Sunday, December 01, 2013

CHADEMA YATOA UFAFANUZI KUHUSU TAARIFA YA NDUGU ALI O. CHITANDA


UFAFANUZI KUHUSU TAARIFA YA NDUGU ALI O. CHITANDA Kutokana na kuwepo kwa taarifa ya Ndugu Ali Omari. Chitanda, huku pia waandishi wa habari wakitaka kujua na kupata ukweli kutoka Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA, tunapenda kutoa ufafanuzi mfupi; Kwanza suala la maamuzi ya Kamati Kuu ya kuwavua uongozi ndani ya chama, Ndugu Zitto Kabwe na Dkt. Kitila Mkumbo, chama kimeshafunga mjadala kwenye vyombo vya habari kwa kuheshimu na kuzingatia taratibu za kikatiba za ndani ya chama kuendelea. Pili kuhusu suala la restructuring ya Makao Makuu ya Chama. Chitanda ametoa taarifa akiwataja wakurugenzi wafuatao, kuwa ni wapya; 1.Mkurugenzi wa Oganaizesheni Mhe. Singo Kigaila Benson.
2. Mkurugenzi wa Mawasiliano na Mahusiano ya ndani Mhe. John Mnyika
3. Mkurugenzi wa Fedha na Uwekezaji Mhe. Anthony Komu.
4. Mkurugenzi wa Bunge na Halmashuri Mhe. John Mrema.
5. Mkurugenzi wa Ulinzi na Usalama Mhe. Wilfred Lwakatale.

Wakurugenzi wote aliowataja si wapya. Mkurugenzi pekee ambaye uteuzi wake ni mpya na umefanyika hivi karibuni na kuthibitishwa ni Mwanasheria Peter Kibatala, atakayesimamia Kurugenzi ya Sheria na Haki za Binadamu.

CHADEMA YAZIDI KUPUKUTIKA .... KATIBU WA WILAYA CHADEMA AJIUNGA NA CCM

 Katibu wa chama cha CHADEMA wilaya ya Chunya, Bwa. Bryson Mwasimba akionesha kadi yake ya chama hicho akiirejesha kwa chama cha CCM,mara baada ya kuachia ngazi, kwenye mkutano wa hadhara uliofanywa na Katibu Mkuu wa CCM, Ndugu Abdulrahman Kinana, uliofanyika kwenye kata ya Lupa Tinga Tinga, Wilaya ya Chunya mkoani Mbeya. 
Ndugu Kinana na ujumbe wake yuko mkoani Mbeya kwenye ziara kukagua utekelezaji wa Ilani ya chama, kukagua miradi mbalimbali ya chama na wananchi sambamba na kusikiliza matatizo ya wananchi na namna ya kuyatafutia ufumbuzi.
Katibu Mkuu wa CCM, Ndugu Abdulrahman Kinana akimkabidhi kadi ya chama cha CCM, Katibu wa chama cha CHADEMA Wilayani Chunya, Bwa. Bryson Mwasimba aliyeamua kujiuzuru wadhifa wake mapema leo na kurejea CCM, huku umati mkubwa wa watu uliofika kwenye mkutano wa hadhara ukishangilia kwa mayowe na miluzi, uliofanywa na Katibu Mkuu wa CCM, Ndugu Abdulrahman Kinana, uliofanyika kwenye kata ya Lupa Tinga Tinga, Wilaya ya Chunya mkoani Mbeya.
 Bwa. Bryson Mwasimba akionesha kadi ya CCM mara baada ya kutangaza kuachia ngazi CHADEMA.
 Bwa. Bryson Mwasimba akizungumza mbele ya wananchi na wanachama wa CCM kuhusiana na kuachia ngazi kwake na kurejea chama cha CCM mapema leo. CHANZO MICHUZI JR

MH. ZITTO AELEZA MAMBO YANAYOMMALIZA KISIASA...!!!


