Sunday, July 26, 2015

14 WAFA KATIKA SHAMBULIO CAMEROON


Watu 14 wameuawa jana usiku katika shambulizi la bomu lililotekelezwa na Boko Haram

Watu 14 wameuawa jana usiku katika shambulizi la bomu lililofanyika kwenye jumba moja la starehe katika mji wa Maroua Kaskazini mwa Cameroon.

Siku chache baada ya kutokea kwa mashambulizi mawili ya bomu katika mji mkuu wa eneo hilo kulingana na habari kutoka kwa maafisa wa usalama. Afisa mmoja wa jeshi lililopelekwa katika eneo hilo kupambana na Boko Haram ndiye aliyetoa habari hiyo kwa siri.

Shambulizi hilo lilifanyika saa mbili kasorobo jana usiku saa za Afrika Mashariki wakati mwanaume mmoja alirusha bomu ndani ya baa katika wilaya ya Ponre kulingana na afisa huyo wa jeshi ambaye hakutaka kutajwa. Wakazi walijaribu kumfuata lakini aliwarushia grunedi kuwafukuza.

Afisa wa polisi aliyekuwa katika eneo hilo la tukio, amesema alihesabu miili 12 baada ya shambulio hilo. Mkazi mmoja wa mji huo anasema kuwa kulikuwa na mlipuko mkubwa ndipo baadaye wakajua ni baa kubwa inayoitwa "Boucan" ndiyo iliyokuwa imeshambuliwa. Jumatano iliyopita watu 13 waliuawawa katika mashambulizi mawili yaliyotokea wakati mmoja katika soko kuu na karibu na eneo jirani.

Mashambulizi hayo yalitekelezwa na wasichana wawili waliokuwa chini ya umri wa miaka 15. Shambulizi hilo lilikuwa la pili kwa ukubwa katika eneo hilo ndani ya siku kumi licha ya kuwa na kampeni kali za kukabili Boko Haram ambalo linaendelea kuwa tishio la usalama katika eneo la Ziwa region.

Siku ya Jumamosi watu 25 waliuawa katika mashambulizi mengine yanayoaminika kutekelezwa na wanamgambo wa Boko Haram kaskazini magharibi mwa Nigeria, huku wakaazi wengi wakilazimika kuhama makwao. Kwa miaka miwili iliyopita kundi hilo limekuwa likifanya mashambulizi katika eneo la mpakani mbali na utekaji nyara kaskazini mwa Cameroun.

Aidha nchi hiyo ambayo ilikuwa imejitolea kuongeza jitihada za kupambana na kundi hilo haikuwa ikishambuliwa na walipuaji wa kujitolea muhanga. Muungano wa wanajeshi wa nchi tano kutoka Nigeria, Niger, Chad, Cameroon na Benin utatumwa kukabiliana na kundi hilo linalohusiana na lile la Islamic State. Kuwepo kwa wapiganaji hao kwa miaka sita umesababisha vifo vya watu 15,000 na tishio kubwa zaidi la usalama katika kanda hiyo.

No comments:

Pro

PropellerAds

LinkWithin

Soma na Hizi Pia Plugin for WordPress, Blogger...