Wednesday, June 17, 2015
SERIKALI YA MUUNGANO WA PALESTINA KUVUNJIKA
Rais wa Palestina amesema kuwa serikali ya muungano kati yake na wanamgambo wa Hamas itavunjika.
Bwana
Mahmud Abbas ameliambia vuguvugu lake la Fatah, kuwa lazima uhusiano
huo uvunjike kwa kuwa Hamas haitairuhusu serikali yake kuendesha
shughuli katika eneo la Gaza, ambako wameshikilia wao.
Serikali hiyo iliundwa mwaka
uliopita na ilitarajiwa kumaliza uhasama kati ya makundi hayo mawili
lakini malengo yake yamekumbwa na matatizo mengi.
Hamas wanaongoza Gaza ilhali kundi la bwana Abbas la Fatah limeshikilia maeneo ya wa Palestina ya West Bank.
Je unahitaji kununua gari kwa bei nafuu, bofya hapa au tuambie unataka gari gani na ya bei gani tukutafutie haraka.
OPERATION ZA UN ZIFANYIWE MABADILIKO
Ripoti
iliyoandaliwa kwa hisani ya umoja wa mataifa imeelezea kuwa oparesheni
za kulinda usalama za shirika hilo zinahitaji kufanyiwa mabadiliko
makubwa.
Ripoti hiyo imekusanywa baada ya madai kutolewa hivi
karibuni dhidi ya vikosi vya umoja huo vya kulinda amani kwamba baadhi
wamekuwa wakiwanyanyasa kingono watoto wadogo.
Miongoni mwa
mapendekezo ya ripoti hiyo ni kuwa nchi ambako maafisa husika wanatoka,
zisikubaliwe kuchangia tena wanajeshi katika vikosi vya umoja wa
mataifa.
Pia ripoti hiyo inasema kuwa wanajeshi waliotajwa
kuhusika na uovu huo wanastahili wakabiliwe na sheria, na nchi zao pia
zinafaa kushurutishwa kueleza wazi ni hatua zipi za adhabu
zilizochukuliwa dhidi yao.
Pendekezo jingine lililotolewa katika
ripoti hiyo ni kuwa madai yote ya unyanyasaji wa ngono yanastahili
kufanyiwa uchunguzi wa kina kwa chini ya miezi sita.
Je unahitaji kununua gari kwa bei nafuu, bofya hapa au tuambie unataka gari gani na ya bei gani tukutafutie haraka.
RATIBA YA MECHI ZA EPL YATOLEWA
Chelsea
itaanza utetezi wa taji la ligi ya Uingereza wakati itakapoikaribisha
nyumbani Swansea katika wikiendi ya tarehe 8-9 mwezi Agosti.
Manchester
City iliomaliza pointi nane nyuma ya Chelsea itaelekea West Bromwich
huku Manchester United ikikabiliana na Tottenham katika uwanja wa Old
Trafford.
Arsenal itaialika West Ham
,Liverpool ikienda Stoke,Newcastle itakabiliana na Southampton huku
Leicester ikiialika Sunderland nyumbani.
Bournemouth iliopandishwa daraja,Watford na Norwich zitakabiliana na Aston Villa,Everton na Crystal Palace mtawalia.
Msimu huu utanza wiki moja mapema ikilinganishwa na msimu uliopita. Je unahitaji kununua gari kwa bei nafuu, bofya hapa au tuambie unataka gari gani na ya bei gani tukutafutie haraka.
MAN CITY YATOA MILIONI 35 KUMNUNUA STERLING
Klabu ya Manchester City imeimarisha ombi la kumsajili mashambulizi machachari wa Liverpool Raheem Sterling.
Mabingwa hao wa mwaka wa 2014 wametoa pauni milioni 35 sawa na dola milioni 55 kusajili huduma za mshambulizi huyo.
The Reds walikataa ombi la kwanza la kumsajili kiungo huyo mwenye umri wa miaka 20 wakisema thamani yake ni pauni milioni 50.
Kuwepo kwa mchezaji huyo raia wa Uingereza katika soko kumetokana na nia yake ya kuondoka Liverpool .
Hata hivyo alizua mjadala baada ya kuzima pendekezo la nyongeza ya mshahara wake hadi pauni laki moja kwa wiki.