Zitto-Kabwe_46197.jpg
Mbunge wa Kigoma Kaskazini, Zitto Kabwe amesema tuhuma alizosomewa na uongozi wa Chadema katika kikao cha Kamati Kuu sizo zilizoelezwa na chama hicho mbele ya waandishi wa habari na viongozi wa chama hicho.
Aidha, amesema kuwa vita aliyopo siyo kati ya Chadema na Zitto, bali ni vita ya watu wengi, akitaja magenge ya watu wanaotaka urais 2015 na walioficha fedha nje ya nchi walioungana wakiona tatizo lao ni yeye hivyo kutaka kumwondoa bungeni.
Akizungumza katika mahojiano maalumu na gazeti la Mwananchi kwa njia ya simu, Zitto alisema kuwa hadi sasa bado hajapokea tuhuma 11 anazokabiliwa nazo, hivyo hajui makosa hayo na bado anasubiri akabidhiwe kwa maandishi.
Ana ugomvi gani na viongozi wenzake?
Alipotakiwa kueleza iwapo ana ugomvi na watu ndani ya Chadema, Zitto alisema kuwa huenda mambo hayo yanatokea kwa sababu mahasimu wake wa kisiasa wa ndani na nje wameamua kuungana na kupambana naye ili kumdhoofisha kisiasa kwa masilahi yao.
"Matatizo yaliyopo ni mafanikio yangu, .... nadhani hii siyo vita kati ya Chadema na Zitto, bali ni vita ya watu wengi, pengine magenge ya watu wanaotaka urais na wale walioficha fedha zao nje wamekaa pamoja wanaona tatizo lao ni Zitto... wanajua siwezi kusemea nje maana sina kinga..., hivyo wanataka kuniondoa bungeni..." alisema.

Aliongeza kuwa kwenye siasa kinachohitajika ni kusimamia misingi, jambo alilosema binafsi amekuwa akilifanya katika kipindi chake chote cha kisiasa.
Zitto alisema kuwa ni vyema wananchi wakawapima wabunge wao kwa kazi wanazozifanya bungeni akibainisha kuwa kati ya mwaka 2011 hadi 2013, yeye amewasilisha hoja nyingi nzuri zilizo na mashiko ikilinganishwa na wabunge wenzake wanaomtuhumu kutumiwa na CCM.

MAGAZETI YA LEO JUMAPILI DESEMBA 01, 2013

.
.



Saturday, November 30, 2013

MPANGO WA SARAFU MOJA WA EAC KUJADILIWA LEO JIJINI KAMPALA

 Wakuu wa Nchi Tano Wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC), leo Novemba 30, wanatarajiwa kutia saini mkataba wa kuwa na sarafu moja.
Mkuu wa Idara ya Uhusiano na Mawasiliano wa EAC, Richard Owora aliwaambia waandishi wa habari jijini hapa kuwa sherehe za kutia saini mkataba huo utakaoanzisha mchakato wa miaka kumi hadi kufikia lengo la kuwa na sarafu moja ya EAC, zitafanyika katika Viwanja vya Kololo jijini Kampala.
Marais Jakaya Kikwete wa Tanzania, Yoweri Mseveni wa Uganda, Paul Kagame wa Rwanda, Pierre Nkuruzinza wa Burundi na Uhuru Kenyatta wa Kenya wanatarajiwa kuwa jijini hapa kuhudhuria mkutano wa mwaka wa wakuu wa nchi za EAC.
Umoja wa sarafu ni moja kati ya mambo makuu manne yaliyoainishwa katika mkataba wa EAC. Masuala mengine ni soko la pamoja na umoja wa forodha ambayo tayari mikataba yake imesainiwa na kuanza kutekelezwa, ingawa kwa kasi isiyotosheleza kutokana na vikwazo kadhaa.
Hatua ya mwisho na juu kabisa katika ushirikiano wa Jumuiya ya Afrika Mashariki ni shirikisho la kisiasa linalolenga kuwa na nchi moja, hatua itakayozihakikishia nchi za ukanda huo nguvu ya soko, biashara, majadiliano na uamuzi katika ngazi ya ndani na kimataifa.
Huu ni mkutano wa kwanza kuwakutanisha wakuu wote wa EAC tangu kuibuka kwa migongano ya kimawazo na mtazamo miongoni mwao kuhusu utekelezaji wa makubaliano na miradi iliyo katika mipango ya EAC pamoja na njia bora na sahihi ya kumaliza vita na migogoro ya wenyewe kwa wenyewe ndani ya baadhi ya nchi wanachama.

MAGAZETI YA LEO JUMAMOSI NOVEMBA 30, 2013 YA UDAKU, MICHEZO NA HARD NEWS


.
.
.

Friday, November 29, 2013

WATANZANIA WENGINE WANASWA NA "UNGA" AFRIKA KUSINI

Kamanda wa Kikosi cha Kuzuia Dawa za Kulevya, Godfrey Nzowa (katikati) akiangalia dawa za kulevya aina ya heroine zilizokamatwa nchini, zikifunguliwa na afisa wa jeshi la polisi Neema Mwakagendi kabla ya kuteketezwa jana, katika tanuri la Kiwanda cha Saruji wazo jijini Dar es Salaam.Dawa aina mbalimbali zilizokamatwa ziliteketezwa. Picha na Juliana Malondo 
********
Watanzania wawili wanahojiwa na Polisi wa Afrika Kusini baada ya kukamatwa jana na kilo 55 za dawa za kulevya.
Watu hao wawili wanatazamiwa kufikishwa mahakamani kesho kujibu tuhuma za kukamatwa na dawa hizo zenye thamani ya Rand75 milioni (Sh11.7 bilioni).

