Mawaziri wa serikali walipokea taarifa
kuhusu tisho la mashambulizi ya kigaidi kabla ya kundi la Al Shabaab
kushambulia jengo la Westgate mjini Nairobi.
Kwa mujibu wa taarifa za kijasusi
zilizofichuliwa, zilionyesha maelezo ya mipango ya mashambulizi hayo
kufanyika Nairobi au mjini Mombasa.
Taarifa zinazohusianaKenya
Mawaziri wanne na mkuu wa majeshi walikuwa wamefahamishwa kuhusu tisho la kufanyika shambulizi la kigaidi.
Mawaziri wanne na mkuu wa majeshi walikuwa wamefahamishwa kuhusu tisho la kufanyika shambulizi la kigaidi.
Watu 67 walifariki na mamia kujeruhiwa
katika shambulizi la kigaidi ambalo Al Shabaab walikiri kulifanya
Septemba 21 mjini Nairobi.
Kwa mujibu wa taarifa za gazeti la
Daily Nation, mawaziri walipokezwa taarifa za kati ta yarehe 13 na 20
kuhusu uwezekano wa kufanyika mashambulizi kadhaa ya kigaidi mjini
Mombasa na Nairobi.
Onyo hizo zilitolewa kwa mara ya kwanza mnamo mwezi Januari kwa mujibu wa gazeti hilo na kwa mara nyingine kuanzia Septemba.
Kuna hofu idadi ya waliofariki huenda ikaongezeka.
Kwa mujibu wa taarifa hizo, serikali
ya Israel pia ilitoa taarifa za kuonya kuwa huenda magaidi wakashambulia
majengo yanayomilikiwa na raia wake kati ya tarehe 4 na 28 Septemba.
Daily Nation limeripoti kuwa taarifa
za kijasusi zilionyesha kuwa viongozi wa al-Shabab walikuwa wameanza
kulenga maeneo ya kushambulia ikiwemo Westgate na kanisa la Holy Family
Basilica.
Kuna hofu idadi ya waliofariki huenda ikaongezeka.
Maafisa wa serikali wanaosemekana
kupokea taarifa hizo ni pamoja na waziri wa fedha, Julius Rotich, waziri
wa usalama Joseph Ole Lenku, waziri wa maswala ya kigeni, Amina
Mohammed, waziri wa ulinzi Raychelle Omamo na mkuu wa majeshi Julius
Karangi.
Mkuu wa shirika la ujasusi Michael
Gichangi, anatarajiwa kuhojiwa na kamati ya bunge kuhusu usalama siku ya
Jumatatu. Chanzo: bbcswahili
No comments:
Post a Comment