Maafisa zaidi wa polisi wametumwa katika maeneo yenye mashambulio dhidi ya raia wa kigeni nchini Afrika Kusini. Yamkini
watu sita wameuawa na makundi yenye silaha, ambayo yanawalaumu
wahamiaji wa kiafrika kwa kuchukua kazi zao nchini Afrika Kusini.
Rais
Jacob Zuma amewatembelea watu hao walioathirika na ghasia hizo, mauwaji
pamoja na kuibwa kwa mali zao huku akiahidi kukabiliana vilivyo na
wimbi la mashambulio hayo.
Bwana Zuma alifutilia mbali ziara yake nchini Indonesia, ili kukabiliana na vurumai hizo zilizoanza majuma mawili yaliyopita.
Yamkini
watu sita wameuawa na makundi yenye silaha, ambayo yanawalaumu
wahamiaji wa kiafrika kwa kuchukua kazi zao nchini Afrika Kusini. Nchini Harare Rais wa Zimbabwe, Robert Mugabe, alilaani ghasia hizo.
Ghasia
hizo zilianza baada ya mfalme mmoja wa Kizulu, Goodwill Zwelethini,
kusema kuwa raia wa kigeni sharti waondoke Afrika Kusini. Akiongea
katika kambi hiyo iliyoko mjini Durban kiongozi mkuu wa jimbo la
Gauteng, David Makhura, anasema kuwa uhasama na ghasia hizo
zinazoshuhudiwa, haundamani na uhuru wa miaka mingi ambayo Afrika Kusini
ilipigania. Tangaza biashara yako hapa kwa bei nafuu zaidi, pia usisahau ku-Like Ukurasa Wetu Wa Facebook Kwa Kubofya/ Click Neno Jambo Tz.