Kutokana na kuwepo kwa uvumi wa kufanyiwa upasuaji wa kurekebisha sura
yake Nicki Minaj awatimuwa kazi watengeneza nywele pamoja na wapambaji
wake muda mfupi kabla ya kupanda jukwaani
Nicki amewatimuwa wafanyakazi wake hao siku moja baada ya rapa huyo
kusema kwamba hajafanyiwa upasuaji wowote wa kurekebisha sura yake
Chanzo cha habari kinasema kuwa "Nicki anajaribu kutengeneza hali ambayo
watu wanamuheshimu kama msanii amemfukuza kazi mtengeneza nywele wake
wa muda mrefu"
"Nicki anaamini kwamba sasa amemalizana na masuala ya American Idol
hivyo watu wataanz kumuangalia kwa jicho la tatu kipindi hiki ambacho
anapanga kutoa albamu yake mpya ya Hip Hop
Tuesday, March 05, 2013
Uchaguzi wa rais nchini Kenya Uhuru Kenyatta aendelea kuongoza huku bado kura zikiwa bado zinaendelea kuhesabiwa.
Zoezi la kuhesabu kura linaendelea nchini Kenya kufuatia uchaguzi mkuu uliofanyika siku ya Jumatatu.
Maafisa
wa uchaguzi wamesema zaidi ya asilimia 70 ya watu milioni 14.3
waliojiandikisha kupiga kura walijitokeza katika uchaguzi huo.
Matokeo
ya awali yanaonyesha kuwa mgombea urais kupitia muungano wa kisiasa wa
Jubilee Bw. Uhuru Kenyatta anaongoza kwa asilimia 55 dhidi ya mpinzani
wake Waziri Mkuu Raila Odinga wa muungano wa kisiasa wa CORD akiwa na
asilimia 40.
Hata
hivyo, muungano wa CORD tayari umeelezea wasiwasi wake kuhusu matokeo
hayo na kutilia shaka mfumo mzima wa utoaji wa matokeo hayo.
Hata
hivyo Mwenyekiti wa Tume Huru ya Uchaguzi na Mipaka ya Kenya-IEBC
Isaack Hassan amesisitiza kuwa matokeo hayo ni ya awali tu.
Mshindi
katika uchaguzi huo, anatakiwa kupata zaidi ya asilimia 50 ya kura la
sivyo wagombea wawili wa juu watalazimika kuingia katika awamu pili ya
uchaguzi mwezi Aprili mwaka huu.
SAKATA LA DIAMOND PLATNUM KUMDHURUMU MENEJA WAKE
Raque akiwa na Diamond kwenye interview
Meneja wa Diamond Platnumz, Raqey Mohamed amelazimika kutumia mtandao wa Facebook kukanusha habari iliyoandikwa na gazeti la udaku la ‘Jumatatu’ kuwa ametapeliwa na Diamond. Amesema Diamond ni mchapakazi na mwaminifu na mkataba wao hauhusiani na mtu yeyote.
Raqey ameandika, “this is coming from me Raqey known as Diamond Platnumz Manager, hakuna ukweli wowote juu ya habari hii, Diamond is a hard working kind and loyal. Our contract has nothing to do with anybody. If you want to write a story at least pay a visit to my studio or call me before you write a story.”
Bongo imempigia simu Raqey ambaye ameendelea kusisitiza kuwa habari hiyo ni ya uzushi na ya upuuzi mtupu.
Meneja wa Diamond Platnumz, Raqey Mohamed amelazimika kutumia mtandao wa Facebook kukanusha habari iliyoandikwa na gazeti la udaku la ‘Jumatatu’ kuwa ametapeliwa na Diamond. Amesema Diamond ni mchapakazi na mwaminifu na mkataba wao hauhusiani na mtu yeyote.
Raqey ameandika, “this is coming from me Raqey known as Diamond Platnumz Manager, hakuna ukweli wowote juu ya habari hii, Diamond is a hard working kind and loyal. Our contract has nothing to do with anybody. If you want to write a story at least pay a visit to my studio or call me before you write a story.”
Bongo imempigia simu Raqey ambaye ameendelea kusisitiza kuwa habari hiyo ni ya uzushi na ya upuuzi mtupu.
