Sunday, April 10, 2016

YANGA YATOKA SARE NA AL AHLY

Mchezo wa Ligi ya Mabingwa Afrika, hatua ya 16 kati ya wawakilishi pekee wa Tanzania katika mashindano hayo, Yanga ya Tanzania na wageni Al Ahly ya Misri umemalizika katika uwanja wa taifa kwa timu hizo kutoka sare ya goli moja kwa moja.  
Katika mchezo huo, Al Ahly ilikuwa ya kwanza kupata goli kupitia kwa mchezaji wake Amr Gamal na dakika chache baadae Yanga kusawazisha baada ya mchezaji wa Al Ahly, Ahmed Hegazy kujifunga dakika ya 16 ya mchezo huo ambapo mpaka mchezo unamalizika, Yanga 1 na Al Ahly 1

WADHAMINI WA UEFA CHAMPIONS LEAGUE WAJITUPA SOKA LA BONGO

heineken
Shirikishio la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) limeishukuru kampuni ya bia ya Heineken ambao ni wadhamini wakuu wa michuano ya Ligi ya Mabingwa barani Ulaya (UEFA) kwa kujitolea kufanya ukarabati wa viwanja vitatu vya mpira wa miguu vilivyopo jijini Dar es salaam.

Katika barua ya Meneja Mkuu wa Heineken nchini Tanzania, Michael Mbugu kwenda kwa wakurugenzi ya Manispaa wilaya za Ilala na kinondoni, nakala yake kutumwa kwa Rais wa TFF, imeeleza mdhamini ameelekeza nguvu zake kwenye kukarabati baadhi ya viwanja nchini ili viwe katika hali nzuri na salama ili kukuza vipaji vya vijana kwenye mchezo wa soka.
 
Heineken imelenga kuboresha dhamira yake ya kushirikiana na jamii sehemu mbalimbali kwa kuchangia ukarabati wa viwanja vya TP Manzese kata ya Sinza, Sigara Segerea kata ya Tabata Sigara na uwanja wa Magunia Msasani uliopo kata ya Msasani.
 
Kufanya ukarabati wa viwanja hivyo kutatoa nafasi kwa vijana wa maeneo ya Ali Maua, Darajani, Sweet Corner na Kijiweni (uwanja wa TP Manzese), Macho, Kisiwani, Msasani na Msikitini (uwanja wa Magunia), Barakuda, Tabata, Senene, Mwembeni, Chang’ombe, Kinyerezi na Segera (uwanja wa Sigara) kufanya mazoezi na kuendeleza vipaji vya mpira wa miguu.
 
Aidha TFF inazipongeza Halmashauri za Manispaa za Ilala na Kinondoni kwa kupata nafasi ya kufanyiwa ukarabati viwanja vyao na kampuni ya Heineken, na kuziomba mamlaka hizo kuvitunza viwanja hivyo ili viweze kutumiwa na vijana wa kike na kiume katika mchezo wa mpira wa miguu. Like page yetu ya facebook Jambo Tz

CRISTIANO RONALDO AANDIKA REKODI MPYA LA LIGA

Ronaldo-Rekodi
Cristiano Ronaldo amekuwa mchezaji wa kwanza kufunga mabao 30 ndani ya misimu sita ya La Liga baada ya Madrid kuichapa Eibar kwa bao 4-0 kwenye mchezo wa ligi. Karim Benema ambaye anapambana na majeruhi ya goti pamoja na Gareth Bale walipumzishwa wakati Madrid inasubiri mchezo wa marudiano siku ya Jumanne wa klabu bingwa Ulaya dhidi ya Wolfsburg. 

James Rodriguez alianza kuzifungua nyavu za Eibar kwa mkwaju wa mpira wa adhabu ndogo kabla ya Lucas Vazquez hajapachika bao la pili. Hadi mapumziko tayari Madrid ilikuwa mbele kwa magoli 4-0 huku Ronaldo akitumbukia nyavuni kupiga bao la tatu akiunganisha pasi ya Jese ambaye naye alipiga bao na kukamisha idadi ya magoli 4-0. 

Real inakumbuka kichapo cha magoli 2-0 kutoka kwa Wolfsburg wakati ikijiandaa na mchezo wao wa marudiano kwenye uwanja wa Bernabeu huku kocha wa klabu hiyo Zinedine Zidane kiweka wazi kwamba, endapo watashindwa kufuzu kwa hatua ya nusu fainali basi msimu wao utakuwa umemaliza. 

Kikosi cha Zidane kwa sasa kipo nyuma ya vinara wa ligi hiyo (Barca) kwa pointi nne nyuma kikisimama nafasi ya tatu nyuma ya Atletico Madrid. Like page yetu ya facebook Jambo Tz

Saturday, April 02, 2016

MAKONDA ATANGAZA NEEMA KWA BODABODA

Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda amekutana na waendesha bodaboda na kuahidi kushugulikia kero zinazowakabili ikiwemo kuondoa vikwazo vya wao kuingia katikati ya jiji.

Aidha, amewaahidi kuwapatia pikipiki kwa marejesho ya  Sh25,000 kwa wiki  kwa muda maalum kabla ya kuwaachia kabisa.

Kwa mantiki hiyo, Makonda amewataka kufanya usajili upya na kusajili vituo vyao ili watambulike kisheria huku akisema atawapatia mavazi maalum 'reflectors' kama utambulisho.

Awali, mmoja wa waendesha bodaboda hao, Daud Laurian alimsomea RC Makonda risala iliyoainisha matatizo yao ikiwemo zuio la ya jiji kutokana na agizo la aliyekua  mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam, Mecky Sadick Machi 3, 2014.

