Tuesday, April 19, 2016
WANAFUNZI WATATU WA KIDATO CHA SITA WASHIKILIWA NA POLISI KWA KUIBA SHULENI
Jeshi
la Polisi mkoani Singida linawashikilia wanafunzi watatu wa Shule ya
Sekondari Mwenge mjini hapa kwa tuhuma za kuvunja na kuiba vitu
mbalimbali kwenye ofisi ya usajili wa wanafunzi katika shule hiyo
vinavyokadiliwa kuwa na thamani ya Milioni 1.5.
Kamanda
wa Polisi wa Singida, Thobias Sedoyeka aliwataja wanafunzi hao ambao
wote ni wa kidato chasSita kuwa ni Emmanuel Mwita (19), Erick Dotto (21)
na Pasua Lawrence (20).
Kwa
mujibu wa Kamanda Sedoyeka, tukio hilo lilitokea Aprili, 16 mwaka huu
majira ya saa 3.30 usiku ambapo inadaiwa wanafunzi hao baada ya kuvunja
ofisi hiyo waliiba seti moja ya Kompyuta, “flash disk” yenye ukubwa wa
GB 8, “Extension Cable” na rimu 51 za karatasi. Like page yetu ya facebook Jambo Tz. tu-follow instagram @jambotz.
KANE HAKAMATIKI KWA KUTUPIA NYAVUNI EPL
Harry Kane alikuwa miongoni mwa nyota wakati Spurs ikipata ushindi wa
mabao 4-0 dhidi ya Stoke jana usiku kwenye dimba la Britania baada ya
kuifungia timu yake magoli mawili na kuendeleza ubora wake kwenye ligi
msimu huu.
Inafurahisha kuona jamaa alianza ligi kwa ukame wa magoli katika
mechi kadhaa na baadhi ya watu kuanza kumsema yeye ni mchezaji wa
ku-shine kwa msimu mmoja. Mshambulizi huyo wa England ameendelea
kujitengenezea soko na huenda akawa miongoni mwa wachezaji watakao
gombewa kwa mkwanja mrefu wakati wa usajili wa dirisha la majira ya
joto.
Bayern Munich na Real Madrid inasemekana kuwa ni klabu mbili kubwa
zinazofukuzana kumsaini lakini pia inasemekana Aston Villa wanataka
kuuza washambuliaji wao wote na kuvunja benki kwa ajili ya kuinasa saini
ya mpachika mabao huyo.
Magoli yake mawili ya jana dhidi ya Stoke yamemfanya afikishe jumla
ya mabao 24 na kuongoza orodha ya wapachika mabao akifatimwa na Jamie
Vardy wa Leicester mwenye magoli 22. Like page yetu ya facebook Jambo Tz. tu-follow instagram @jambotz.
TOTTENHAM YAISOGELEA LEICESTER CITY, YAIPIGA STOKE CITY 4-0
Mchezo
mmoja wa Ligi Kuu ya Uingereza umeendelea usiku wa Jumatatu ambapo
Stoke City ilikuwa mwenyeji wa Tottenham Hotspur katika uwanja wake wa
nyumbani wa Britannia.
Mchezo
huo umemalizika kwa wenyeji Stoke City kumaliza mchezo huo kwa kupokea
kipigo kutoka kwa Totenham Hotspur cha goli 4-0, magoli ya Tottenham
yakifungwa na Harry Kane aliyefunga magoli mawili dk. 9 na 71 na mengine
mawili yakifungwa na Dele Alli dk. 67 na 82.
Baada
ya matokeo hayo, Tottenham imefikisha alama 68 ikiwa nyuma kwa alama
tano na viongozi wa ligi, Leicester City ambao wana alama 63, kwa upande
wa Stoke City wao wamemesalia katika nafasi ya tisa ya msimamo wakiwa
na alama 47. Like page yetu ya facebook Jambo Tz. tu-follow instagram @jambotz.
Thursday, April 14, 2016
Monday, April 11, 2016
WATUMISHI HEWA WAMPONZA MAMA ANNA KILANGO MALECELA
Rais wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli ametengua uteuzi wa mkuu wa mkoa wa Shinyanga kutokana na kuwepo kwa watumishi hewa. Bi Anna Kilango Malecela alitangaza kwenye vyombo vya habari kuwa mkoa wake hakuwa na watumishi hewa.
Ikulu hata hivyo ilifanya uchunguzi wake na kubaini kuwepo kwa wafanyakazi hewa 45 katika awamu ya kwanza. Awamu ya pili ya uchunguzi huo bado inaendelea katika wilaya mbili za Ushetu na Shinyanga Vijijini.
Akiongea Ikulu jijini Dar es Salaam, Rais Magufuli amesema
amesikitishwa na hali hiyo na kuagiza mkuu huyo wa mkoa na Katibu Tawala
wa Mkoa Abdul Rashid Dachi kuondolewa kazini mara moja.
