakazi kutoogopa maandamano na migomo kudai haki," alisema huku akishangiliwa.
Hata hivyo, Rais wa CWT, Gratius Mukoba alisema madai ya wafanyakazi yaliyowasilishwa Serikalini ni kutaka nyongeza ya mishahara kwa asilimia 100.
Mkoba alisema CWT hivi sasa wanasubiru ndani ya miezi mwili hadi Desemba kupata majibu.
hayatapatikana basi Serikali ijue imejipalia mkaa.
''Hatuwezi kuendelea kuwaona watu wasiofanyakazi wanapata mishahara mikubwa wakati wafanyakazi wanasota. Mwisho wa matatizo hayo ni sasa'' alisema huku akiwataka wafanyakazi hususan walimu kuachana na njama za kutaka kuwatenganisha.
Alisema Serikali inatakiwa kuwalipa walimu Sh49 bilioni wanazodai zikiwamo Sh30 bilioni walizopunjwa katika mishahara na kwamba pia lazima ipunguze kodi kwa wafanyakazi na kuboresha mazingira ya kazi.
CHANZO MWANANCHI

No comments:

Pro

PropellerAds

LinkWithin

Soma na Hizi Pia Plugin for WordPress, Blogger...