Maelfu ya Wananchi wa Kata ya kikuyu kusini wakiandamana katika mitaa ya mji wa Dodoma kwa ajili ya kupinga kubomolewa na mamraka ya ustawishaji makao makuu [CDA] wanaotarajia kubomoa nyumba, mapagale na misingi ya wakazi hao.
Diwani wa kata ya Kikiyu kusini Ancelmu Kutaka
akifafanua jambo mbele ya Wananchi wa kata hiyo waliondamana kupinga
kubomolewa na Mamraka ya ustawishaji makao makuu [CDA] walipanga kuboa
wakati wowote kuanzia leo.
Kaimu Mkurugenzi wa CDA Paskas Mulagili Akifafanua jambo wakati
alipokuwa akiongea na waandishi wa Habari wa vyombo mbalimbali kuhusu
maandamano ya wananchi wa kata ya Kikuyu Kusini walioandamana kupinga
ubomoaji unaotarajiwa kufanywa na mamlaka hiyo siku yoyote kuanzia leo.
PICHA NA JOHN BANDA
Na John Banda, Dodoma
WAKAZI wa
Kata za Kikuyu Kusini na Kilimani mkoani Dodoma
wameandamana kupinga amri iliyotolewa na Mamlaka ya Ustawishaji ya Makao Makuu
(CDA) ambayo inawataka kuhama katika eneo hilo
ndani ya siku saba.
Wakazi
hao walioandamana kutoka Kikuyu hadi Viwanja vya Nyerere Square katikati ya mji
wakimtaka mkuu wa Mkoa wa Dodoma,
Dk. Rehema Nchimbi kuzungumza nao.
Maandamano
hayo yalisindikizwa na ulinzi wa polisi hadi katika viwanja hivyo huku wakazi
hao wakiwa wameshikilia mabango yenye jumbe mbalimbali.
Wakazi
hao wakiwa wanaimba nyimbo huku wakiinua mabango yao
juu yenye ujumbe kama Cda ni zaidi ya
Alshababi, CCM mnaiona bomoabomoa, Cda ni zaidi ya Nduli Idd Aminini Dada na
lingine likisomeka Hata wanyama hupewa hifadhi.
Wakizunguza
na waandishi wa habari katika viwanja hivyo wakati wakimsubiri mkuu wa mkoa
baadhi ya wananchi na viongozi wao wa mitaa walidai kuwa lengo la maandamano
hayo ni kufikisha kilio chao kwa serikali ya mkoa.
Andrew
Mdumi mwenyekiti wa mtaa wa Mkalama ambao ni sehemu ya eneo linalotakiwa
kuvunjwa alisema kuwa wameamua kufanya maandamano hayo mara baada ya kupewa
amri ya kuondoka katika eneo wanaloishi kwa kipindi kirefu.
Mdumi
alisema, kuwa Mamlaka ya ustawishi Makao makuu imekuwa ikiwapatia namba kila
wakati na kudai kuwa itakuja kuwapimia lakini katika hali ya kushangaza imewapa
amri ya kuondoka ndani ya siku saba kwa madai kuwa wamevamia katika eneo hilo ambalo lilikuwewa
limetengwa kwajili ya bustani za mbogamboga na matunda.
“Wanataka
tuondoke ili kupisha kilimo cha mbogamboga na matunda hivi kweli mboga na
maisha yetu kipi cha msingi kuna nyumba zaidi ya 1000 ambazo watakakuzibomoa
kwajili tuu ya kupisha bustani” alisema
Alisema
kuwa wamekuwa wakishirikiana na CDA kwa kipindi kirefu ili kuweza kufanikisha
zoezi la upimaji wa viwanja hivyo hata kwa gharama zao wenyewe.
Mwekiti
wa kamati ya upimaji katika Kata ya Kikuyu kusini Mathew Ndallu, alisema kuwa
katika kufuatilia suala hilo
la kupimiwa viwanja walikutana na CDA na kukubaliana kuwa waje wafanye utambuzi
wa nyumba zilizopo, mapagale na misingi ili waweze kufanya upimaji.
Ndallu alisema kuwa walikubaliana na kuwa kutokana na
eneo hilo kuwa halijapimwa wao wako tayari kuchangia gharama za upimaji ili
kuwezesha zoezi hilo kufanyika.
“Tulikubaliana
nao mara baada ya wao kuja kutambua idadi ya nyumba mapagale na misingi
watupimia na sisi tuko tayari kuchangia kiasi cha sh.500,000 kwa kila mwenye
eneo” alisema Ndalllu.
Aidha
alisema kuwa katika hali ya kushangaza pale ambapo walikuwa wanasubiri kupimiwa
CDA waliwageuka na kuwataka kwanza wao wapatiwe viwanaja 500 ili waweze
kuwapiamia.
“Mara
baada ya kukubaliana nao kuwa tuko tayari kuchangia lakini Mkurugenzi
alituambia kwanza tuwape wao viwanja 500 ili waweze kuja kutupimia na kama hatutakubali basi watakuja kutubomolea” alisema.
Alisema
kuwa mara baada ya wao kukataa kumpa mkurugenzi huyo viwanja hivyo aliwaandikia
barua hiyo ambayo ilikuwa inawataka wakazi wa maeneo hayo kuondoka kabla ya
tarehe 30 ya mwezi Septemba (jana).
“Walituandikia
barua ambayo inatutaka kuaondoka ndani ya siku hizo saba ikiwa ni kuanzia
tarehe 23 ya mwezi huu ambapo inaishia leo (jana) na kesho (leo )wanakuja
kuanza kubomoa” alisema Ndallu.
Alisema
kutokana na hali hiyo ambayo imeonyesha kuwa CDA imeshindwa kuwasikiliza kilio
chao wameona kuwa hiyo ndiyo njia sahihi ya wao kupata suluhu ya tatizo lao.
Alisema
kuwa jumla ya mitaa mnne katika kata hizo ndiyo inayotakiwa kubomolewa ambayo
ni mitaa ya Mkalama, Chidachi pamoja na Image A na B.
Akizungumza
na kundi la wakazi hao mkuu wa mkoa wa Dodoma Dk Rehema Nchimbi, alisema kuwa anatengua
amri hiyo iliyotolewa na CDA na kumtaka Mkurunzi wa mamlaka hiyo kukutana na
viongozi wa maeneo husika.
“Naitengua
amri hiyo na namwagiza Mkurugenzi akutane na wananchi hawa pamoja na viongozi
wao ili kuweza kufikia muafaka kwani kubomoa sio suluhu hamuwezi kubomoa Dodoma nzima na
ningependa kuletewa taarifa juu ya sula hili … mnachotakiwa ni kuboresha na
kutumia njia sahihi ambazo hazita waumiza wananchi ambao ndiyo wateja wenu.
No comments:
Post a Comment