"Na wale
wote wa Shinyanga ambao walisemekana ni zero, hakuna mtumishi hewa,
walikuwa tayari wameshalipwa shilingi milioni 339.9, nimejiuliza sana,
na nikajiuliza sana na kwa kweli nimejiuliza sana na kwa masikitiko
makubwa, kwa nini mkuu wa mkoa alisema hakuna mtumishi hewa?" amesema
Dkt Magufuli.
Kwa jumla, zaidi ya wafanyakazi hewa 2,000 waligunduliwa baada ya utathmini kufanywa mikoani. Like page yetu ya facebook Jambo Tz. tu-follow instagram @jambotz.
CHINA KUJENGA VIWANJA 60,000 VYA SOKA KWA MIAKA 6...!!!
China inapania kujenga viwanja 60,000 vya Kandanda katika kipindi cha miaka 6 ijayo.
Uwanja wa taifa wa Beijing
Hayo ni baadhi ya mapendekezo katika ruwaza ya
kandanda ya China ya 2050 ya kuifanya nchi hiyo iwe kati ya mataifa
makuu duniani katika kandanda. Ripoti moja ya serikali imeelezea
mipango ya kuimarisha idadi ya wachezaji na watoto wanaosakata dimba
kutimia watoto milioni 50.
Viwanja elfu 60 vitakarabatiwa na vingine kujengwa upya. Kulingana na ruwaza hiyo China itakuwa na vilabu vyenye hadhi ya kimataifa kufikia mwaka wa 2050. Like page yetu ya facebook Jambo Tz. tu-follow instagram @jambotz
Rais Xi Jinping amenukuliwa akisema kuwa angeli furahishwa mno iwapo
timu ya taifa ya China ingelifuzu tena kwa kombe la dunia la kandanda na
hata kushinda kombe la dunia.
Aidha rais Jinping pia anaitaka kombe la dunia la kandanda liandaliwa nchini mwake. Like page yetu ya facebook Jambo Tz. tu-follow instagram @jambotz
VAN GAL AISIFIA MAN U
Meneja wa Manchester United, Louis
van Gaal amesema hajuti kuangushwa na Tottenham katika msimu huu wa
majira wa 2014, akisema Manchester United ni 'klabu kubwa'. Manchester United wako alama 12 chini ya Spurs baada ya kuchapwa mabao 3-0 katika uwanja wa White Hart Lane siku ya Jumamosi.
'Changamoto
zilikuwa kubwa kwangu katika Manchester United na zitazidi kuwa kubwa'
alisema Van Gaal , wako nafasi ya tano. ''Naomba radhi kwa Tottenham
lakini Manchetser United ni Klabu kubwa'' Ingawaje United wamepata shida nyingi msimu huu ,Van
Gaal , ambaye amekuwa akifanya mazungumzo na Spurs kuhusiana na kuwa
meneja, anaamini United bado wako mbele kwa klabu za Uingereza.
Hata hivyo alimpuuzilia mbali mwanahabari ambaye alimuuliza iwapo anajutia kuchagua United dhidi ya Spurs. 'Ni
jambo la kuudhi kuuliza hivyo,'' meneja huyo mwenye umri wa miaka 64
alisema. Ni rahisi kuuliza, lakini sawa wewe jifurahishe.
Baada ya
Van Gaal kutia sahihi mkataba wa miaka mitatu huko Old Trafford,
Tottenham imemteuwa meneja wa zamani wa Southampton Mauricio Pochettino. Like page yetu ya facebook Jambo Tz. tu-follow instagram @jambotz
Sunday, April 10, 2016
NDANDA KOSOVO AFARIKI DUNIA
Msanii
mkongwe kwa miondoko ya dansi nchini, ambaye aliwahi kuwa katika bendi ya FM
na baadae kuanzisha yake iliyofahamika kwa jina la Stono Musica au
jina linguine Wajela Jela, Ndanda Kosovo amefariki dunia. Like page yetu ya facebook Jambo Tz. tu-follow instagram @jambotz
Katika
taarifa ambayo imetufikia imeeleza kuwa marehemu amefariki jana asubuhi
katika hospitali ya taifa ya Muhimbili alipokuwa amelazwa alipokuwa
amelazwa akisumbuliwa na vidonda vya tumbo. Mungu ailaze roho ya marehemu peponi, Amin.
YANGA YATOKA SARE NA AL AHLY
Mchezo
wa Ligi ya Mabingwa Afrika, hatua ya 16 kati ya wawakilishi pekee wa
Tanzania katika mashindano hayo, Yanga ya Tanzania na wageni Al Ahly ya
Misri umemalizika katika uwanja wa taifa kwa timu hizo kutoka sare ya
goli moja kwa moja.
Katika
mchezo huo, Al Ahly ilikuwa ya kwanza kupata goli kupitia kwa mchezaji
wake Amr Gamal na dakika chache baadae Yanga kusawazisha baada ya
mchezaji wa Al Ahly, Ahmed Hegazy kujifunga dakika ya 16 ya mchezo huo
ambapo mpaka mchezo unamalizika, Yanga 1 na Al Ahly 1
WADHAMINI WA UEFA CHAMPIONS LEAGUE WAJITUPA SOKA LA BONGO
Shirikishio la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) limeishukuru kampuni ya
bia ya Heineken ambao ni wadhamini wakuu wa michuano ya Ligi ya Mabingwa
barani Ulaya (UEFA) kwa kujitolea kufanya ukarabati wa viwanja vitatu
vya mpira wa miguu vilivyopo jijini Dar es salaam.
