Rais wa Sudan Omar El bashir amethibitisha kwamba atahudhuria mkutano wa Umoja wa Mataifa jijini New york juma hili, licha ya kusakwa na mahakama ya kimataifa kuhusu uhalifu wa kivita ICC.
Bashir anatuhumiwa kwa mauaji ya kimbari katika jimbo la Darfur.
Katika taarifa kwa vyombo vya habari
Bashir amesema kuwa tayari amekodisha chumba cha kulala katika hoteli
moja mjini humo na kwamba hatishiki kukamatwa na Marekani kwa kuwa sio
mwanachama wa ICC.
Hata hivyo haijulikani iwapo atapewa
viza kwa kuwa imekuwa utamaduni wa taifa hilo ambalo limetoa vibali
hivyo kwa viongozi kama Robert Mugabe wa Zimbabwe na Mahmoud Ahmedinejad
wa Iran kuhudhuria mkutano huo. Chanzo: bbcswahili
No comments:
Post a Comment