Mwenyekiti
wa chama cha watu wenye ulemavu Tanzania (TAS) “Tanzania Albino
Society” ndugu Ernest Kimaya akizungumza kwa uchungu mbele ya Mkuu wa
Mkoa wa Rukwa Injinia Stella Manyanya (Pichani chini) kuelezea juu ya
tukio la kinyama alilofanyiwa Maria Chambanenge (39) la kukatwa mkono
wake wa kushoto kwa kile kinachodaiwa kwa imani za kishirikina kuwa ni
kupata utajiri. Watuhumiwa waliohusika na tukio hilo ambao pia yupo mume
wake na muathirika wameshakamatwa na polisi na kuonyesha mkono huo,
taratibu za mashitaka zinaendelea ili haki iweze kupatikana. Mwenyekiti
huyo ameiomba Serikali kufkiria adhabu kali kwa watuhumiwa kama ho
ikiwepo kunyongwa ili fundisho kwa wengine na Albino waweze kuishi
katika nchi yao kwa amani.
Mwenyekiti
wa TAS akizungumza na Mkuu wa Mkoa wa Rukwa ofisini kwake. Kulia ni
Katibu Mkuu wa chama hicho ndugu Mohammed Chanzi.
Mkuu wa
Mkoa wa Rukwa Injinia Stella Manyanya akizungumza kwa uchungu na kutoa
onyo kali kuwa vitendo hivyo vya kinyama havitavumiliwa. Alitoa wito kwa
wananchi kuendelea kutoa ushirikiano kutokomeza vitendo hivyo.
Kabla ya
kwenda kumtembelea mgongwa Mkuu wa Mkoa wa Rukwa aliandaa chakula kwa
wageni wake.
Mkuu wa
Mkoa wa Rukwa Injinia Stella Manyanya na msafara wake pamoja na viongozi
wa chama cha Albino Tanzania (TAS) wakimfariji Mama Maria Chambanenge
walipomtembelea katika hospitali kuu ya Mkoa Rukwa ambapo hali yake kwa
sasa inaendelea vizuri japo ameongezewa ulemavu mwingine wa viungo kwa
kukatwa mkono wake wa kushoto.
Mwenyekiti
wa chama cha watu wenye ulemavu Tanzania (Albino) ndugu Ernest Kimaya
akimfariji Mama Maria Chambanenge ambaye anaendelea kupatiwa matibabu
katika hospitali kuu ya Mkoa Rukwa kufuatia kukatwa mkono wake wa
kushoto na watu walioshirikiana na mume wake na ambao tayari wapo
mikononi mwa polisi.
NA HAMZA
TEMBA – OFISI YA MKUU WA MKOA RUKWA
………………………………………………………………………………………………………………………………………
Mwenyekiti
wa chama watu wenye ulemavu wa ngozi Tanzania “Tanzania Albino Society”
(TAS) ndugu Ernest Kimaya ameiomba serikali kupitia upya sheria ya haki
ya kuishi kwa kuwapatia adhabu kali ya kifo wale wote wanaohusika kwa
vitendo vya kinyama dhidi ya albino ikiwepo mauaji na ukataji wa viungo
vyao wakiwa hai kwa kile kinachoaminika katika imani za kishirikina kuwa
ni kujipatia utajiri.
Aliyasema hayo
jana akizungumza na Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Injinia Stella Manyanya
ofisini kwake alipomtembelea akiongozana na viongozi wengine wa chama
hicho kumpa pongezi zake za dhati kwa kile alichosema ni mfano wa kuigwa
kwani tangu vitendo hivyo vianze hapa nchini kwa muda wa miaka mitano
iliyopita ni Mkoa wa Rukwa pekee umefanikiwa kuwakamata wahalifu wa
namna hiyo pamoja na kiungo husika kwa muda mfupi usiozidi siku tatu.
Amesema
kuwa maalbino wamenyanyasika sana katika nchi yao kwa kukosa uhuru na
amani kama watu wengine jambo ambalo ni kinyume na haki za binadam.
“Watu waliokamatwa sio wa kuachiwa huru, wabanwe hata kuchomwa moto
wataje wahusika wengine kwani mtandao wao ni mmoja na inatia uchungu
sana kwa sisi maalbino” alisema mwenyekiti huyo.
Kwa upande
wake Mkuu wa Mkoa wa Rukwa alimshukuru mwenyekiti wa chama hicho na
viongozi wenzake kwa kufika Mkoani kwake kujionea hali halisi baada ya
kuskika kwa matukio hayo ya kinyama kwa Albino wenzao na pia
kuwashukuru wananchi na jeshi la Polisi kwa ushirikiano mzuri walioutoa
kufanikisha watuhumiwa kutiwa mbaroni ili haki iweze kutendeka. Mkuu
huyo wa Mkoa alisema vitendo kama hivo kaamwe havitaweza kuvumilika
Mkoani kwake.
Kumekuwepo
na matukio ya kusikitisha hivi karibuni ya ukatili kwa Albino ambapo
mama mlemavu wa ngozi Maria Chambanenge (39) mkazi wa kijiji cha
kavifuli katika Wilaya ya Sumbawanga alivamiwa nyumbani kwake usiku wa
manane na kukatwa mkono wake wa kushoto na watuhumiwa ambao
wameshakamatwa na jeshi la polisi na taratibu za mashitaka yao
zinaendelea.
Vilevile
katika bonde la ziwa Rukwa kata ya Milepa mtoto wa kiume mwenye ulemavu
wa ngozi ‘albino” Mwigulu Matomange Magessa mwenye umri wa miaka saba
ameshambuliwa na vijana watatu waliovaa kininja na kumkata mkono wake
mmoja na kutokomea na kusikojulikana. Polisi wanaendelea na uchunguzi
kuwabaini wahusika.
Matukio
yote hayo yanahusishwa na wahalifu kutoka Mkoa jirani wa Mbeya ambapo
vitendo hivi vya imani za kishirikina vimeshamiri
No comments:
Post a Comment