Friday, March 11, 2016

MAREKANI YAMFILISI MTANZANIA MUUZA UNGA

SHKUBA
SERIKALI ya Marekani juzi ilitangaza kutaifisha mali za bilionea Mtanzania, Ali Khatib Haji Hassan, maarufu Shikuba pamoja na mtandao wake wa kimataifa wa biashara ya dawa za kulevya.
Shikuba ambaye ni mfanyabiashara maarufu Dar es Salaam, anamiliki msururu wa biashara kama vile maduka ya kubadili fedha (bureau de change), kampuni za ulinzi, majumba na utitiri wa magari ya kifahari.

Taarifa iliyotolewa na Wizara ya Fedha ya Marekani kupitia ofisi yake ya Udhibiti wa Mali Haramu za Raia wa Kigeni (OFAC), Shikuba na taasisi yake wameangukia katika sheria za nchi hiyo za kudhibiti mapapa wa unga wa kigeni (Kingpin Act).

Mbali ya sababu za kisheria, Marekani imesema bilionea huyo amekuwa akitumia faida haramu kutokana na biashara zake chafu kuhonga maofisa wa Serikali ya Tanzania ili asikamatwe na kushtakiwa. Like page yetu ya facebook Jambo Tz

TRUMP NA RUBIO WATOFAUTIANA KUHUSU UISLAMU

Marco Rubio na Donald Trump katika mjadala
Mgombea wa urais kupitia tiketi ya chama cha Republican Marco Rubio amemshtumu Donald Trump kwa kusema kuwa Uislamu unachukia Marekani katika mjadala uliokuwa moja kwa moja runingani.

Bwana Rubio ambaye anakabiliwa na ushindani wa maisha yake katika jimbo la Florida siku ya Jumanne amesema kuwa Uislamu una tatizo la itikadi kali lakini akaongezea kuwa Waislamu wengi wanapenda Wamerekani.

''Marais hawawezi kusema kile wanachotaka ,kuna madhara'',alisema huku raia wakimpigia makofi. Wagombea hao wanne wa chama cha Republican walisikia maombi kutoka kwa viongozi wa chama hicho kuwa na mjadala wa amani.

Ikilinganishwa na mjadala uliopita ambao ulikabiliwa na na matusi ya kibinafsi mjadala huu ulikuwa na muongozo mzuri huku wagombea wote wakitoa malengo ya sera zao.

''Kufikia sasa siamini vile tumekuwa watulivu hapa'',bwana Trump alinukuliwa akisema. Lakini katika swala la Uislamu,kulikuwa na tofauti kubwa kati ya Trump na wagombea wengine huku wenzake wote wakitofautiana naye kwamba familia za magaidi ziangamizwe. Like page yetu ya facebook Jambo Tz

SIMBA YARUDI KILELENI YAINYUKA NDANDA 3-0

Pg 32
TIMU ya soka ya Simba jana ilirejea kileleni mwa msimamo wa Ligi Kuu Tanzania Bara kwa kishindo baada ya kuinyuka Ndanda FC mabao 3-0 katika mchezo uliopigwa Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
Matokeo ya ushindi wa jana yameiwezesha Simba kufikisha pointi 51 na kuwashusha mahasimu wao wa jadi Yanga hadi nafasi ya pili, wakiwa wamejikusanyia pointi 50 huku Azam FC wakibaki nafasi tatu na pointi 47.

Simba wamerejea kileleni kwa kuwazidi mahasimu wao Yanga kwa pointi moja, lakini Wanajangwani hao wapo nyuma kwa mchezo mmoja kutokana na kushuka dimbani mara 21 huku wapinzani wao wakicheza mara 22. Like page yetu ya facebook Jambo Tz

