Kamanda
wa Polisi kanda Maalum Dar es Salaam DCP Suleiman Kova akiwa
maeshikilia baadhi ya vipande vya meno ya Tembo vilivyokamatwa hivi
karibuni katika eneo la Kimara Wilaya ya Kinondoni.
Kamanda
wa Polisi kanda Maalum Dar es Salaam DCP Suleiman Kova akifafanua kuwa
Jeshi la polisi limeweka mikakati ya mpango kazi ikiwa ni pamoja na
kushirikiana na vyombo mbalimbali vya ulinzi na usalama pamoja na kikosi
cha zimamoto ili kuhakikisha kuna udhibiti wa matukio ya uhalifu au
fujo.
Aidha
amesema jeshi hilo pia limefanikiwa kukamata bunduki mbili aina
tofauti, moja ikiwa ni Shotgun yenye namba AB 44736 na ya pili ni
Greener yenye namba 10883 pamoja na risasi 17.
Jeshi
la polisi kanda Maalum ya Dar es salaam limefanikiwa kukamata vipande
vya meno ya Tembo vipatavyo 13 ambavyo thamani yake haikufahamika mara
moja. Tukio hilo limetokea katika eneo la Kimara wilaya ya Kinondoni
ambapo askari walipata taarifa kutoka kwa wasamaria wema.
Pamoja
na kukamatwa kwa vipande hivyo pia amekamatwa mtuhumiwa Christopher
Julius mwenye umri wa miaka 18, mwanafunzi wa Kidato cha Nne – Kibaha
sekondari.
Katika
hatua nyingine kupitia misako mikali inayoendelea Jeshi la polisi
limefanikiwa kukamata noti bandia 32 za shilingi elfu 10,000/= zenye
thamani ya shilingi 320,000/= za kitanzania.
Akizungumza
na vyombo vya habari Kamanda wa Polisi kanda Maalum Dar es Salaam DCP
Suleiman Kova ametoa tahadhari kwa wananchi kuwa makini hasa katika
kuelekea siku kuu ambapo watu wasio na nia njema wanapenyeza pesa bandia
kwa nia ya kujiongezea kipato binafsi.
Na.Mo
Blog Team
No comments:
Post a Comment