Mamia
ya raia wa nchini Haiti wameandamana katika mitaa ya Port-au-Prince
wakishinikiza Rais Michel Martelly kuondoka madarakani.
Hata hivyo
maandamano hayo yamegeuka vurugu baada polisi kutumia mabomu ya mchozi
kuwatawanya waandamanaji hao. polisi wamepambana na waaandamanaji hao
ambao wamekuwa wakirusha mawe na kuchoma moto matairi mitaani.Madai ya raia hao ni kumtaka Rais Martelly kuitisha uchaguzi na kuunda serikali,ambapo uchaguzi ulitakiwa kuitishwa miaka mitatu iliyopita.
Waziri mkuu wa Haiti Laurent Lamothe, siku ya jumapili aliamua kuachia ngazi baada ya shinikizo la siku mbili.Maoni kutoka vyama vya upinzani ni kwamba wanamtaka rais Martelly kujiuzulu. Awali Waziri wa mambo ya nje wa Marekani John Kerry ameitaka Hait kuitisha uchaguzi mara moja.
Asante kwa kutembelea blog hii ya Jambo Tz, ili kuboresha blog yetu tunatoa fulsa ya kutangaza matangazo mbalimbali na pia kutoa maoni yako kupitia namba ya simu (WhatsApp & SMS) 0715 221198, E-mail jambotz8@gmail.com. Merry Chistmass & Happy New Year.
Na BBC