Huku hali ya mshikemshike ikiendelea kushuhudiwa katika jengo la Westgate lenye maduka, ufyatulianaji risasi umesikika ndani ya jengo hilo lenye maduka na mikahawa zaidi ya themanini.
Wapiganaji wa Al shabaab wamewateka
nyara raia ambao idadi yao haijulikani. Walikuwemo ndani ya jengo
wakiendelea na shughuli zao kuanzia Jumamosi mchana wakati wapiganaji wa
Al shabaab walipowavamia na kuanza kufyatua risasi kiholela.
Inaarifiwa kuna maiti kumi katika ghorofa ya kwanza ya jengo hilo.
Inaarifiwa wapiganaji hao wanaoaminika
kuwa wanachama wa Al Shabaab ni kati ya kumi na kumi na watano na bado
wangali ndani ya jengo hilo.
Ripoti zinasema kuwa ufyatulianaji mkubwa wa risasi umesikika katika jengo hilo kwa takriban dakika 15.
Harakati za kuendelea kumaliza operesheni hiyo zinaendelea lakini hali ya mateka walio ndani ya jengo hilo inaendelea kudorora.
Wakenya waliofanikiwa kuondoka katika jengo la Westgate kwa usaidizi wa polisi
Rais Kenyatta amesema kuwa jueshi linajitahidi kuhakikisha kuwa linakabiliana vilivyo na wanamgambo hao.
Helikopta za polisi zinazunguka juu ya
jengo hilo pamoja na ndege za kijeshi kushika doria. Vikosi vya usalama
vinaendelea na operesheni kujaribu kuwanusuru waathiriwa wakati hali
ikiwa ni ya ati ati katika eneo la shambulizi.
Awali jeshi la Kenya lilisema limeweza
kudhibiti jengo hilo lote ingawa bado limetaja hali kuwa tete mno hasa
katika kujaribu kuwaokoa mateka waliosalia ndani ya jengo hilo.
Ripoti zinasema kuwa watu 69
wamefariki katika shambulizi hilo la Al Shabaab kufikia sasa huku 175
wakijeruhiwa. Baadhi wametibiwa na kuondoka hospitalini. Baadhi ya
majeraha waliyopata ni majereha ya risasi na kutokana na guruneti ambalo
Al shabaa waliwarushia wale waliokuwa ndani ya mikahawa siku ya
Jumamosi.
Kundi hilo limekiri kutekeleza
shambulio hilo kutokana na hatua ya kenya kupelekeka majeshi yake nchini
Somalia ili kukabiliana na wapiganaji hao. Chanzo: bbcswahili
No comments:
Post a Comment