Mwenyekiti wa Jumuiya ya Kikristo Tanzania (CCT), Askofu Dk Alex Malasusa
Jukwaa la Wakristo Tanzania
limewataka waumini wake kujiandikisha kwa wingi katika Daftari la Kudumu
la Wapigakura, kuisoma Katiba Inayopendekezwa na kujitokeza kuikataa
kwa kupiga kura ya “hapana”.
Taarifa iliyotolewa na Jukwaa hilo jana na
kusainiwa na mwenyekiti wa Jumuiya ya Kikristo Tanzania (CCT), Askofu Dk
Alex Malasusa, mwenyekiti wa Baraza la Maaskofu wa Kanisa Katoliki
Tanzania (TEC), Askofu Tarcisius Ngalalekumtwa na mwenyekiti wa Kanisa
la Pentekoste Tanzania (CPCT), Askofu Daniel Awet, imetaja sababu mbili
za uamuzi wake kuwa ni muswada wa Mahakama ya Kadhi kukiuka misingi ya
Taifa kuwa na Serikali isiyo na dini, na Kura ya Maoni kusababisha
mgawanyiko.
“Hivyo basi, Jukwaa linawataka waumini wake wote
wajitokeze kwa wingi kujiandikisha katika Daftari la Kudumu la Wapiga
Kura, waisome Katiba Inayopendekezwa na kushiriki kikamilifu vipindi vya
elimu juu ya Katiba Inayopendekezwa na kisha wajitokeze kwa wingi
kupiga kura ya hapana kwa Katiba Inayopendekezwa kwa sababu zilizotajwa
hapo juu,” linasema tamko hilo la kurasa nne.Tangaza biashara yako hapa kwa bei nafuu zaidi, pia usisahau ku-Like Ukurasa Wetu Wa Facebook Kwa Kubofya/ Click Neno Jambo Tz.