Thursday, March 10, 2016

UTUMBUAJI MAJIPU WAOKOA BILLION 700/=

KASI ya kuzuia ukwepaji kodi za Serikali uliofanywa kwa kipindi cha miezi mitatu na utawala wa Rais Dk. John Magufuli kwa ‘kutumbua majipu’ umeokoa wastani wa Sh bilioni 700.
Katika utawala wa Serikali iliyopita ya awamu ya nne, wastani wa makusanyo ya kodi kwa kiwango cha juu kwa mwezi yalikuwa Sh bilioni 900, lakini baada ya kuingia kwa awamu hii kumekuwapo na ongezeko la zaidi ya Sh bilioni 700 kwa miezi mitatu ya Desemba hadi Februari.
Akitangaza ongezeko hilo kwa waandishi wa habari Dar es Salaam jana, Kaimu Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Alphayo Kidata, alisema katika kipindi cha Desemba 2015, pia TRA iliweza kuvuka lengo kwa kukusanya kiasi cha zaidi ya Sh. trilioni 1.4 sawa na ongezeko la wastani wa Sh. bilioni 490 kwa mwezi.
Alisema kiasi hicho ni kikubwa kikilinganishwa na wastani wa makusanyo kwa mwezi Julai hadi Novemba mwaka jana ambapo ilikuwa ni Sh. bilioni 900 kwa mwezi. Like page yetu ya facebook Jambo Tz

'NITAFANYA KAZI NA ALI KIBA BILA VIKWAZO' HARMONIZE

Harmonizeff
LICHA ya tetesi kwamba wasanii wawili wa muziki wa Bongo Fleva, Ali Kiba na Nasibu Abdul ‘Diamond’, kutoonyesha nia ya kushirikiana katika muziki wao, msanii anayetamba na wimbo wa ‘Bado’, Rajabu Ibrahimu ‘Harmonize’, amesema yupo tayari kufanya kazi na Ali Kiba bila kikwazo chochote.

Msanii huyo alisema Ali Kiba ni msanii wa Tanzania na ni msanii mzuri katika muziki hivyo kufanya naye ‘kolabo’ ni kitu cha kawaida kama wasanii wengine anavyofanya nao.
“Mimi sijui kiukweli kama kuna bifu kati ya Diamond na Ali Kiba kwa sababu sijawahi kumsikia Diamond akimzungumzia Ali Kiba kwamba wana ugomvi,” alisema Harmonize.

Harmonize ambaye hivi karibuni alijinadi kutoanzisha uhusiano wa kimapenzi, anazidi kujizolea umaarufu kutokana na nyimbo zake tatu ukiwemo ‘Aiyola’, ‘Kidonda Changu’ na ‘Bado’ huku akizidi kujipanga kwa mambo mengine makubwa yatakayokuja kupitia kampuni ya wasafi anayoifanyia kazi. Like page yetu ya facebook Jambo Tz

MKWASA ATAJA SABABU ZA KUMUITA KAZIMOTO

kazimotozKOCHA mkuu wa timu ya Taifa ya soka ‘Taifa Stars’, Boniface Mkwasa, amesema uwezo mkubwa aliokuwa nao kiungo wa Simba, ndio umemfanya amuite kwenye kikosi chake kitakachocheza na Chad, Machi 23 kwenye mchezo wa kufuzu fainali za mataifa ya Afrika (Afcon), utakaochezwa mji wa Djamena, nchini Chad.

Mkwasa alimjumuisha mchezaji huyo kwenye kikosi chake hicho chenye jumla ya wachezaji 25, licha ya kuwa tayari ameshatangaza kuacha kuichezea timu ya Taifa ili kutoa nafasi kwa wachezaji wengine.

Akizungumza na mwandishi wa habari hii jana, Mkwasa alisema, Mwinyi ameonyesha mchango mkubwa kwenye timu yake ya Simba na ndio sababu iliyompelekea kumjumuisha kwenye kikosi chake ambacho kulingana na ratiba ilivyobana anahitaji kuwa na wachezaji wenye uzoefu mkubwa ili kuweza kupambana na Chad kwani hawana muda mrefu wa kujiandaa.

“Hizo taarifa za kuwa amestaafu kuichezea timu ya Taifa sijazipata hivyo haikuwa kikwazo kwangu kumuita, lakini pia bado ana kiwango kizuri ni kijana mkongwe na amekuwa na mchango mkubwa kwenye timu yake, bado ana nafasi kubwa ya kulisaidia Taifa lake,” alisema. Like page yetu ya facebook Jambo Tz

LIVERPOOL KUCHUANA NA MAN U EUROPA

Mkufunzi wa timu ya Liverpool Jurgen Klopp ameitaja mechi ya Alhamisi ya kombe la Europa kati ya Liverpool na Manchster United kuwa mechi kubwa sana.
Liverpool wanaikaribisha Anfield timu ya Manchester United ikiwa ni mkutano wao wa kwanza Ulaya.

