Lema akiongozana na wanafunzi wa chuo cha uhasibu
baada ya wanafunzi hao kumpokea juzi chuoni hapo
Arusha,Tanzania
MAMBO yamezidi kumwendea kombo Mbunge wa Arusha Mjini,
(Chadema) Godbless Lema baada ya Jeshi la Polisi kutangaza rasmi kwamba
itamfikisha Mahakamani, siku ya Juma tatu.
Mwanadishi wa Habarimpya.com mjini Arusha anasema kwamba, Kamanda wa
Polisi Mkoa wa ArushaLiberatus
Sabas amema kwamba Mbunge huyo hawezi kuachilia huru kwa sababu mashtaka
dhidi yake yameshakamilika na atafikishwa Mahakamani siku ya Juma
tatau.
"Hatuwezi
kumwachia kwa sababu anatarajia kufikishwa mahakamani kujibu tuhuma
zinazomkabili" alisema Sabas.
Wakati Kamanda huyo
akitoa msimamo huo, taarifa za ndani ya Jeshi hilo zinaeleza kwamba
Mbunge huyo amehojiwa kwa zaidi ya saa nane sasa na bado yuko katika
chumba maalum kwa mahojiano zaidi na maofsa wa Polisi huku akitakiwa
kuonyesha ujumbe mfupi wa vitisho aliyodaiwa kuwa ametumiwa na Mkuu wa
Mkoa wa Arusha Magesa Mulongo.
Katika hatua nyingine Kamati ya Ulinzi na Usalama wa
Mkoa wa Arusha, kimekuwa na kikao kirefu kinachoongozwa na Mkuu wa Mkoa
Mulongo na kwamba ajenda kubwa inayojadiliwa ni tukio zima la vurugu
zilizotokea katika Chuo cha Uhasibu mkoani humo. Lema alikamatwa
usiku wa kuamkia leo baada ya Askari wa Jeshi la Polisi kumfuata
nyumbani kwake na kuzingira nyumba yake kabla ya zoezi la kumchomoa
ndani ya nyumba hiyo kufanyika.
Mbunge huyo anatuhumiwa kwa makosa mbalimbali ikiwemo
kosa la kuchochea vurugu katika chuo hicho baada ya kutokea mauaji ya
Mwanafunzi Henry Koga aliye uawa kwa kuchomwa kisu juzi akirejea chuoni
hapo kutoka kwenye matembezi yake, hata hivyo haijajulikana mara moja
sababu za kuawa kwa mwanafunzi huyo wala watuhumiwa hawajakamatwa.