JOHN MNYIKA APANGA KUITISHA MAANDAMANO MAKUBWA MACHI 26
Mbunge
wa Jimbo la Ubungo JOHN MNYIKA amesema Ofisi yake imepanga kuitisha
Maandamano makubwa Machi 16 Mwaka huu kuelekea Ofisi za Wizara ya Maji,
kutokana na Wizara hiyo kushindwa kulipatia ufumbuzi suala la
upatikanaji wa Majisafi pamoja na uondoaji wa Majitaka katika maeneo
mbalimbali ya Jimbo hilo.
Akizungumza na CLOUDS FM, MNYIKA
amesema kuwa tayari Ofisi yake imekamilisha hatua za msingi za uratibu
wa maandano hayo, ikiwa ni pamoja na kulishirikisha Jeshi la Polisi
pamoja na Uongozi wa Manispaa ya Kinondoni.Endelea kupiti audifacejackson blog ..Amebainisha
kuwa licha ya ofisi yake kulifikisha suala la tatizo la Maji katika
baadhi ya maeneo ya Jimbo hilo Wizarani sambamba na kuwasilisha hoja
Binafsi bungeni, hakuna hatua zozote za awali zilizochukuliwa huku
Wakazi wa maeneo hayo wakitaabika kwa kukosa maji.
SHULE INA WALIMU 8 WA KIKE,6 KATI YAO NI WAJAWAZITO WAOMBA MSAADA
SERIKALI
imeombwa iwapatie walimu wa kiume Shule ya Msingi Orbili, kutokana na
walimu wote wanawake wa shule hiyo kupata ujauzito na hawafundishi hivi
sasa.
Ombi hilo limetolewa na wakazi wa Kijiji cha Orbili Kata ya
Shambarai wilayani Simanjiro mkoani Manyara.
Wakazi
hao ambao hawakutaka kutaja majina yao wakati wakiongea na waandishi wa
habari, walisema kuwa shule hiyo ina walimu nane, ambapo wanaume ni
wawili na wanawake ni sita, akiwemo Mwalimu Mkuu, wote wana ujauzito.
Walisema
walimu wawili wanaume, hawawezi kuwafundisha wanafunzi wote
wa shule hiyo kuanzia darasa la kwanza hadi la saba, hasa ukizingatia
kuwa darasa la nne na la saba, watafanya mtihani wa Taifa mwaka huu.
Walisema
kuwa hivi karibuni Mwalimu Mkuu wa shule hiyo, alijifungua mtoto na
walimu wengine watano waliobaki, wanatarajiwa kujifungua wakati wowote.Endelea kupiti audifacejackson blog
“Nadhani shule hii
ifungwe ili Serikali ilete walimu wengine kwani hawa walimu wenye mimba
hawafundishi wanafunzi wetu, wenyewe wamebaki kula udongo na malimao,” alisisitiza mkazi mmoja.
SOURCE::HABARI LEO:
President Kikwete Meets With MCC Officials In Dar Es Salaam.
President
Jakaya Mrisho Kikwete greets Mr Steve Kaufman, the Millenium Challenge
Corporation’s Chief of Staff, who paid him a visit at the State House in
Dar es salaam March 4, 2013. Centre is the US Ambassador to Tanzania,
Mr Alfonso Lenhardt.
President
Jakaya Mrisho Kikwete holds talks with (from left) Mr Steve Kaufman,
the Millenium Challenge Corporation’s Chief of Staff, MCC’s Vice
President for East and Southern Africa, Mr Andrew Mayock,the US
Ambassador to Tanzania, Mr Alfonso Lenhardt. and Mr Matt KAvanagh, MCC
Resident Country Director , who paid him a visit at the State House in
Dar es salaam March 4, 2013. Centre is the US Chief of Staff, Ambassador
to Tanzania, Mr Alfonso Lenhardt.