Maofisa wa Kikosi Maalumu cha Kupambana na Makosa ya Jinai na Rushwa cha Afrika Kusini (The Hawks), kiliwakamata watu hao katika Kitongoji cha Kempton Park, Ekurhuleni, Jimbo la Gauteng.

MAGAZETI YA LEO IJUMAA NOVEMBA 29 2013 UDAKU, MICHEZO NA HARDNEWS

.

.

KIJANA WA MIAKA 21 ATUHUMIWA KUMUUA BOSS WAKE KWA KOSA LA KUULIZWA UMECHELEWA WAPI....!!!

DV7A2649 6bcea
Kijana Daniel Kossam (21) anayetuhumiwa kumuua bosi wake Bi. Pelesi Chaula (32) akiwa chini ya polisi kwenda kuonyesha pesa na simu alivyotumbukiza chooni.
DV7A2851 b8fdc
Marehemu Bi. Pelesi Chaula (32) enzi za uhai wake
Na Uswege Luhanga
Kijana Daniel Kossam (21) anatuhumiwa wa kumuua bosi wake Bi. Pelesi Chaula (32) ambaye alikuwa akiishinaye nyumba moja huko mtaa wa Ilembo kata ya Iyela mkoani Mbeya. Daniel alikuwa akiuza duka la vifaa vya pikipiki la bi. Pelesi lijulikanalo kwa jina la 'Twiyanze' lililopo kijiji cha Mbalizi nje kidogo ya jiji la Mbeya. 

Chanzo cha ugomvi inadaiwa kuwa ni kuchelewa kurudi nyumbani kijana huyo ndipo Pelesi alipochukua jukumu la kumuuliza jambo lililozua ugomvi katiyao na kusababisha kifo cha bi. Pelesi Chaula. Kifo cha marehemu Pelesi kimetokana na kupigwa na kitu chenye ncha kali mwilini mwake. Wakati mauaji hayo yanafanyika mume wa bi Pelesi Chaula alikuwa safarini wilayani Makete mkoani Iringa.
Baada ya mauaji hayo Kijana Daniel alichukua simu mbili za marehemu na simu yake pamoja na fedha kiasi cha 114, 000/= na kuzitumbukiza chooni kisha alienda kwa jirani kuwajulisha kuwa walikuwa wamevamiwa na majambazi na kwamba wamemuua bosi wake huyo.
Majirani walipofika eneo la tukio walishangaa kuona kuwa hakuana sehemu ya nyumba iliyokuwa imevunjwa, walipo muuliza Daniel alijibu kuwa alisahau kufunga milango, baaada ya majibu hayo waliingiwa na mashaka na kuamua kutoa taarifa polisi.

Akizungumza na mwandishi wa habari hizi Mjumbe wa serikali ya mtaa Bi. Neema Mwasampeta alisema, 'Dan alichelewa kurudi na alifokewa sana,nadhani hicho ndiyo chanzo cha ugonvi wao'. Aliongeza kuwa alimjua kijana huyo kwa muda wa mwaka mmoja.

HUU NI WAKATI WA KUTANGAZA BIASHARA YAKO KITAIFA NA KIMATAIFA


Jambo Tz Blog tunapenda kuwatangazia wasomaji wetu wote kuwa kuna punguzo maalum ya funga na fungua Mwaka kwa kutangaza nasi ndani ya blog. Wahi sasa tangaza biashara yako. Ofa hii inaanza leo hii mpaka 2o January 2014.

Wasiliana nasi:+ 255 715 22 11 98 au + 255 766 22 11 98
Email: jambotz8@gmail.com / kenypino2@yahoo.com

Ahsante.

JACQUELINE WOLPER AANIKA SIRI ZA WAPENZI WAKE, AMTAJA ALIYEMFUNDISHA MAPENZI NI STAA WA MUZIKI WA BONGO FLAVA....!!!

MOYO huhifadhi mengi mazito hasa ya kuumiza! Staa mkubwa wa sinema za Kibongo, Jacqueline Wolper Massawe amejikuta akimwaga machozi wakati akianika siri tano nzito kuhusu mapenzi katika mahojiano (exclusive interview) na Amani kwa takriban saa mbili.
 
Wolper akifunguka
Katika ‘intavyu’ hiyo iliyofanyika Jumatatu iliyopita kwenye Ofisi za Global Publishers, Bamaga-Mwenge jijini Dar kuanzia saa 8:44 alasiri hadi saa 10:44 jioni, Wolper alifunguka vitu vingi.
KISA/MKASA
Akizungumza kwa masikitiko, uchungu na majuto, Wolper alisema hawezi kumsahau mwanaume huyo ambaye ni Abdallah Mtoro ‘Dallas’ kwa namna alivyomwingia kijanja na kutaka kumvunjia heshima aliyoijenga karibia miaka kumi nyuma.
 
