ULIMWENGU umepatwa na mshtuko mkubwa kwa kuona picha za tukio kubwa la kigaidi kwenye moja ya maduka makubwa jijini Nairobi. Hili ni shambulio kubwa la kigaidi kupata kutokea Afrika Mashariki tangu lile la mwaka 1998. Na ajabu ya kihitoria ni kuwa matukio mengi ya kigaidi yametokea katika mwezi wa Septemba.
La Nairobi ni shambulizi la kigaidi la kulaaniwa vikali na wapenda amani wote ulimwenguni. Hata hivyo, moja ya tafsiri ya vitendo vya kigaidi tunavyovishuhudia Nairobi ni kuwepo kwa hali ya vita vya kigaidi vyenye kuendeshwa kwenye maeneo ya mijini (Urban terrorism).
Ni shambulizi lenye athari mbaya kiuchumi si tu kwa nchi ya Kenya, bali hata majirani zake ikiwemo Tanzania. Ni shambulizi lililowaogopesha wageni wengi wakiwamo wawekezaji pia. Kwamba Al Shabaab inalenga pia nchi za Magharibi. Hivyo basi,
hata raia wake. Kunahitajika jitihada
za pamoja kuwaondoa hofu watu wa mataifa ya nje, kuwa kilichotokea
Nairobi kitadhibitiwa kwa njia zote, kisitokee tena.
Na hakika, aina hii ya ugaidi ni ngumu
sana kudhibitika hatakama nchi ina jeshi kubwa na lenye vifaa vya
kisasa. Inahitaji ushiriki wa raia wema katika kutoa taarifa za wahalifu
hata kabla hawajafanya matendo yao maovu. Inahitaji pia maandalizi
makini, ya kuwa na vikosi vilivyo tayari wakati wote kukabiliana na
matukio kama haya.
Ni dhahiri, kuwa mbinu inazotumika
kikundi cha kigaidi cha Al Shaabab ambacho maana hasa ya jina hilo ni '
Vijana', ni moja ya changamoto kubwa katika mapambano dhidi ya ugaidi.
Al Shabaab iliundwa mwaka 2006.
Kinasemekana kuwa na wapiganaji wenye silaha wapatao 10,000. Al Shabaab
katika miaka ya karibuni wamepoteza maeneo mengi ya mijini waliyokuwa
wakiyadhibiti, ikiwamo mji wa Kismayu ambao majeshi ya Kenya
yaliudhibiti baada ya kuwasambaratisha Al Shabaab. Kwa sasa Al Shabaab
bado wana nguvu maeneo ya vijijini katika Somalia.
Kufuatia Kenya kujiingisha kijeshi
kupanbana na Al Shaabab, kikundi hicho kimeifanya Kenya kuwa adui na
kutangaza wazi azma yake ya kuishambulia Kenya. Mwezi Aprili mwaka huu
watu watano walipoteza maisha nchini Kenya baada ya wapiganaji wa Al
Shabaab kuingia kwa nguvu wakiwa na silaha kwenye mgahawa mmoja kwenye
mji wa Garissa nchini Kenya.
Mwaka 2012 ndipo Al Shabaab
walipojiunga rasmi na mtandao wa kigaidi wa Al qaida chini ya kiongozi
wa Al qiada, Ayman al- Zawahiri.
Hakika, hapa duniani matukio ya kigaidi yameongezeka.
Kwa faida ya wasomaji, nitaanza kwa kuangalia chimbuko la ugaidi kihistoria. Ni rahisi kusema kwamba ulimwengu umebadilika baada ya ugaidi wa Septemba 11 mwaka 2001 kule Marekani. Kwamba ugaidi umesogea karibu zaidi katika fikra zetu. Watanzania bado tunakumbuka tukio la shambulizi la kigaidi dhidi ya jengo la Ubalozi wa Marekani jijini Dar Es Salaam Agosti 7, 1998.
Kwa faida ya wasomaji, nitaanza kwa kuangalia chimbuko la ugaidi kihistoria. Ni rahisi kusema kwamba ulimwengu umebadilika baada ya ugaidi wa Septemba 11 mwaka 2001 kule Marekani. Kwamba ugaidi umesogea karibu zaidi katika fikra zetu. Watanzania bado tunakumbuka tukio la shambulizi la kigaidi dhidi ya jengo la Ubalozi wa Marekani jijini Dar Es Salaam Agosti 7, 1998.
