Mmoja wa wakazi wa Rugelele kata Rujewa wilaya ya Mbarali mkoani Mbeya DUKA MKWILA[20]ni miongoni mwa wananchi waliopiga simu za uongo katika kikosi cha zimamoto mkoa wa mbeya akiwa amepewa adahabu ya kuosha gari la zimomoto |
JESHI la
zimamoto na uokoaji limewataka wananchi kuacha matumizi mabaya ya miito ya simu
ya dharula kwa Jeshi hilo ili kuepusha usumbufu kwa Jeshi pindi wanapopigiwa
simu za dharula.
Wito huo
umetolewa na Jeshi hilo baada ya kupata kero za mara kwa mara kutoka kwa
wananchi wanaopiga simu kwenye Jeshi hilo wakihitaji huduma za gari hilo lakini
wanapofika eneo waliloelekezwa wanakuta hakuna tukio lolote.
Wamekuwa
wakipokea simu nyingi za uongo hivyo serikali kuingia gharama kubwa za mafuta
ambayo yangetumika kwenye maafa pindi yanapotokea.
Mmoja wa
wakazi wa Rugelele kata Rujewa wilaya ya MBARALI DUKA MKWILA[20]ni miongoni mwa
wananchi waliopiga simu za uongo katika Jeshi hilo mara kadhaa na kuomba huduma
nyingine badala ya ajali ya moto hali iliyofanya Jeshi hilo kumkamata na
kumhoji.
DUKA amesema
yeye namba hiyo alipewa na mtu mwigine aliyedai kuwa mwenye namba hiyo huwa
anatoa pesa za FREE MASON pia dawa za kienyeji kwa matatizo mbalimbali.
|
No comments:
Post a Comment