Mmiliki
wa Manchester United, Malcom Glazer amefariki dunia akiwa na umri wa
miaka 85, na kuacha umiliki wa klabu hiyo kwa watoto wake sita.
Familia ya bilionea huyo iliinunua Man United kwa
gharama ya Euro 790 milioni Mei, 2005 licha ya pingamizi kali kutoka kwa
mashabiki wa klabu hiyo. Hata hivyo, chini ya umiliki wake
uliosababisha deni kubwa kwa klabu hiyo ‘’the Red Devils’’ walishinda
taji la Ligi Kuu mara tano na Ligi ya Mabingwa 2008.
Watoto wa Mmarekani huyo waliozaliwa Marekani
Byan, Joel, na Avram wote wamejumuishwa katika bodi ya klabu hiyo, huku
Joel na Avram wakiwa wenyekiti wenza.
Kifo cha Glazer hakitarajiwi kuathiri umiliki wa
Man United, kwani familia hiyo bado inamiliki asilimia 90 za hisa za
klabu hiyo.
Asilimia 10 inayosalia inamilikiwa na wenye hisa
katika soko la hisa la NY stock Exchange. Glazer alikuwa pia mmiliki wa
Tampa Bay Buccaneers, iliyobadili sura ya kandanda ya Marekani kwa
kushinda taji la Super Bowl. Tafadhari Like Ukurasa Wetu Wa Facebook Kwa Kubofya/ Click Neno Jambo Tz
Bilionea huyo ambaye hakuwahi kukanyaga uwanjani
Old Trafford kutokana na hofu ya kuwaudhi mashabiki wa timu hiyo ambao
walikuwa wanamsuta kwa kupanga njama ya kuinunua klabu hiyo kwa kutumia
madeni.