Hatahivyo Klopp anasema :''kila siku kombe la Europa linafurahisha.Ni Mechi kubwa sana.Ijapokuwa sio kubwa zaidi katika kazi yangu kama mkufunzi wa Liverpool lakini ni muhimu sana''.

Manchester United imeshinda makombe 3 ya bara Europa hivi karibuni ikiwa 2008,huku Liverpool ikilibeba kombe hilo mara tano.

Mkufunzi wa Manchester United Louis Van Gaal amesema kuwa wale wanaomkosoa kwa kushushwa katika kombe la Europa hawaelewi huku Klopp akisema kuwa anaamini mechi hiyo itasisimua mashabiki katika uwanja wa Anfield.

Friday, March 04, 2016

MAGUFULI "MAJIPU YAKINISHINDA SINA SABABU YA KUENDELEA KUWA RAIS"

RAIS Dk. John Magufuli, amesema kama atashindwa kutumbua majipu dhidi ya wazembe na wabadhirifu serikalini, hana sababu ya kuendelea kushika wadhifa huo.

Amesema endapo hali hiyo ikitokea ni bora arudi nyumbani kwake akalale, kwa sababu lengo lake la kuwapatia wananchi Tanzania mpya, litakuwa halijatimia.

Rais Dk. Magufuli aliyasema hayo jana, wakati wa hafla ya kuweka jiwe la msingi la ujenzi wa barabara ya Arusha-Holili yenye urefu wa kilometa 234.3, itakayogharimu Sh bilioni 209.3
“Ndugu zangu kazi hii ni ngumu, wapo watu ambao hawataki mimi na Serikali yangu kuwatumbua, nitapambana hadi nihakikishe ninafanikiwa.

“Na iwapo nitashindwa hakuna sababu ya mimi kuendelea kuwa Rais wa nchi hii, ni bora nirudi nyumbani kwangu kulala,” alisema. Like page yetu ya facebook Jambo Tz

MAGAZETI YA LEO IJUMAA MACHI 04, 2016

20160304_053145
20160304_053212
20160304_053230 
Like page yetu ya facebook Jambo Tz

ALIYEDAI HAKUNA 'MUNGU' ASHITAKIWA

Mwanamume aliyeandika kwamba hakuna Mungu katika majibizano mtandaoni ameshtakiwa kusini mwa Urusi. Viktor Krasnov aliripotiwa kwa polisi na wanaume wawili waliokasirishwa na lugha aliyoitumia wakati wa majibizano katika mtandao wa kijamii wa Kirusi wa VKontakte mwaka 2014.

Mtandao huyo hufanana sana na Facebook na ni maarufu sana. Ameshtakiwa Stavropol kwa kosa la "kutusi hisia za waumini”. "Matusi” kama hayo yaliharamishwa kisheria mwaka 2013 baada ya kesi ya Pussy Riot. Wakati wa majibizano hayo, Bw Krasnov anadaiwa pia kupuuzilia mbali Biblia na kusema ni “mkusanyiko wa hadithi za kubuni za Wayahudi”.

Wataalamu wa lugha waliunga mkono msimamo wa Bw Krasnov kwamba maandishi yake yalikuwa “matusi kwa waumini” hao. Kwa mujibu wa sheria ya Urusi, akipatikana na hatia, anaweza kufungwa jela mwaka mmoja na kutozwa faini ya hadi $4,083) au kufanyishwa kazi ngumu saa 240. Like page yetu ya facebook Jambo Tz.

RATIBA YA LIGI KUU TANZANIA BARA WEEKEND HII

Wachezaji wa Timu ya Yanga
 
Ligi kuu ya Tanzania itaendelea tena mwisho wa wiki hii kwa nyasi za viwanja mbalimbali kuwaka moto. Hapo kesho katika dimba la taifa Jijini Dar es Salaam kutachezwa mchezo wa wababe wawili wa soka Azam Fc watakaowakabili vinara wa ligi hiyo Yanga.
Wachezaji wa Timu ya Simba 

Huku African Sport wakiwa nyumbani katika uwanja wa mkwakwani kukipiga na Majimaji.
Toto Africans,watakua katika uwanja wa Kirumba, kupepetana na Ndanda FC. Kagera Sugar wao watakuwa na kibarua kizito dhidi ya Mgambo JKT.