President
Jakaya Mrisho Kikwete in a group photos with (from left) Mr Steve
Kaufman, the Millenium Challenge Corporation’s Chief of Staff (right)
MCC’s Vice President for East and Southern Africa, Mr Andrew Mayock
(second row right),the US Ambassador to Tanzania, Mr Alfonso Lenhardt
(front row left) Mr Matt KAvanagh, MCC Resident Country Director (second
row left) and the Minister for Finance Dr Willim Mgimwa and
Mr Bernard Mchomvu, the CEO of the Millenium Challenge Account (MCA)
-Tanzania, at the State House in Dar es salaam March 4, 2013. Centre
is the US Chief of Staff, Ambassador to Tanzania, Mr Alfonso Lenhardt.(STATE HOUSE PHOTO)
BIFU LA WEMA SEPETU NA AUNTY EZEKIEL!! BIFU: AUNT EZEKIEL NA WEMA SASA..
Wacheza
filamu wenye majina makubwa Bongo, Wema Sepetu na Aunt Ezekiel wadaiwa
kuwa na bifu kubwa kwa sasa. inasemekana bifu hilo lilianza kwenye
mkesha wa mwaka mpya baada ya aunt kutofika kwenye sherehe ya
kukaribisha mwaka mpya iliyoandaliwa nyumbani kwa Wema licha ya kukubali
mwaliko.
Ilipotimu
saa 6:01 usiku bila ya Aunt kuonekana, Wema alimtumia ujumbe mzito
kupitia BBM na Aunt akaanza kuomba radhi na ujumbe wa Wema ulisomeka
hivi: “Hata sina hamu na wewe ila Happy New Year, sihitaji samahani yako
sijui niku-delete?”akimaanisha amfute BBM.
Inasemekana
Wema alikasirika na kuhisi kwamba Aunt aliungana na baadhi ya wasanii
wengine wa Bongo Movie ambao hakuwaalika kwenye shughuli yake kutokana
na kupishana nao
Kiswahili siku za nyuma.
Asubuhi ya
mwaka mpya, Aunt aliandika kwenye mtandao wa BBM maneno ya kuomba radhi
kwa wema; “ Chondechonde my luv, nimekosea mamy naomba unisamehe, naomba
msamaha mbele ya hadhara.”. juhudi za kuomba radhi azikuzaa matunda
kwan Wema hakujibu kitu zaidi ya kumpotezea rafiki yake huyo
MSANII MWINGINE BONGO MOVIE MBURULAS. VIDEO INAYOMUONESHA MSANII WA FILAMU BONGO ( SHAMSA FORD) AKIJIFUNGUA YAVUJA NA KUSAMBAA...
VIDEO
inayomuonesha msanii wa filamu Bongo, Shamsa Ford akijifungua imezua
kizaazaa baada ya mtu asiyejulikana kuichukua bila ridhaa ya mhusika na
kuisambaza kwa watu mbalimbali.
Akizungumzia
suala hilo hivi karibuni, rafiki wa karibu wa Shamsa alisema kuwa,
video hiyo msanii huyo alirekodiwa kwa ajili ya kumbukumbu zake lakini
ameshangaa kusikia kuna baadhi ya watu wanayo.
“Yaani video hiyo imezua kizaazaa, Shamsa
anahaha kumjua aliyeisambaza lakini pia anahakikisha haiwafikiii watu
wengine na vyombo vya habari kwani inamuonesha hatua kwa hatua
akijifungua,” kilisema chanzo hicho
Baada ya kuzipata taarifa hizo, mwandishi
wetu alimtafuta Shamsa ambaye alisema:“Kiukweli nimeumia sana, hiyo
video ni kwa ajili ya kumbumbuku zangu, kwa nini mtu aichukue na
kuisambaza bila ridhaa yangu? Imeniletea matatizo makubwa.”
Source-mpekuzi
Monday, March 04, 2013
TAARIFA KUTOKA TANESCO
Shirika la umeme nchini Tanesco limesema tatizo la ukatikaji wa umeme linaloikabili inchi hivi sasa linatokana na kutumia mitambo ya dharura kuzalisha umeme ambayo inatumia gharama kubwa kuiendesha, matengenezo makubwa yanayoendelea katika kituo cha Ubungo pamoja na uharibifu uliotokea katika mfumo wa Songosongo.
