Hivi
karibuni tumesikia Mlipuko wa Ugonjwa Hatari wa Ebola ambapo tayari
umesharipotiwa kuua zaidi ya watu 1000 huko Guinea, Siera Lione, Liberia
...Na Juzi umeripotiwa Kuingia Nigeria......na Mpaka Sasa watu
takribani 1750 wameripotiwa kuathirika na Ugonjwa huu.
SASA TUJIFUNZE KIDOGO
Ebola Ni Nini?
Ebola
ni ugonjwa wa Mlipuko ambao virusi vyake hushambulia mfumo wa Damu wa
Binadamu. Kwa Lugha ya Kisayansi Ebola huitwa haemorraghic fever,
Ugonjwa huu hupelekea Muathirika kuvuja damu sehemu karibu sehemu yoyote
ile ya mwili wake na hatimaye kusababisha kifo kutokana na muathirika
huyo kupoteza damu nyingi. Na Kuvuja Damu huko kunaweza kuwa ni ndani ya
Mwili au Nje ya Mwili.
Dalili
za Ugonjwa Wa Ebola huanza kuonekana siku mbili hadi wiki tatu mara
baada ya mtu kuambukizwa virusi hivyo na Kupelekea Homa, Muscle kuuma
pamoja na Kichwa Kuuma huku dalili zingine zikiwa ni Kutapika, kuharisha
kukifuatiwa sambasamba na Kupungua kwa ufanyaji kazi wa Ini na Figo
katika Mwili wa Binadamu.
Virusi Vya Ebola vinaweza kupatikana kwa kugusa damu au majimaji kwenye mizoga ya Wanyama hususani Nyani na Popo. Kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa ku-Like page yetu ya facebook kwa ku-click/ bofya neno Jambo Tz