Wolper akijibu maswali ya waandishi.
ALIANZIA WAPI NA DALLAS?
“Siku ya kwanza Dallas alinipigia simu na kuniambia aliniona Magomeni (Dar). Naikumbuka sana siku hiyo, ilikuwa baada ya mizunguko yangu, mwanzoni sikupokea simu yake kwa sababu ilikuwa namba ngeni kwangu.

Wednesday, November 27, 2013

SERIKALI YATANGAZA NAFASI MPYA 2,748 ZA KAZI ... FUNGUA HAPA KUZIONA NA NAMNA YA KUZIOMBA

Serikali kupitia Ofisi ya Rais Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma inawatangazia watanzania wenye sifa na uwezo kujaza jumla ya nafasi wazi za kazi 2,748 kwa ajili ya waajiri mbalimbali Nchini.
Kwa mujibu wa Katibu wa Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma Bw. Xavier Daudi nafasi hizo za kazi ambazo zinapatikana katika tovuti ya Sekretarieti ya Ajira ambayo ni www.ajira.go.tz ni kwa ajili ya waajiri mbalimbali wa Ofisi za Umma.
Daudi alitaja nafasi za kazi zinazotangazwa kuwa ni Afisa Uvuvi daraja la ii, Mvuvi msaidizi daraja la ii, Afisa Mifugo msaidizi daraja la ii, Afisa mifugo daraja la ii, Mteknolijia wa samaki daraja la ii, Daktari wa mifugo daraja la ii,Afisa utafiti Mifugo daraja la ii, Daktari utafiti Mifugo daraja la ii, Fundi sanifu Maabara Mifugo daraja la ii, Mkufunzi Mifugo daraja ii, Mkufunzi wa Mifugo msaidizi na Daktari Mifugo.

Kada nyingine ni Mkufunzi daraja la ii, Mtekinolojia wa Samaki msaidizi daraja la ii, uunda boti daraja ii, nafasi 2, Dereva wa vivuko daraja la ii, msaidizi mifugo,afisa kilimo daraja la ii, Afisa kilimo msaidizi daraja la ii, Mhandisi kilimo daraja la ii, Fundi sanifu daraja la ii, Afisa utafiti kilimo daraja la ii, Mkufunzi wa kilimo msaidizi, Afisa kilimo msaidizi daraja la iii,Dereva daraja la ii, mlinzi, Mhasibu mkuu daraja ii, Msanifu lugha mkuu iii na Afisa vipimo

SOMA MASHITAKA 11 YA MH. ZITTO NA DK. KITILA


Mwanasheria Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Tundu Lissu, akionyesha nakala ya kile alichokieleza kuwa ndiyo mpango wa mabadiliko 2013 uliosababisha adhabu ya kuvuliwa nyadhifa za aliyekuwa Naibu Katibu Mkuu wa chama hicho, Zitto Kabwe, na Dk. Kitila Mkumbo, wakati akizungumza na waandishi wa habari makao makuu ya chama hicho, Kinondoni jijini Dar es Salaam jana. Kushoto ni Mkurugenzi wa Habari wa chama hicho, John Mnyika.
Hatimaye Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kimewaandikia barua aliyekuwa Naibu Katibu Mkuu, Zitto Kabwe, na aliyekuwa Mjumbe wa Kamati Kuu, Dk. Kitila Mkumbo, ambao wiki iliyopita walivuliwa nafasi za uongozi, zinazoeleza mashtaka ya makosa 11 wanayotuhumiwa kuyatenda dhidi ya chama hicho.  
*****
Mkurugenzi wa Habari na Uenezi wa Chadema, John Mnyika, alisema barua hizo, ambazo Zitto na Dk. Mkumbo, walitarajiwa kukabidhiwa jana, zinawataka wajieleze kwa nini wasichukuliwe hatua zaidi, ikiwamo kufukuzwa uanachama.

Alisema hayo alipozungumza na waandishi wa habari, jijini Dar es Salaam jana, siku mbili baada ya Zitto na Dk. Mkumbo, kuitisha mkutano na waandishi wa habari, Jumapili wiki iliyopita na kusema hadi siku hiyo walikuwa hawajapata barua hizo zaidi ya kusikia suala hilo kwenye vyombo vya habari.

MAGAZETI YA LEO JUMATANO NOVEMBA 27, 2013 YA UDAKU, MICHEZO NA HARD NEWS

.
.
.

Pro

PropellerAds

LinkWithin

Soma na Hizi Pia Plugin for WordPress, Blogger...