Kikosi cha JKT Ruvu kitawaalika Mwadui Fc, toka Mkoani shinyanga wakati Wajelajela wa Tanzania Prisons watakua wenyeji wa Stand United, nao wakata miwa wa Mtibwa watapimana ubavu na Coastal Union.

Jumapili utapigwa mchezo mmoja ambapo Wekundu wa Msimbazi watakuwa na kibarua kizito cha kuwakabili Mbeya City mchezo utakaochezwa kwenye uwanja wa Taifa Dar es Salaam. Like page yetu ya facebook Jambo Tz.

UGANDA NDIO TIMU BORA AFRIKA MASHARIKI

Timu ya taifa ya Uganda

Timu ya taifa ya Cape Verde 
 
Cape Verde wametua kileleni mwa orodha ya Fifa ya uchezaji kandanda barani Afrika ya mwezi Machi. Huo ni ufanisi mkubwa kwa taifa hilo linalojumuisha visiwa kadha vidogo kaskazini magharibi mwa Afrika.

Wamefanikiwa kuwapita mabingwa wa Afrika wa mwaka 2015 Ivory Coast ambao wameshuka hadi nambari mbili. Cameroon pia wameimarika, na kuingia katika orodha ya 10 bora na kuwaondoa Guinea.

Licha ya kushinda Kombe la Afrika kwa wachezaji wa ligi za ndani, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo wameshuka nafasi moja hadi nambari 58. Miongoni mwa nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki, Uganda inaongoza ikiwa nambari 67, ikifuatiwa na Rwanda (85), Kenya (103), Tanzania (125), Burundi (129) na Sudan Kusini (140). Like page yetu ya facebook Jambo Tz.

"ARSENAL HATUJIAMINI" SANCHEZ

Alexi Sanchez 
Kiungo wa kati wa Arsenal Alexis Sanchez amesema kuwa Arsenal haina imani kwamba itashinda ligi ya Uingereza baada ya kushindwa mara mbili mfululizo na Manchester United na Swansea. The Gunners walipoteza 3-2 katika uwanja wa Old Trafford na 2-1 nyumbani dhidi ya Swansea na hivyobasi kuwa pointi sita nyuma ya viongozi wa ligi Leicester.

''Mara nyingine tunakosa motisha kwamba tayari tumeshinda 1-0 tunapoelekea uwanjani'',aliiambia Directiv Sport kabla ya mechi dhidi ya United.''Tunakosa ile ari kwamba tunaweza kuwa mabingwa''. Sanchez aliongea: Iwapo tutaingia katika uwanja na ari ya kuwa mabingwa ,kushinda ligi ama hata kombe la vilabu bingwa Ulaya,tunaweza kuafikia hilo.

''Ninakumbuka mechi dhidi ya Manchester United mwaka uliopita.Wachezaji walikuwa na motisha ya kushinda taji tulipoingia uwanjani.Tuliwashinda katika dakika 20 na kupata 3-0.Tulikuwa na ari na kujiamini siku hiyo''. Arsenal imeshinda mara tatu pekee kutoka mechi 11 katika mashindano yote na wako katika nafasi ya tatu katika ligi.

Tuesday, March 01, 2016

DAKTARI ASIMAMISHWA KAZI KISA LAKI MOJA

Baada ya kufichua uozo katika bandari tatu kubwa hapa nchini, Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amehamia katika afya baada ya kumsimamisha kazi daktari wa kitengo cha upasuaji katika Hospitali ya Ligula, Fortunatus Namahala kwa madai ya kumuomba mgonjwa rushwa ya Sh100,000.

Waziri Mkuu alichukua hatua hiyo jana alipotembelea hospitali hiyo ya mkoa na kukabiliwa na Tatu Abdallah ambaye alidai kwamba alilazimika kuuza shamba lake la ekari 2.5 ili apate Sh100,000 kwa ajili ya upasuaji wa baba yake.

“Februari Mosi nilimleta baba yangu hapa nikaambiwa anatakiwa kufanyiwa upasuaji. Nikaandikiwa ninunue dawa za Sh85,000 hapo nje kwenye duka la dawa pia uzi wa kushonea kwa Sh25,000. Lakini pia daktari akasema anataka Sh100,000 ya kwake. Lakini hadi Februari 7 hakufanyiwa huo upasuaji,” alidai.

Pro

PropellerAds

LinkWithin

Soma na Hizi Pia Plugin for WordPress, Blogger...