Rais Jakaya Mrisho Kikwete akizungumza na kuwafariji waathirika wa Mvua
ya Mawe,iliyonyesha hivi karibuni katika Kijiji cha Mwakata,Wilayani
Kahama Mkoa wa Shinyanga.
Rais Jakaya Kikwete amesema Serikali
itajenga nyumba 403 ambazo zimebomolewa na mvua kubwa iliyonyesha wiki
iliyopita katika kijiji cha Mwakata wilayani Kahama na kusababisha watu
649 kukosa mahali pa kuishi.
Kauli hiyo aliitoa jana kwenye kijiji cha Mwakata
baada ya kutembelea eneo lililoathiriwa na mvua hiyo na kujionea maisha
duni wanayoishi watu hao.
Akizungumza na wananchi waliohudhuria mkutano wake
Rais Kikwete alisema Serikali iko pamoja na wananchi hao na
itahakikisha makazi yao yanarejea katika hali yake ya kawaida kwa
kuwajengea nyumba hizo.
Pia,
Rais Kikwete aliagiza Jeshi la Kujenga
Taifa(JKT) wajenge nyumba hizo bila kupitia mkandarasi yeyote kama vile
ulivyo ujenzi wa Serikali kwa kuwa ujenzi wa jeshi unaisha kwa muda
mfupi na hakuna uchakachuaji. Tangaza biashara yako hapa kwa bei nafuu
zaidi, pia usisahau ku-Like Ukurasa Wetu Wa Facebook Kwa Kubofya/ Click
Neno Jambo Tz.