Manchester City inaaminika kuwa iko tayari kutoa marupurupu mengine yatakayofikisha gharama yake hadi pauni milioni 40 japo wanalalamika kuwa Liverpool imeongeza maradufu thamani yake ikifahamika kuwa wenyewe hawakuwa hata wakimlipa pauni laki moja kwa juma.
Kwa upande wake kocha Brendan Rodgers anashikilia kukutu kuwa anamtarajia Sterling kusalia Anfield hadi kandarasi yake itakapokatika.

Tuesday, June 09, 2015
WAGOMBEA URAIS VIKUMBO KILA KONA
MAKADA wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) waliotangaza nia ya kugombea urais, sasa ni wazi wanapigana vikumbo kila kona ya nchi.
Hatua hiyo inatokana na kila mtangaza nia kwa nyakati tofauti kutoa kauli nzito.
Wapo makada ambao kauli zao zinaonyesha wazi kuwa kuna mgongano ndani ya
CCM, huku wengine wakitangaza nini watakifanya endapo watateuliwa
kuongoza nchi.
MEMBE: SINA UNDUGU NA JK
WAZIRI wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bernard Membe, amesema hana undugu na Rais Jakaya Kikwete.
Membe ambaye pia ni Mbunge wa Mtama, alikanusha undugu wake na Rais
Kikwete mjini Dodoma jana wakati akizungumza na waandishi wa habari
baada ya kuchukua fomu ya kuomba kuwania urais kupitia CCM. Nunua gari kwa bei rahisi bofya hapa. Pia tangaza biashara yako hapa kwa bei nafuu zaidi, na usisahau ku-Like Ukurasa Wetu Wa Facebook Kwa Kubofya/ Click Neno Jambo Tz.
WATOTO KUNUFAIKA NA DAWA MPYA ZA ARV
Watoto
walioathirika na Virusi vya Ukimwi watanufaika kutokana na uamuzi wa
mamlaka ya Chakula na Dawa ya Marekani kuidhinisha dawa mpya ambazo
zinaweza kuchanganywa kwenye Chakula ili kuwarahisishia matumizi watoto
wanaoishi na virusi vya ukimwi.Shirika la Umoja wa Mataifa la
kushughulikia Ugonjwa wa Ukimwi ,UNAIDS na Shirika linalohudumia watoto
duniani, UNICEF yameeleza.
Mkurugenzi mtendaji wa UNAIDS, Michel
Sidibe' amesema kuwa dawa hizi ni mbadala wa zile ambazo zilikuwa
hazifurahiwi na watoto, zenye ladha mbaya.Dawa hizi zitawawezesha watoto
kuzidi kupata tiba nzuri na kuwafanya watoto wawe na afya, amesema
haikubaliki kuwa asilimia 24 pekee ya watoto walioathirika wapate dawa
za kupunguza makali.
Dawa hizi zimetengenezwa nchini India, zina
viambata vya Lopinavir na ritonavir ambazo zinaweza kuchanganywa kwenye
chakula cha mtoto.Dawa hizi haziharibiwi na joto la chakula na zina
ladha nzuri kuliko zinazopatikana sasa, vidonge hivi vinafaa kwa
matibabu kwa watoto.
Hii ni hatua mpya katika mipango ya kuokoa
maisha ya Watoto waishio na virusi vya ukimwi, Mkurugenzi wa Mradi wa
Ukimwi wa UNICEF,Craig McClure amesema '' tunatarajia kuimarisha
upatikanaji wa matibabu kwa ajili ya watoto wengi zaidi na kuunga mkono
mpango wa kuwafikia watoto wasiopata huduma hii duniani kote''. Nunua gari kwa bei rahisi bofya hapa. Pia tangaza biashara yako hapa kwa bei nafuu zaidi, na usisahau ku-Like Ukurasa Wetu Wa Facebook Kwa Kubofya/ Click Neno Jambo Tz.
UZI MPYA WA ARSENAL 2015/16 HUU HAPA...!!!
Kwa wale wanaojiuliza ni lini Arsenal watatoa jezi zao mpya za Puma kwa ajili ya msimu wa 2015/2016, jibu hili hapa.
Jezi za nyumbani za Arsenal
zitakazotumika msimu ujao wa 2015/2016 zimevuja….hivyo mashabiki wa
London na duniani kote wajiandae kupata mzigo mpya.
