LULU AINGIA MZIGONI RASMI NA KUFYATUA FILAMU YAKE........!!!
HATIMAYE staa wa filamu za Kibongo, Elizabeth
Michael ‘Lulu’ ameingia mzigoni na kufyatua filamu yake mpya baada ya
kimya cha muda mrefu, Amani limeinyaka.
Kwa mujibu wa mtandao wake wa kijamii wa Instagram, Lulu
alitupia picha akiwa ‘location’ kuashiria kwamba amerudi kazini baada
ya kusimama kuigiza kwa muda mrefu.
Baadhi ya picha
hizo zinamuonesha Lulu akiwa na staa mwingine wa filamu Bongo, Hashimu
Kambi mbele ya kamera kwa ajili ya kushuti filamu hiyo ambayo jina
lake halijapatikana.
Mara baada ya kutupia picha hizo mtandaoni, watu
mbalimbali walimtumia ujumbe kumsifia kwa kumwambia kuwa ana kipaji cha
kazi hiyo.

Miss Tanzania namba mbili 2006, Jokate Mwegelo naye
alichangia mada hiyo na kumsifu Lulu kwa uwezo wake wa kuigiza.
Lulu
amekuwa kimya kwa muda mrefu baada ya kupata msala wa kumuua bila ya
kukusudia staa mwingine wa filamu za Kibongo, Steven Kanumba, Aprili 7,
mwaka jana, hivi sasa yuko nje kwa dhamana.
No comments:
Post a Comment