Wednesday, February 20, 2013

Naibu Waziri wa TAMISEMI ataka watendaji wa vijiji Singida kufanya kazi ya kuandikisha wanafunzi wa madarasa ya awali na msingi.


Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe. Kassim Majaliwa (Mb), akizungumza na walimu wakuu wa shule za sekondari mkoa wa Singida na baadhi ya watendaji wa sekta ya elimu. Mazungumzo hayo ambayo yalikuwa ni pamoja na kuweka mikakati ya kuinua taaluma mkoani Singida yamefanyika kwenye ukumbi wa mikutano wa ofisi ya mkuu wa mkoa mjini Singida. Kushoto ni kaimu mkuu wa mkoa wa Singida ambaye pia ni mkuu wa wilaya ya Ikungi, Manju Msambya na Kulia ni katibu tawala mkoa wa Singida, Liana Hassan.
Baadhi ya walimu wakuu wa shule za sekondari mkoa wa Singida wakimsikiliza kwa makini Mh. Kassim Majaliwa (hayupo kwenye picha). (Picha na Nathaniel Limu).
Na Nathaniel Limu.
Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe. Kassim Majaliwa, amesema kuanzia sasa kazi ya kuandikisha wanafunzi kuanza madarasa ya awali na yale ya msingi, itafanywa na watendaji wa vijiji na si walimu wakuu wa shule za msingi.
 Majaliwa amesema hayo wakati akizungumza na walimu wakuu wa shule za sekondari na baadhi ya viongozi wa sekta ya elimu mkoani Singida.
Amesema kutokana na ukweli huo, serikali  itafanya kazi ya uandikishaji watoto wenye sifa ya kuanza madarasa ya awali na yale ya msingi, ni watendaji wa vijiji na kazi hiyo, itakuwa na ufanisi mkubwa kuliko kipindi cha miaka ya nyuma.
Aidha, Naibu Waziri huyo amesema kuwa kila mtendaji wa kijiji anapaswa kuwakilisha ripoti ya kazi ya uandikishaji wanafunzi wa shule za awali na wale wa msingi mbele ya kikao cha maendeleo ya kata (WDC)  ili kupata Baraka ya kikao hicho.
 Majaliwaa mesema ili kuipa umuhimu mkubwa elimu ya awali ni lazima kuwepo na bajeti ambazo zitaonyesha ongezeko la shule za awali.
 Katika hatuna nyingine, Naibu Waziri huyo amekumbusha kuwa kila shule ya msingi ni lazima iwe na vyumba vya kutosha vya madarasa ya awali.
Mh. Majaliwa amesema wanafunzi wa shule za awali sio walundikwe tu madarasani au wawe wa kucheza tu kipindi chote wawapo shuleni, hapana, ihakikishwe wanasoma kikamilifu ili wakianza darasa la kwanza katika shule za msingi, wawe wameiva barabara.

No comments:

Pro

PropellerAds

LinkWithin

Soma na Hizi Pia Plugin for WordPress, Blogger...