Cristiano Ronaldo amekuwa mchezaji wa kwanza kufunga mabao 30 ndani
ya misimu sita ya La Liga baada ya Madrid kuichapa Eibar kwa bao 4-0
kwenye mchezo wa ligi. Karim Benema ambaye anapambana na majeruhi ya goti pamoja na Gareth
Bale walipumzishwa wakati Madrid inasubiri mchezo wa marudiano siku ya
Jumanne wa klabu bingwa Ulaya dhidi ya Wolfsburg.
James Rodriguez alianza kuzifungua nyavu za Eibar kwa mkwaju wa mpira
wa adhabu ndogo kabla ya Lucas Vazquez hajapachika bao la pili. Hadi mapumziko tayari Madrid ilikuwa mbele kwa magoli 4-0 huku
Ronaldo akitumbukia nyavuni kupiga bao la tatu akiunganisha pasi ya Jese
ambaye naye alipiga bao na kukamisha idadi ya magoli 4-0.
Real inakumbuka kichapo cha magoli 2-0 kutoka kwa Wolfsburg wakati
ikijiandaa na mchezo wao wa marudiano kwenye uwanja wa Bernabeu huku
kocha wa klabu hiyo Zinedine Zidane kiweka wazi kwamba, endapo
watashindwa kufuzu kwa hatua ya nusu fainali basi msimu wao utakuwa
umemaliza.
Kikosi cha Zidane kwa sasa kipo nyuma ya vinara wa ligi hiyo (Barca)
kwa pointi nne nyuma kikisimama nafasi ya tatu nyuma ya Atletico Madrid. Like page yetu ya facebook Jambo Tz
No comments:
Post a Comment