Kiungo wa kati wa
Arsenal Alexis Sanchez amesema kuwa Arsenal haina imani kwamba itashinda
ligi ya Uingereza baada ya kushindwa mara mbili mfululizo na Manchester
United na Swansea. The Gunners walipoteza 3-2 katika uwanja wa
Old Trafford na 2-1 nyumbani dhidi ya Swansea na hivyobasi kuwa pointi
sita nyuma ya viongozi wa ligi Leicester.
''Mara nyingine tunakosa
motisha kwamba tayari tumeshinda 1-0 tunapoelekea uwanjani'',aliiambia
Directiv Sport kabla ya mechi dhidi ya United.''Tunakosa ile ari kwamba
tunaweza kuwa mabingwa''. Sanchez aliongea: Iwapo tutaingia katika
uwanja na ari ya kuwa mabingwa ,kushinda ligi ama hata kombe la vilabu
bingwa Ulaya,tunaweza kuafikia hilo.
''Ninakumbuka mechi dhidi ya Manchester United mwaka
uliopita.Wachezaji walikuwa na motisha ya kushinda taji tulipoingia
uwanjani.Tuliwashinda katika dakika 20 na kupata 3-0.Tulikuwa na ari na
kujiamini siku hiyo''. Arsenal imeshinda mara tatu pekee kutoka mechi 11 katika mashindano yote na wako katika nafasi ya tatu katika ligi.