Simon Sserunkuma
Mshambuliaji huyo raia wa Uganda alikuja nchini na timu ya Express ya
nchini humo na kucheza mechi mbili za kirafiki dhidi ya Simba na Yanga
na ndipo viongozi hao wa Yanga walipomwona na kumleta nchini ili kufanya
naye mazungumzo lakini mambo yakawa tofauti kwani alitoroshwa kimya
kimya na kupelekwa Zanzibar ambako Simba iliweka kambi kujiandaa na
mechi ya Nani Mtani Jembe iliyochezwa juzi Jumamosi.
ACHANA na Yanga kufungwa mabao 2-0 na Simba katika mechi ya Nani Mtani
Jembe, imebainika kuwa Simba iliifanyia Yanga umafia kwa mchezaji Simon
Ssrenkuma baada ya kumtorosha kutoka mikononi mwa viongozi wa klabu hiyo
na kwenda kumficha kwenye kambi ya timu hiyo visiwani Zanzibar wiki
iliyopita.
Asante kwa kutembelea blog hii ya Jambo Tz, ili kuboresha blog yetu tunatoa fulsa ya kutoa maoni kupitia namba ya simu (WhatsApp & SMS) 0715 221198, E-mail jambotz8@gmail.com. Merry Chistmass & Happy New Year.
Asante kwa kutembelea blog hii ya Jambo Tz, ili kuboresha blog yetu tunatoa fulsa ya kutoa maoni kupitia namba ya simu (WhatsApp & SMS) 0715 221198, E-mail jambotz8@gmail.com. Merry Chistmass & Happy New Year.
Mshambuliaji huyo raia wa Uganda alikuja nchini na timu ya Express ya
nchini humo na kucheza mechi mbili za kirafiki dhidi ya Simba na Yanga
na ndipo viongozi hao wa Yanga walipomwona na kumleta nchini ili kufanya
naye mazungumzo lakini mambo yakawa tofauti kwani alitoroshwa kimya
kimya na kupelekwa Zanzibar ambako Simba iliweka kambi kujiandaa na
mechi ya Nani Mtani Jembe iliyochezwa juzi Jumamosi.
Simon ambaye ni mdogo wa Dann Sserunkuma anayeichezea Simba pia,
aliliambia Mwanaspoti kuwa viongozi wa Yanga ndiyo waliyeongea naye kwa
ajili ya kumsajili na alikuja nchini ili kuzungumza nao lakini
alishangaa kujikuta akipelekwa kwenye kambi ya Simba visiwani Zanzibar.
“Kusema kweli nilikuja hapa kwa ajili ya kufanya mazungumzo na Yanga na
ndiyo walionileta, nilishangaa kujikuta niko kwenye kambi ya Simba,
sijui ni kitu gani kilitokea,” alisema Simon.
Mbali na hilo mshambuliaji huyo aliongeza kuwa anafurahi kuwa amejiunga
na kikosi cha Simba kwani kina wachezaji wengi vijana kuliko kile cha
Yanga kilichojaa wachezaji ambao wamecheza muda mrefu.
“Nafurahi kuwa nimeingia kwenye kikosi chenye damu changa nyingi, ni
rahisi kutengeneza kombinesheni hapa kuliko kwenye kikosi cha Yanga,
nafikiri nitafanya makubwa hapa,” alisema Simon.
Katika mchezo wa juzi, Sserunkuma alifanya vizuri na kuzima kabisa
harakati za Yanga za kupata ushindi katika mchezo huo wa pili wa Nani
Mtani Jembe. Asante kwa kutembelea blog hii ya Jambo Tz, ili kuboresha blog yetu tunatoa fulsa ya kutoa maoni kupitia namba ya simu (WhatsApp & SMS) 0715 221198, E-mail jambotz8@gmail.com. Merry Chistmass & Happy New Year.
Na Mwanaspoti
No comments:
Post a Comment