Cheki uzi mpya wa nyumbani wa Arsenal chini;
OSCAR PISTORIOUS KUACHILIWA, AUGUST
Wakuu
wa magereza Nchini Afrika Kuisini wamesema kuwa Oscar Pistorius,
ataachiliwa kutoka gerezani mwezi Agosti mwaka huu miezi kumi baadaye,
ili atumikie kifungo cha nje, cha hukumu aliyopewa ya miaka mitano.
Bingwa
huyo wa nishani ya dhahabu katika mbio za Olimpiki, alikutwa na hatia
ya kumpiga risasi bila ya kukusudia na kumuuwa mpenziwe, Reeva
Steen-kamp,
na kumuuwa mwana mitindo huyo.
Mahakama kuu
Nchini Afrika Kusini mwezi Novemba mwaka huu, itasikiliza rufaa ya
waendesha mashtaka ya kujaribu kupunguza makali ya hukumu iliyotolewa
dhidi ya mwanariadha huyo mlemavu. Nunua gari kwa bei rahisi bofya hapa. Pia tangaza biashara yako hapa kwa bei nafuu zaidi, na usisahau ku-Like Ukurasa Wetu Wa Facebook Kwa Kubofya/ Click Neno Jambo Tz.
Sunday, June 07, 2015
WAGOMBEA URAIS CCM WAWANUFAISHAUKAWA
Dar es Salaam. Baada ya wiki nzima ya makada wa
CCM kutangaza nia na hatimaye kuchukua fomu za kugombea urais, wapinzani
ndio wanaonekana kunufaika zaidi kutokana na wengi kutumia hotuba zao
kuelezea udhaifu wa kila mmoja.
CCM imepanga mwezi mzima, kuanzia Juni 3 hadi Julai 2 kuwa ni muda wa makada wake kuchukua na kurudisha fomu kabla ya vikao vya juu vya chama hicho kukutana kuanzia Julai 12 kuchuja wagombea na baadaye kumpata mmoja atakayesimama kwenye Uchaguzi Mkuu kupambana na wa vyama vingine.
Tayari makada 15 wameshachukua fomu na wengine wanaendelea kuchukua, huku waliochukua wakiwa wameshaanza kuzunguka mikoani kutafuta wadhamini 30 kila mkoa ili kupata idadi ya wadhamini 450. Wanatakiwa kupata wadhamini kwenye mikoa 15, kumi ya Bara na mitano ya Zanzibar. Nunua gari kwa bei rahisi bofya hapa. Pia tangaza biashara yako hapa kwa bei nafuu zaidi, na usisahau ku-Like Ukurasa Wetu Wa Facebook Kwa Kubofya/ Click Neno Jambo Tz.<

MSAFARA WA MAKONGORO NYERERE WAPATA AJALI
Akitoa taarifa za ajali hiyo, kamanda wa polisi wa
Mkoa wa Kigoma, Ferdinand Mtui alisema ajali hiyo ilihusisha gari aina
ya Toyota Land Cruiser lililokuwa linaendeshwa na Julius Kambarage
Nyerere ambalo lilipinduka saa 4:30 lilipofika eneo la Mwilamvya na
kujeruhi watu watano.
SOMA MAGAZETI YA LEO JUMAPILI JUNI 07, 2015 YA DINI, MICHEZO NA HARD NEWS
NYAMA YA PUNDA YASINDIKWA NCHINI...!!!
SERIKALI imekiri kuruhusu uanzishwaji wa kiwanda cha kusindika nyama ya punda kilichopo mkoani Dodoma.
Imekiri hivyo baada ya Mbunge wa Ole, Rajab Mbarouk Mohamed (CUF), kuibua hoja hiyo juzi (ijumaa) jioni wakati wa kupitisha makadirio ya bajeti ya Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii kwa mwaka wa fedha 2015/2016.
Katika hoja yake, alitaka kujua juhudi zilizofanywa na Mamlaka ya Chakula, Dawa na Vipodozi (TFDA), kukagua viwanda vya usindikaji wa chakula ikiwa ni pamoja na kiwanda hicho. Nunua gari kwa bei rahisi bofya hapa. Pia tangaza biashara yako hapa kwa bei nafuu zaidi, na usisahau ku-Like Ukurasa Wetu Wa Facebook Kwa Kubofya/ Click Neno Jambo Tz.

Subscribe to:
Posts (Atom)