Jeshi
la Polisi mkoani Singida linawashikilia wanafunzi watatu wa Shule ya
Sekondari Mwenge mjini hapa kwa tuhuma za kuvunja na kuiba vitu
mbalimbali kwenye ofisi ya usajili wa wanafunzi katika shule hiyo
vinavyokadiliwa kuwa na thamani ya Milioni 1.5.
Kamanda
wa Polisi wa Singida, Thobias Sedoyeka aliwataja wanafunzi hao ambao
wote ni wa kidato chasSita kuwa ni Emmanuel Mwita (19), Erick Dotto (21)
na Pasua Lawrence (20).
Kwa
mujibu wa Kamanda Sedoyeka, tukio hilo lilitokea Aprili, 16 mwaka huu
majira ya saa 3.30 usiku ambapo inadaiwa wanafunzi hao baada ya kuvunja
ofisi hiyo waliiba seti moja ya Kompyuta, “flash disk” yenye ukubwa wa
GB 8, “Extension Cable” na rimu 51 za karatasi. Like page yetu ya facebook Jambo Tz. tu-follow instagram @jambotz.
Alisema
kuwa baada ya kuiba vitu hivyo walienda kuvificha kwenye mawe yaliyopo
jirani na shule hiyo. Hata hivyo, alisema kuwa wanafunzi hao walibainika
kutokana na kukuta kandambili ya mmoja wao ikiwa imetelekezwa kwenye
ofisi hiyo ya msajili.
“Baada
ya kuhojiwa, wanafunzi hao walikiri kuwa walihusika na wizi huo na
ndipo walipoenda kuonesha mahali walikoweka vitu hivyo. Pia walikiri
kuvaa vifaa vya kufunika nyuso zao wakati walipoenda kuvunja ofisi hiyo
ili wasiweze kufahamika na mtu yeyote,” alieleza Sedoyeka.
Walipohojiwa
na waandishi wa habari, wanafunzi hao walidai kuwa lengo lao
halikuwa kuiba bali ilikuwa ni kulipiza kisasi tu kutokana na uongozi
wa shule hiyo kutowapa ushirikiano pale walipoenda kutoa taarifa kuwa
wameibiwa vitu mbalimbali mabwenini, zikiwemo fedha. Like page yetu ya facebook Jambo Tz. tu-follow instagram @jambotz.
Na Nathaniel Limu, Singida
No comments:
Post a Comment