Kenya inaanza siku tatu za maombolezi
ya kitaifa kwa waathiriwa wa mashambulizi ya kigaidi yaliyofanyika
katika jengo la kibiashara la Westgate mjini Nairobi.
Watu 67 wameuawa ikiwemo wanajeshi kadhaa wa usalama, ingawa kuna hofu kuwa idadi ya waliofariki huenda ikaongezeka.
Maafisa wa uchunguzi wa kimataifa
wanaungana na wale wa Kenya kujaribu kuondoa mili ambayo imenaswa kwenye
vifusi vya jengo hilo ambalo sehemu yake iliporomoka jana. Nia ni
kujaribu pia kutambua uraia wa washambulizi hao.
Baraza la usalama wa kitaifa linatarajiwa kukutana leo kudadisi yaliyotokea na kujiandaa kwa mkakati mpya wa kigaidi.
Magaidi watato waliuawa katika
shambulizi hilo lililodumu siku nne na kuwa washukiwa wengine 11
walikamatwa wakijaribu kuondoka nchini.
Katika hotuba yake kwa taifa siku ya
Jumatano , Rais Uhuru Kenyatta alisema kuwa alihisi uchungu mkubwa na
kuwa Kenya imejeruhiwa vibaya,lakini alielezea matumaini kwa kuwa
shambulizi limeisha na kusema kwamba waliohusika watakiona cha
mtemakuni.
No comments:
Post a Comment