Waendesha hao wamehaokikishia Makonda kuwa raia wema katika suala zima la ulinzi iwapo Jeshi la Polisi Kanda Maalum litawachukulia kama ndugu zao na marafiki.

KONDAKTA ALIETISHIA KUMUUA MAGUFULI ASHTAKIWA

Kondakta wa daladala amefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu akikabiliwa na shtaka la kutishia kumuua Rais John Magufuli.

Hamim Seif (42) mkazi wa Mwananyamala Ujiji, alidaiwa kutenda kosa hilo Machi 10 mwaka huu katika baa ya Soweto, maeneo ya Makumbusho jijini Dar es Salaam.

Wakili wa serikali Keneth Sekwao aliambia mahakama Alhamisi kuwa mshtakiwa, akiwa katika baa hiyo, alitishia kumuua Dkt Magufuli kwa maneno kwa njia ya kujitoa mhanga. 

“Kwa haya mambo anayoyafanya Rais Magufuli, mimi nimo tayari kujilipua kwa kujitoa mhanga ili kumuangamiza,” alinukuliwa na Wakili Sekwao. Mshtakiwa alikana shtaka hilo 

Hakimu Mkazi, Hellen Liwa aliweka wazi dhamana ya mshtakiwa huyo na kumtaka kutafuta wadhamini wawili, kutoka taasisi ya Serikali inayotambulika, ambao watasaini hati ya dhamana ya Sh2 milioni. Alishindwa kutimiza masharti ya dhamana na akawekwa rumande hadi 14 Aprili kesi ikatapotajwa tena.

BOKO HARAM WAAPA KUTOSALIMU AMRI

 Abubakar Shekau kiongozi wa Boko Haram

 Wapiganaji wa kundi la Boko Haram wametoa kanda mpya ya video wakiapa kuendeleza vita vya kutaka uongozi wa sheria za kiislamu. 

'Lazima mujue kwamba hakuna ukweli, hakuna majadiliano,hakuna kusalimu amri'', alisema mtu mmoja aliyejifunika uso na kuzungumza kwa lugha ya hausa.

 Ujumbe huo unajiri baada ya kanda ya video isiojulikana mwezi uliopita kumuonyesha kiongozi wa Boko Haram Abubakar Shekau akionekana dhaifu swala linaloongeza uvumi kwamba mda wake katika uongozi wa kundi hilo unaelekea ukingoni.

 Katika kanda hiyo ya video kuna watu wamesimama na bunduki za AK-47 mbele ya magari.

Sunday, March 27, 2016

Tuesday, March 22, 2016

MWALIMU ANAEHITAJI KUBADILISHANA KITUO

TANGAZO: Mimi ni mwalimu wa secondary nipo halmashauri ya Tandahimba nahitaji mwalimu wa kubadilishana nae Mbeya kutoka Iringa, Morogoro, Pwani au tuwasiliane kwa no. 0655591881.

Monday, March 21, 2016

MAGUFULI ATII AGIZO LA MKUU WA MKOA, POLISI WAENDA IKULU KUHAKIKI SILAHA ZAKE





SHEIN ASHINDA URAIS KWA ASILIMIA 91.4

 
Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi Zanzibar Jecha Salim Jecha amemtangaza Rasmi Mgombea urais wa CCM Dr. Ali Mohammed Shein kuwa mshindi wa kiti cha urais wa Zanzibar akiwa na kura 299.982 sawa na asilimia 91.4.

Friday, March 11, 2016

HATIMAE MAGUFULI AWAPA SAFARI YA NJE MAWAZIRI WAWILI

Tangu Novemba 5 wakati Dk John Magufuli alipoapishwa, ni Waziri Mkuu Kassim Majaliwa na Waziri wa Mambo ya Nje, Balozi Augustine Mahiga pekee waliotoka nje ya nchi, lakini jana Rais aliwaruhusu mawaziri wengine wawili kusafiri nje.

Rais Magufuli alizuia safari za nje siku chache baada ya kuapishwa akisema watumishi wa umma watakaokuwa wakitaka kwenda nje watalazimika kuomba kibali kutoka Ikulu, ikiwa ni mkakati wake wa kudhibiti matumizi ya fedha za Serikali.

Tangu wakati huo, safari za nje kwa watumishi wa umma zimekuwa za nadra na mawaziri wamekuwa wakifanya ziara za kwenda mikoani kufuatilia utendaji na utoaji wa huduma kwa wananchi. Like page yetu ya facebook Jambo Tz

MBOWE: NAWALETEA KATIBU MKUU MAKINI

mbowe.

MWENYEKITI wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Freeman Mbowe, amevunja ukimya na kusema atawasilisha jina makini la mrithi wa nafasi ya aliyekuwa Katibu Mkuu wa chama hicho, Dk. Willibrod Slaa. 

Akizungumza mjini hapa jana, baada ya kumalizika kikao cha kwanza cha Kamati Kuu, Mbowe alisema sifa za kiongozi anayepaswa kushika wadhifa huo zinafahamika.

Alisema wajumbe na wanachama wa Chadema watarajie kumpokea mtu makini ambaye jina lake atalipendekeza kisha kupigiwa kura na wajumbe wa Baraza Kuu kesho. Like page yetu ya facebook Jambo Tz

MAGAZETI YA LEO IJUMAA MACHI 11, 2016

20160311_043412 20160311_043507 20160311_043525 
Like page yetu ya facebook Jambo Tz

Pro

PropellerAds

LinkWithin

Soma na Hizi Pia Plugin for WordPress, Blogger...