Mgombea urais wa CCM, Dk John Magufuli akiwahutubia wananchi wa Mkoa wa Mtwara nje ya ofisi ya CCM jana. Picha na Ofisi ya CCM
Waziri wa Ujenzi na
mgombea urais wa CCM, Dk John Magufuli amesema kuwa wana-CCM mwaka huu
wanapaswa kufanya kampeni za kisayansi zaidi kuhakikisha wanapata
ushindi wa tsunami utakaowezesha kuundwa kwa Serikali imara
itakayowaletea maendeleo Watanzania wote.
Alisema kwa
kufanya hivyo kutawasaidia kupata viti vingi na kusimamia shughuli zote
za maendeleo na kwa manufaa ya wanaCCM na Watanzania wote kwani mahitaji
yao na matarajio yao ni kupata maendeleo makubwa.
“Niwaombe
wana CCM wenzangu, tushikamane tuwe wamoja. Kampeni za mwaka huu ni
lazima tufanye kampeni za kisayansi zaidi, ni lazima kampeni zianze
katika ngazi ya nyumba kumi, vitongoji kwa vitongoji, vijiji, mitaa,
kata majimbo, wilaya, mikoa na baadaye urais kwa ujumla. Katika umoja
huu nataka niwahakikishie ushindi wa mwaka huu wala si wa kimbunga, ni
wa tsunami,” alisema Dk Magufuli. Asante kwa kutembelea blog hii, endelea kuwa nasi, like page yetu ya facebook bofya neno Jambo Tz.