Katika barua ya Meneja Mkuu wa Heineken nchini Tanzania, Michael
Mbugu kwenda kwa wakurugenzi ya Manispaa wilaya za Ilala na kinondoni,
nakala yake kutumwa kwa Rais wa TFF, imeeleza mdhamini ameelekeza nguvu
zake kwenye kukarabati baadhi ya viwanja nchini ili viwe katika hali
nzuri na salama ili kukuza vipaji vya vijana kwenye mchezo wa soka.
Heineken imelenga kuboresha dhamira yake ya kushirikiana na jamii
sehemu mbalimbali kwa kuchangia ukarabati wa viwanja vya TP Manzese kata
ya Sinza, Sigara Segerea kata ya Tabata Sigara na uwanja wa Magunia
Msasani uliopo kata ya Msasani.
Kufanya ukarabati wa viwanja hivyo kutatoa nafasi kwa vijana wa
maeneo ya Ali Maua, Darajani, Sweet Corner na Kijiweni (uwanja wa TP
Manzese), Macho, Kisiwani, Msasani na Msikitini (uwanja wa Magunia),
Barakuda, Tabata, Senene, Mwembeni, Chang’ombe, Kinyerezi na Segera
(uwanja wa Sigara) kufanya mazoezi na kuendeleza vipaji vya mpira wa
miguu.
Aidha TFF inazipongeza Halmashauri za Manispaa za Ilala na Kinondoni
kwa kupata nafasi ya kufanyiwa ukarabati viwanja vyao na kampuni ya
Heineken, na kuziomba mamlaka hizo kuvitunza viwanja hivyo ili viweze
kutumiwa na vijana wa kike na kiume katika mchezo wa mpira wa miguu. Like page yetu ya facebook Jambo Tz
CRISTIANO RONALDO AANDIKA REKODI MPYA LA LIGA
Cristiano Ronaldo amekuwa mchezaji wa kwanza kufunga mabao 30 ndani
ya misimu sita ya La Liga baada ya Madrid kuichapa Eibar kwa bao 4-0
kwenye mchezo wa ligi. Karim Benema ambaye anapambana na majeruhi ya goti pamoja na Gareth
Bale walipumzishwa wakati Madrid inasubiri mchezo wa marudiano siku ya
Jumanne wa klabu bingwa Ulaya dhidi ya Wolfsburg.
James Rodriguez alianza kuzifungua nyavu za Eibar kwa mkwaju wa mpira
wa adhabu ndogo kabla ya Lucas Vazquez hajapachika bao la pili. Hadi mapumziko tayari Madrid ilikuwa mbele kwa magoli 4-0 huku
Ronaldo akitumbukia nyavuni kupiga bao la tatu akiunganisha pasi ya Jese
ambaye naye alipiga bao na kukamisha idadi ya magoli 4-0.
Real inakumbuka kichapo cha magoli 2-0 kutoka kwa Wolfsburg wakati
ikijiandaa na mchezo wao wa marudiano kwenye uwanja wa Bernabeu huku
kocha wa klabu hiyo Zinedine Zidane kiweka wazi kwamba, endapo
watashindwa kufuzu kwa hatua ya nusu fainali basi msimu wao utakuwa
umemaliza.
Kikosi cha Zidane kwa sasa kipo nyuma ya vinara wa ligi hiyo (Barca)
kwa pointi nne nyuma kikisimama nafasi ya tatu nyuma ya Atletico Madrid. Like page yetu ya facebook Jambo Tz
Saturday, April 02, 2016
MAKONDA ATANGAZA NEEMA KWA BODABODA
Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda amekutana na waendesha bodaboda na kuahidi kushugulikia kero zinazowakabili ikiwemo kuondoa vikwazo vya wao kuingia katikati ya jiji.
Aidha, amewaahidi kuwapatia pikipiki kwa marejesho ya Sh25,000 kwa wiki kwa muda maalum kabla ya kuwaachia kabisa.
Kwa mantiki hiyo, Makonda amewataka kufanya usajili upya na kusajili vituo vyao ili watambulike kisheria huku akisema atawapatia mavazi maalum 'reflectors' kama utambulisho.
Awali, mmoja wa waendesha bodaboda hao, Daud Laurian alimsomea RC Makonda risala iliyoainisha matatizo yao ikiwemo zuio la ya jiji kutokana na agizo la aliyekua mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam, Mecky Sadick Machi 3, 2014.
Waendesha hao wamehaokikishia Makonda kuwa raia wema katika suala zima la ulinzi iwapo Jeshi la Polisi Kanda Maalum litawachukulia kama ndugu zao na marafiki.
Subscribe to:
Posts (Atom)