TAZAMA WAKENYA WANAVYOENDELEA KUPIGA KURA LEO KUMPATA MRITHI WA MWAI KIBAKI ANAYEACHIA NGAZI... MAMILIONI WAJITOKEZA... MCHUANO NI MKALI KATI YA MAWAZIRI WAKUU WA SASA UHURU KENYATTA NA ODINGA
Odinga akijaindaa kupiga kura yake |
Uhuru akiendelea na mchakato wa kumchagua mbunge wa Gatundu |
SHEKH ISSA PONDA ANALO SHITAKA LA KUJIBU KATIKA KESI INAYOMKABILI
Baadhi ya wafuasi wa shekh Issa Ponda
wakionyesha mikono huku wakisema takbir wakati shekh ponda akiwa katika
gari la magereza mara baada ya kusomewa shitaka lake na kudai anayo kesi
ya kujibu katika mahakama ya kisutu leo
Askari magereza akimfungua pingu shekh
Issa ponda katika mahakama ya kisutu leo akisubiri kusomewa shitaka
lake la kudaia kuvamia katika eneo la markazi changome bila ruhusa
mwenyewe
Shekh Issa Ponda akisindikizwa na askari wa jeshi la magereza mara baada ya kusomewa shitaka lake leo
WAANDISHI WA HABARI ZA UDAKU, WAMNYIMA RAHA MAMA KANUMBA
Mama
yake mzazi na marehemu Steven Kanumba amesema maswali anayoulizwa kila
mara na waandishi wa habari hasa za udaku humfanya asipitishe siku mbili
bila kulia kutokana na kumkumbuka mwanae kipenzi.
Akiongea na kipindi cha The
Avenue cha TBC 1, mama huyo ambaye hivi karibuni amejiingiza kwenye
uigizaji wa filamu pia amesema mara nyingi anapofuatwa na waandishi wa
habari kumuuliza maswali kuhusiana na mwanae hubaki akilia na waandishi
wa habari huishia kuandika habari za uongo tofauti na alivyoongea.
“Kupoteza mtoto wa miaka 28 sio mchezo, inauma,” alisema Mama Kanumba.
Aliongeza kuwa hawezi kuangalia filamu za mwanae kwakuwa humfanya ajisikie vibaya japo nguo zake bado zipo na huziona kila siku.
WADAU WAMTUPIA MADONGO IRINE UWOYA KWA KUYAANIKA MAKALIO YAKE
Huu ni upotofu mkubwa wa maadili unaoendekezwa na hawa wanaojiita MASTAA.....
Kumbukumbu zangu zinaniambia kuwa Uwoya ni mzazi wa mtoto mmoja ambaye walizaa na Ndikumana na hatimaya wakaachana baada ya kushindana kitabia...
Swali la kujiuliza ni kwamba, Anajisikiaje kuyaanika matako yake kwa mtoto wake wa kumzaa???...Atajenga msingi upi kwa mtoto wake akikua????.....
Achilia mbali mtoto wake, vipi juu ya wazazi wake, wadogo zake, shemeji zake na ndugu na jamaa???...
Irene jitambue.....umri umeenda sasa...unayoyafanya hayaendani na umri wako.....
Umaarufu hauji kwa kukaa uchi.....Wapo akina Lady jaydee, Monalisa....Ni wasanii maarufu pengine kuzidi hata wewe....kwa nini usiige kutoka kwao
Kitendo hiki ni sawa na kuwatusi watazamaji wa filamu zako
UZINDUZI WA CHUO KIKUU CHA TUMAINI MAKUMIRA TAWI LA MBEYA WAFANA
ASKOFU
Mkuu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT), Dkt. Alex
Malasusa akikata utepe kuzindua chuo kikuu cha Tumaini Makumira tawi la
Mbeya
|
Viongozi mbali mbali wa mkoa wa Mbeya walihudhuria uzinduzi huo |
U
Askofu
Mkuu wa Kanisa la Kiluthei Dayosisi ya Konde Askofu Dk. Dr.Israel
Mwakyolile akisoma somo la kwanza katika ibada ya uzinduzi wa tawi hilo
|
ASKOFU Mkuu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT), Dkt. Alex Malasusa Akihubiri katika ibada ya uzinduzi wa tawi la chuo kikuu cha Tumaini Makumira Uyole mbeya |
Subscribe to:
Posts (Atom)