Wassira alitoa kauli hiyo bungeni jana wakati
akijibu hoja za wabunge mbalimbali akiwamo Mbunge wa Kawe (Chadema),
Halima Mdee kuwa majadiliano ndani ya Bunge la Katiba yanakiuka Sheria
ya Mabadiliko ya Katiba.
Katika mchango wake, Mdee alisema Ukawa hawako
tayari kurejea ndani ya Bunge Maalumu la Katiba Agosti, mwaka huu endapo
majadiliano ya Katiba hiyo hayatajikita kwenye Rasimu ya Pili ya
Katiba.
Hata hivyo, Wassira akijibu kauli hiyo ya Mdee na
wabunge wengine waliopaza sauti kuhusu kukiukwa kwa sheria hiyo alisema:
“Kama hamrudi tutatumia kanuni zile kutafuta akidi na Bunge
litaendelea.”
“Tusigeuze Bunge hili kuwa Bunge la Katiba… Bunge
la Katiba lipo tena lipo kisheria…. Kuna watu wanageukageuka wanasema
sheria ilivunjwa, lakini hawasemi kifungu gani kilivunjwa,” alisema
Wassira. Tafadhari Like Ukurasa Wetu Wa Facebook Kwa Kubofya/ Click Neno Jambo Tz