Rais wa zamani wa Afrika Kusini, Nelson Mandela
amelazwa tena hospitalini baada ya kuugua ugonjwa wa mapafu kwa mara
nyingine.
Taarifa kutoka kwa serikali ya nchi hiyo,
ilisema kuwa Mandela mwenye umri wa miaka 94 alilazwa hospitalini muda
mfupi kabla ya saa sita usiku.
Mandela alilazwa siku kumi na nane
hospitalini mwezi Disemba mwaka jana kupokea matibabu ya ugonjwa wa
mapafu na kibofu.
Anasifika sana kama baba wa taifa hilo kwa
kuongoza vita dhidi ya utawala wa ubaguzi wa rangi.
Kadhalika Mandela alihudumu kama rais wa kwanza
mweusi Afrika Kusini tangu mwaka 1994 hadi mwaka 1999, ingawa hali yake
ya kiafya imezua wasiwasi kwa muda sasa.
Rais Jacob Zuma alimtumia taarifa ya kumpa pole
na kumtakia kupona Mandela
"tunawataka watu wa Afrika Kusini pamoja na
duniani kote kuwa watulivu na kumuombea Madiba na familia yake. Tuna
imani kuwa kikosi cha madaktari wanaomtibu Mandela watafanya kila hali
kuhakikisha anapona,'' alisema Zuma katika taarifa yake.
Mapema mwezi huu bwana Mandela alilazwa
hospitalini mjini Pretoria baada ya kufanyiwa ukaguzi wa kiafya.
No comments:
Post a Comment