Jamaa za familia ya aliyekuwa rais wa Afrika Kusini, Nelson Mandela,
wamewasilisha kesi ya uhalifu dhidi ya mjukuu wa Mandela,Mandla Mandela.
Msemaji
wa polisi, Mzukisi Fatyela aliambia BBC kuwa maafisa wa usalama
watachunguza tuhuma dhidi ya Mandla za kufukua makaburi kinyume na
sheria
Mwendesha mashtaka wa umma, kisha ataamua ikiwa amshtaki Mandla au la.
Inahusisha
maiti za watoto watatu wa Mandela ambao inaaminika walifukuliwa na
Mandla kutoka makaburi ya familia miaka miwili iliyopita.
Katika
kesi nyingine, jamaa kumi na sita wa familia ya Mandela, wanataka
kurejesha miili hiyo katika kijiji cha Qunu, ambako Mandela, ambaye
anaumwa sana hospitalini anataka kuzikwa akifa.
Kesi hiyo
inayosikilizwa katika mahakama kuu ya Mthatha, katika mkoa wa Mashariki
iliakhirishwa hapo jana kuanza kusikilizwa leo.
Wiki
jana, mahakama ilitoa amri ya muda kwa maiti za watatu hao kuhamishwa
kutoka nyumbani kwa Mandla katika kijiji cha Mvezo hadi Qunu, umbali wa
kilomiya 22.
Lakini Mandla Mandela, ambaye alitawazwa kama kiongozi wa kijamii na babu yake, sasa anapinga vikali amri hiyo.
No comments:
Post a Comment