Sura ya ugaidi imeonekana vema zaidi
miongoni mwa walimwengu. Bila shaka, picha ya filamu ya televisheni
yenye kuonesha majengo mawili ya World Trade Centre kule Marekani
yakitunguliwa na kuanguka, zimeonwa na takribani asilimia 75 ya watu wa
ulimwengu huu. Katika hili la kuchambua ugaidi, hebu
basi tuanze na kujiuliza;
basi tuanze na kujiuliza;
Ugaidi ni nini?
Itakumbukwa wabunge wa bunge la
Jamhuri ya Muungano walipokutana Dodoma mwaka 2002 walipitisha Muswaada
wa Ugaidi. Wabunge wetu walitumia muda mwingi sana kujadili tafsiri ya
neno "ugaidi".
Kwa kifupi, ugaidi ukitafsiri kutoka
neno la Kiingereza "Terrorism" tunapata maana ya "hofu". Neno la
Kiingereza "Terror" lina maana ya hali ya "kutisha".
Vitendo vya kigaidi hutumiwa na mtu au
makundi ya watu ili kuwaingizia watu hofu ndani ya mioyo yao na pengine
hata kuchukua madaraka ya kisiasa. Ugaidi ni njia ya mnyonge na hata
mwenye nguvu kutimiza malengo yake. Hili litafafanulika zaidi kadri
utakapofuatilia maandiko haya.
Kihistoria tunaona kuwa, vitendo vingi
vya kigaidi humu duniani vimefanywa pia na dola zilizo madarakani kwa
minajili ya kuendelea kushika hatamu za dola. Mathalan, msemo wa "
Utawala dhalimu" kwa tafsiri ya Kiingereza "Terror regime" hutumika
tunapoielezea dola yenye kutumia mabavu na nguvu nyingi kupita kiasi.
Dola au mtawala asiyezingatia sheria wala haki za kibinadamu.
Msamiati huu wa utawala dhalimu
unatokana na lugha ya Kifaransa na una chimbuko la Mapinduzi ya Wananchi
kule Ufaransa kati ya mwaka 1789 hadi 1799. Utawala dhalimu wenye
kutisha" la terreur" ulikuwepo kule Ufaransa kunako miaka ya kati ya
1792 hadi 1794. Katika kipindi hicho watu takribani 40,000, wengi wao
wakiwa wakulima na wahunzi waliuawa.
Mifano ya tawala dhalimu na za kutisha
katika sehemu nyingine za dunia ni kama Urusi ya zamani chini ya
dikteta Stalin, utawala wa Kinazi wa Ujerumani kati ya 1933-1945 chini
ya Fashisti Hittler.
Katika Afrika, tuna pia mifano kadhaa
ya tawala dhalimu na za kutisha ambazo kimsingi ni tawala za kigaidi.
Uganda ya Idd Amin, Afrika ya Kati ya Bokassa, Zaire ya Mobutu, na nchi
nyingine nyingi. Hizi zilikuwa tawala dhalimu.
Ugaidi kimsingi ni ile hali ya mtu,
kikundi au dola, kwa maana ya taifa,kutumia nguvu nje ya wigo wa sheria
ili kufikia malengo yao. Mwenye kuendesha vitendo vya kigaidi huchagua
watu wake watakaoathirika na vitendo hivyo. Si lazima mtu au watu hao
watakaoathirika wawe ni wahusika wa moja kwa moja wa mgogoro husika,
isipokuwa, waathirika mara nyingi huchaguliwa na huonekana kama
wawakilishi wa malengo ambayo magaidi wanataka kuyafikia.
Malengo au sababu za ugaidi zaweza kuwa ni za kidini, kijamii na kisiasa.
Malengo au sababu za ugaidi zaweza kuwa ni za kidini, kijamii na kisiasa.
Ugaidi huwa wa kimataifa pale tukio la
kigaidi linapofanywa nje ya mipakaya yule anayatenda tendo la kigaidi,
au raia wa nchi moja wanapokuwawalengwa na kauthirika na tendo la
kigaidi katika nchi ya tatu, mathalan,magaidi kutoka Colombia
wanapofanya tendo la kigaidi dhidi ya raia waUingereza katika nchi ya
Zambia.
Na Maggid Mjengwa,
No comments:
Post a Comment